Basi, ni kweli mkuu hapo ndipo tunapotofautiana na tukubaliane kutoufautiana. Mimi na wengine wenye imani kama yangu wanaamini sadaka wanayotoa ni kwa ajili ya kufanya kazi ya kueneza neno la Mungu. Watu wengi wanapolijua na kulishika neno la Mungu basi furaha kubwa inakuwapo katika jeshi la Mungu
Luka 15:7-10
7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
8 Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
9 Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.