safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Kama una laki moja yako usiipeleke msikitini/kanisani kwanza fikiria mama yako hana shida binafsi ambazo anaweza kutatua kwa pesa hiyo?
Baba je?
Ndugu wengine wa karibu?
Kuna watu wazazi wao wanahangaika kutafuta ugali wa siku mtu ile package ya kula wiki hana lakini mtu huyu anachukua pesa anapeleka kwenye nyumba ya ibada.
Mungu anakuona aisee, hautaadhibiwa na Mungu kwa nini pesa yako ulimpa mzazi akatatue shida zake wakati nyumba ya ibada haijapigwa rangi n.k
Lakini Mungu anaweza kukutia adabu kwa nini mzazi wako alilala njaa wakati wewe ulipeleka pesa kwingine.
Lengo la sadaka ni kuwasaidia wasiojiweza, sasa kama mzazi wako naye hajiwezi msapoti.
Kuna kitabu nilikichungulia kinasema toa walau 10% ya kipato chako ukatoe sadaka.
Niliamua tu sadaka yangu hiyo 10% nawapa wazazi. Sina maana ya kukosoa sadaka lakini nakumbusha tu wazee wetu wana dhiki nyingi, tusijifanye wema sana kwenye nyumba za ibada wakati wazee wetu hilo salio lingewasaidia.
Wema, sadaka huanzia nyumbani kwa watu wako wa karibu.
NB ; Kama wazazi wako wanajiweza hii mada haikugusi