Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nama hao ndo niliowakusudia.Umeomgea ukweli mtupu...
Unakuta jitu kwao shida tupu, wazazi anawalaza njaa, pesa yote anakimbiza kutoa sadaka... anachopata huko hakuna...
Unataka walawi wakale wapi?mana maandiko walawi walipewa kazi ya kuhudumu kwenye hekalu...pia hawakupewa urithi kati ya makabila ya wana wa Israel.Ukigundua nyumba za ibada ni biashara, hakika utawapa wazazi hiyo pesa ya sadaka. Au masikini unaemfahamu. Sijui timefungwa akili! Kila siku naangalia hapa Tanganyika perkers, watu wanavyomiminika na sadaka zao. "Ee baba wa Mbinguni tunasue na hili janga"
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hao hao wazazi wetu ukimpa hiyo sadaka anaweza kuipeleka kanisani.
Kuna siku bibi yangu aliniambia nifukuze jogoo ili ampe padri ambaye alikuja home kumsalimia. Wakati huo home hamna kitu.
Nikifikiriaga na ile hali aliyokuwaga nayo bibi na yule padri kumchukua yule jogoo ndio najua wakati mwingine hata mapadri ni njaa kali tu.
Tatizo liko hapoUkimpa mzazi anaipeleka mwenyewe huko kwenye nyumba za ibada.
Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Asante kwa ujumbe huuKama una laki moja yako usiipeleke msikitini/kanisani kwanza fikiria mama yako hana shida binafsi ambazo anaweza kutatua kwa pesa hiyo?
Baba je?
Ndugu wengine wa karibu?
Kuna watu wazazi wao wanahangaika kutafuta ugali wa siku mtu ile package ya kula wiki hana lakini mtu huyu anachukua pesa anapeleka kwenye nyumba ya ibada.
Mungu anakuona aisee, hautaadhibiwa na Mungu kwa nini pesa yako ulimpa mzazi akatatue shida zake wakati nyumba ya ibada haijapigwa rangi n.k
Lakini Mungu anaweza kukutia adabu kwa nini mzazi wako alilala njaa wakati wewe ulipeleka pesa kwingine.
Lengo la sadaka ni kuwasaidia wasiojiweza, sasa kama mzazi wako naye hajiwezi msapoti.
Kuna kitabu nilikichungulia kinasema toa walau 10% ya kipato chako ukatoe sadaka.
Niliamua tu sadaka yangu hiyo 10% nawapa wazazi. Sina maana ya kukosoa sadaka lakini nakumbusha tu wazee wetu wana dhiki nyingi, tusijifanye wema sana kwenye nyumba za ibada wakati wazee wetu hilo salio lingewasaidia.
Wema, sadaka huanzia nyumbani kwa watu wako wa karibu.
NB ; Kama wazazi wako wanajiweza hii mada haikugusi
Kwaiyo mitume wa kileo hawana urithi?Unataka walawi wakale wapi?mana maandiko walawi walipewa kazi ya kuhudumu kwenye hekalu...pia hawakupewa urithi kati ya makabila ya wana wa Israel.
Hivyo walawi watakula madhabahuni.
Halafu injili itawafikiaje wasio amini kama injili ikinuka umasikini ?..leteni fedha makanisani ili kuisukuma injili isonge mbele wengi waokolewe na wampokee kristo.
#MaendeleoHayanaChama
Quran imetofautisha sadaka zaka. Zaka ni lazima na ni moja ya nguzo ya uislam. Na unatakiwa kutoa kila unapopata mavuno au kipato. Quran 17:26 na 30:38 inaelekeza zaka zipelekwe kwa wazazi maskini, ndugu maskini, watoto yatima, wagonjwa wasiojiweza, ambao hawana makazi ya kuishi. Sadaka ni hiari. Quran 9:60 inaelekeza kutoa sadaka kwa hiari . Sadaka ziende kwa wanaozikusanya hapa namaanisha wanaohudumia miskiti, kuwakomboa watumwa waliomateka, masikini walio na madeni na wahitaji wengine.Afu kuna watu wanakuunga mkono kabisaaa kua uko sahihi?
Kama hawajawahi kusoma Bible na Qurani mtakua pamoja, ila najua mtoa mada ni mpagani, vinginevyo ni wivu tu unakusumbua.
Dini zipi,siyo dini zote zinapenda pesa aka Sadaka na Zaka broo,Dini zingine zipo Smart sana kwenye kustawisha hali za mwanadamuDini zinafukarisha watu zaidi kuliko kuwasaidia.
Kama mtu una pesa zako sio tatzo,ila tatizo ni kuwa mtu anajibana kumpa mzazi eti kisa kingine akatoe kanisani wakati huo anachompa mzazi hakitoshi.Kuna baraka za kumpa pesa mzazi na kutoa sadaka kanisani..
Malaki 3:10
Leteni zaka kamili nyumbani mwa Bwana...