keynessian
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 590
- 419
Sadaka ni sehemu ya ibada
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama kweli una Imani kweli na Mungu wako, wewe toa kunako husika, kumpa mzazi wako ni jukumu lako pia, watakao kula hiyo hela watakutana na Mungu wao. Usiingie kwenye mtego wa ibilisi na malaika zake.Kama una laki moja yako usiipeleke msikitini/kanisani kwanza fikiria mama yako hana shida binafsi ambazo anaweza kutatua kwa pesa hiyo ?
Baba je ?
Ndugu wengine wa karibu ?
Kuna watu wazazi wao wanahangaika kutafuta ugali wa siku mtu ile package ya kula wiki hana lakini mtu huyu anachukua pesa anapeleka kwenye nyumba ya ibada.
Mungu anakuona aisee,hautaadhibiwa na Mungu kwa nini pesa yako ulimpa mzazi akatatue shida zake wakati nyumba ya ibada haijapigwa rangi n.k
Lakini mungu anaweza kukutia adabu kwa nini mzazi wako alilala njaa wakati wewe ulipeleka pesa kwingine.
Lengo la sadaka ni kuwasaidia wasiojiweza,sasa kama mzazi wako naye hajiwezi msapoti.
Kuna kitabu nilikichungulia kinasema toa walau 10% ya kipato chako ukatoe sadaka.
Niliamua tu sadaka yangu hiyo 10% nawapa wazazi.sina maana ya kukosoa sadaka,lakini nakumbusha tu wazee wetu wana dhiki nyingi tusijifanye wema sana kwenye nyumba za ibada wakati wazee wetu hilo salio lingewasaidia.
Wema,sadaka huanzia nyumbani kwa watu wako wa karibu.
NB ; kama wazazi wako wanajiweza hii mada haikugusi
Maarifa anayo sana tuHuna maarifa mtoa mada
Imeandikwa Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Nanyi mwasema tumekuibia nini? Mmeniibia ZAKA NA DHABIHU.."LETENI ZAKA NA SADAKA GHALANI, KIWEMI CHAKULA NYUMBANI MWANGU ASEMA BWANA" (Malaki 3)Hata hiyo ya kanisani itaenda kutumiwa hivyo nayo ni matumizi.
Sadaka ni neno tu lakini lengo ni moja kufanya matumizi.
Katika mfumo wa matumizi ni kitu kimoja.Ni tofauti
Kama una laki moja mzazi anashida na nyumba ya ibada inataka bati ukimpa mzazi wako ndio solution bora zaidi.Kama kweli una Imani kweli na Mungu wako, wewe toa kunako husika, kumpa mzazi wako ni jukumu lako pia, watakao kula hiyo hela watakutana na Mungu wao. Usiingie kwenye mtego wa ibilisi na malaika zake.kama una
Kumpa mzazi hela hiyo sio sadaka bali ni wajibu wako hivyo ni kama matumizi yakoKama una laki moja yako usiipeleke msikitini/kanisani kwanza fikiria mama yako hana shida binafsi ambazo anaweza kutatua kwa pesa hiyo?
Baba je?
Ndugu wengine wa karibu?
Kuna watu wazazi wao wanahangaika kutafuta ugali wa siku mtu ile package ya kula wiki hana lakini mtu huyu anachukua pesa anapeleka kwenye nyumba ya ibada.
Mungu anakuona aisee, hautaadhibiwa na Mungu kwa nini pesa yako ulimpa mzazi akatatue shida zake wakati nyumba ya ibada haijapigwa rangi n.k
Lakini Mungu anaweza kukutia adabu kwa nini mzazi wako alilala njaa wakati wewe ulipeleka pesa kwingine.
Lengo la sadaka ni kuwasaidia wasiojiweza, sasa kama mzazi wako naye hajiwezi msapoti.
Kuna kitabu nilikichungulia kinasema toa walau 10% ya kipato chako ukatoe sadaka.
Niliamua tu sadaka yangu hiyo 10% nawapa wazazi. Sina maana ya kukosoa sadaka lakini nakumbusha tu wazee wetu wana dhiki nyingi, tusijifanye wema sana kwenye nyumba za ibada wakati wazee wetu hilo salio lingewasaidia.
Wema, sadaka huanzia nyumbani kwa watu wako wa karibu.
NB ; Kama wazazi wako wanajiweza hii mada haikugusi
Sijui kama umeelewa baba Mchungaji,issue ni hivi, kama mama yako,baba,kaka,mjomba,jirani nk ana uhitaji wa msingi halafu wewe ukaachana nao na kuamua kupeleka amana yako kwa prophet bilionea au bilionea gwajima siku Mungu akikutia kwapani utakula makwenzi ya kutosha baba mtumishi,lakini we endelea tu kupiga mluzi ili mbwa wajilete wamezwe!Kama watoto wameshafariki, then huyo mzazi atasaidiwa na nani? Maana kila mtoto atakuwa 'preoccupied' na mzazi wake tu. Hivyo, kuna umuhimu wa kujua kwamba kutoa sadaka kanisani (bila kulalamika) maana yake ni kumsaidia kila mtu mwenye shida even if huyo mtu hawezi kusaidiwa na ndugu zake. We have to learn to give as it is only through giving that we can receive abundantly. As for me, nimesoma kwa kusaidiwa na watu nje ya familia yangu (na kutokana na kusaidiwa niliwezeshwa kufika nchi zifuatazo nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Zambia, Malawi, Uingereza, Ireland, France, Poland, Kenya, Msumbiji, South Africa - so much so that kama nisingesaidiwa hata nisingeweza kutoka nje ya wilaya yangu) na mimi nimejifunza umuhimu wa kuguswa na shida za wengine, hasa wale wanaohitaji kusaidiwa na mtu anayeweza kufanya hivyo kwa muda huo. God rewards our generosity and kindness in ways that may be unfamiliar to us. So, usidanganyike!
Mbona zilipoanzia dini wao sio mafukara shida ni dini au mtu.Dini zinafukarisha watu zaidi kuliko kuwaisaidia.
Angalia moyo wako na utafakari ndiko hazina yako ilipo!Kama una laki moja mzazi anashida na nyumba ya ibada inataka bati ukimpa mzazi wako ndio solution bora zaidi.
naona bwana gwajiboy umetoa povu!Huna maarifa mtoa mada
Kuyajua haya mpaka uanze kufundishwa ukiwa mdogo, kamawazazi wenyewe ndiyo hao sijui watoto wao watakuwaje!Kumpa mzazi hela hiyo sio sadaka bali ni wajibu wako hivyo ni kama matumizi yako
Sadaka zinazotolewa kanisani ni kwa mujibu wa maamrisho ya Mungu mwenyewe hapewi mzazi bali wanapewa makuhani mzazi sio kuhani zipo
1) Sadaka za Mguso hizi ni za hiari wanaweka chombo mbele unaenda kutoa mwenyewe kwa hiari
2) ZAKA hizi unatoa sehemu ya 10 kwa mwaka unapeleka kwa makuhani anapewa kuhani si mzazi wako
3) MAVUNO kumtolea Mungu shukrani kama ilivyokuwa inafanyika nyakati za agano la kale anapewa kuhani si mzazi wako
4) MALIMBUKO hutoa sehemu ya kwanza ya tunda la kwanza anapewa kuhani si mzazi wako
5) MICHANGO KWA MAHITAJI MAALUMU hii huwezi kukwepa ujenzi, n.k