SADC ina faida gani kwa nchi yetu?

Kwa kweli kabisa Jumuia ya kikanda inayotufaa sisi ni EAC, hii ya SADC ni mwendelezo tu wa vugu vugu la ukombozi wa nchi za kiafrika ambapo manufaa tunayoyapata huko ni kidogo mno.

..DRC, Zambia, Malawi, na Msumbiji, ni majirani zetu walioko ktk jumuiya ya SADC.

..Naamini tukijipanga tunaweza kufaidika kwa fursa zinazopatikana ktk nchi hizo.
 
Habari wakuu.

Naomba kujuzwa faida za SADC kwa nchi yetu.

Tuacheni uvivu wa kufikiria . Soma kwanza ndiyo uje na maswali tuache kupenda drama kwenye kila kitu. Kama hujui kusoma tumia muda huu jifunze

 
..DRC, Zambia, Malawi, na Msumbiji, ni majirani zetu walioko ktk jumuiya ya SADC.

..Naamini tukijipanga tunaweza kufaidika kwa fursa zinazopatikana ktk nchi hizo.
Hizo nchi zote ulizo orodhesha tunapakana nazo hivyo tunanufaika nazo hata bila kuwa SADC, aidha muda si mrefu DRC itakuwa mwanachama la EAC.
 
Just another Alphabetized organization where African leaders advance globalist c**k sucking by borrowing money for projects that you the "commoner " will pay dutifully in taxes.. it is more advantageous for African countries to work bilaterally rather than under a big umbrella name.


It is a Grift
 
Hizo nchi zote ulizo orodhesha tunapakana nazo hivyo tunanufaika nazo hata bila kuwa SADC, aidha muda si mrefu DRC itakuwa mwanachama la EAC.

..kama hatuwezi kunufaika na DRC ikiwa mwanachama wa SADC, unaamini tutafaidika na DRC ikiwa mwanachama wa EAC?

..nadhani SADC haina matatizo kwasababu kuna nchi zinafaidika na jumuiya hiyo, tatizo liko kwetu sisi Watanzania.

..Na kuna watu hapa JF naamini ni watu werevu tu, wanaipenda jumuiya ya SADC kuliko EAC. Wanaamini ktk EAC Wakenya wanatunyonya.
 
tatizo liko kwetu sisi Watanzania.
Bila hata kuwa na Jumuia mbili za kikanda Mashariki ya DRC yote inahudumiwa na Tanzania kwa njia zisizo rasmi na hii ni kwa miaka mingi sana. Udhaifu wetu katika kutumia fursa zilizopo ikiwemo eneo la nchi yetu kimkakati ndio kikwazo kwetu kitaifa, ingawa wananchi mmoja mmoja kwa pande zote mbili wananufaika.
 
we kuna faida za SADC umeziona?
 
kuisoma SADC na faida zake haimaanishi kuwa ina faida. wewe kuna faida za SADC umeziona?
 
Kutumia lugha ya kiswahili katika majukumu yake.
Asante kwa swali.
Jf tumekosa adabu
Mtu anauliza swali haijalishi ni jepesi au gumu badala ya kumjibu wanamshambulia tena kwa kejeli!
Tujifunze kuishi na kila kiumbe cha muumba
 
Kutumia lugha ya kiswahili katika majukumu yake.
Asante kwa swali.
Jf tumekosa adabu
Mtu anauliza swali haijalishi ni jepesi au gumu badala ya kumjibu wanamshambulia tena kwa kejeli!
Tujifunze kuishi na kila kiumbe cha muumba
Tabia hiyo inatokana na mfumo wa elimu tulionao. Waalimu waliomfundisha walitumia kiboko na adhabu hata ukikosa moja kati ya kumi. Ndio maana badala ya kuelimisha mtu, anaanza na tusi au kumalizia nalo....

Tutegemee nini kwa mwalimu anayefundisha na fimbo pembeni wakati mwanafunzi nae pamoja na madaftari na kalamu, ana dumu,fagio jembe na reki ?
 
Hawa ndio wale darasani wanjiona bora hawataki wengine waulize swali
 
Ugali una ubaya gani? Kwenu mnakula Nini Hadi useme NO to ugali?
Haiwezekani jamii nzima ya wala Ugali ikashindwa kugundua hata Sindano,haiwezekani jamii nzima ya wala Ugali ikawa na Zero IQ

Ni nani aliyetuletea Ugali huku Afrika? huyo ndio katumaliza.
 
Kwani magroup ya wasapu tunayojiunga yana faida gani???labda tuanzie hapo
 
Ukiimport gari ambalo kwa sehemu kubwa limetengenezwa SA unapata Msamaha wa tozo?
 
Nadhani kwa mimi (mtu mmoja mmoja) kusafiri visa free kwa nchi nyingi
Kwa wana biashara nk watujuze
 
Kijiwe cha kupiga soga na 'kuchoma moto' pesa za walalahoi.
 
Faida yake kubwa ni kwa Wakulima na wafanya biashara mfano vitunguu vikiwa havina soko Bongo basi vitauzwa kwenye nchi za SADC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…