Saddam Hussein alikuwa ni Dikteta mwenye faida kwa nchi yake

Kuna tatizo gani kudharau mamlaka au kuleta ujuaji mbele ya Rais wa nchi??
Swali zuri , Rais wa nchi ni kama mfalme maamuzi yake yanatakiwa yaheshimiwe hata kuyahoji yahojiwe kwa busara na heshima sio kumbwatukia hovyo hovyo kama anafanya mambo tofauti aambiwe kwa hoja sio matusi
 
Asante sana kwa kuliona hili. Kisehemu nilichoweka kwenye nyekundu umekiandika wewe na ndiyo maana halisi ya demokrasia. Yaani wananchi wakubaliane na mfumo. Kwa kifupi demokrasia siyo lazima iwe ya vyama vingi au kuwe uchaguzi kwa kutumia njia za maboksi ya kura. Na ndipo hili bandiko lilipokosea. i.e. kusema kuna nchi zinahitaji kuendeshwa kwa udikteta. Ukishesema tu udikteta ina maana matakwa ya wananchi yamepuuzwa. Kwa kifupi zipo namna nyingi za demokrasia na wananchi ndiyo waamuzi.
Misingi mikuu ya demokrasia ni
1. Chaguzi huru na za haki hata na kama hakuna vyama vingi au hakuna vyama kabisa.
2. Mihimili huru ya dola na taasisi zililizo huru kama za Polisi.
3. Uhuru wa vyombo vya habari
4. Due process
5. Individual liberties
 
Swali zuri , Rais wa nchi ni kama mfalme maamuzi yake yanatakiwa yaheshimiwe hata kuyahoji yahojiwe kwa busara na heshima sio kumbwatukia hovyo hovyo kama anafanya mambo tofauti aambiwe kwa hoja sio matusi
Rais wa nchi sio kama mfalme (katika nchi za kidemokrasia na hata zisizo za kidemokrasia),
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Jamuhuri na Ufalme (absolute monarchy). Nyerere ndio alitengeneza na kutuaminisha mfumo wa Urais wa Kifalme Tanzania ambao kwa kiasi kikubwa sana umeharibu nchi na kutudumaza kimaendeleo na kisiasa.
 
WAkati wa utawala wq Sadam Hussein hakukuwa na makundi ya kiislam yenye msimamo mkali, wakiristo pamoja na kuwa wachache waliabudu bila kubaguliwa na alikuwa na waziri mkiristo aliyekuwa waziri wa mambo yq nje.
Uchumi wao ulikuwa imara, mapungufu yalikuwepo ila kulinganisha na sasa ni afadhali ya utawala wake.
Huyu wa Malawi ameanza kutenganisha wamalawi kwa kutumia dini, undugu na mbaya zaidi anatumia rasilimali za Tanganyika kujinufaisha yeye binafsi, familia yake na watu wake wa karibu wanaomzungukq, maosha yamekuwa jui sana.
 
Kwa historia ya nchi yetu, hulka za viongozi wetu na wananchi.

Mfumo wa kuongozwa na kila kitu kuwa chini ya Mtu mmoja au Kikundi cha watu wachache haufai, mara mia Demokrasia.
 
Waarabu Waislamu hawako compatible na demokrasia, kwa kiasi kikubwa ni vigumu demokrasia kufanya kazi katika nchi za Waislamu watupu kwa sababu kuna mambo mengi demokrasia inapingana na Uislamu. Hata mfumo wa utawala kama wa China ni vigumu kufanya kazi kwenye nchi za Waislamu wengi kwa sababu uko ki secular zaidi.

Pakistan sio nchi ya kidemokrasia, ni kama Tanzania tu. Jeshi ndilo linaamua uongozi uweje.

Ni ukweli yapo mazingira yanayofanya demokrasia kuwa ngumu kufanya kazi ikiwemo nchi kuwa na raia wengi wafia dini na population kubwa kupitiliza kama ilivyo India.

Zaidi binadamu wengi (has wasio wahafidhina wafia dini) wanapenda maendeleo yaliyo pamoja uhuru mkubwa kwa raia binafsi (individual liberties), inapotekea wanapata kimojawapo ni afadhali lakini sio ideal.
Unaongelea Pakistan ya juzi hapa Jeshi kuchukua Nchi ila kabla ya hapo ilikua ni nchi ya Kati, ambayo kwa Nchi zetu hizi ilikua ikisifiwa, so is India.

Na Tunisia inasifika kwa Nchi za Kiarabu kuwa liberal country so excuse ya dini haiaplly huko, Ila still ina struggle. Ukiangalia matatizo Yao sasa hivi ni exactly matatizo wanayopata Nchi za Ki Africa zinazojinasibisha na Democracy kama Kenya na South Africa, security imekuwa ndogo, ukosefu wa Ajira unaongezeka, umasikini unaongezeka, matajiri wanaongezeka etc coincidence? Algeria sasa hivi percentage ya wananchi wenye kipato chini ya Dola 15 ni 1, Tunisia percentage ya wananchi wenye kipato chini ya Dola 5 ni zaidi ya 15.

Sometimes Sisi binadamu tunapenda vitu na kuwa huru, Ila inabidi vitu vingine tufanye hata kwa kulazimishwa ili kupata maendeleo, Nchi nyingi zinazopigia chapuo democracy na ubepari Pato Lao linatokana na kunyonya Nchi nyengine na sio mifumo ya Nchi zao ndani ni Bora.
 
Nipe mfano wa Nchi ya Middle East yenye Demokrasia na Maendeleo,

Mfano Mzuri Angalia hapo North Africa, Tunisia wanakua regarded kama Nchi yenye Demokrasia zaidi Middle East na North Africa, ila maendeo Yao still hayafikii the likes of Algeria na Morocco, watu wale wale, geography Ile Ile, resource zile zile.

Same kwa Asia kuna kanda kibao the so called democratic countries ni upuuzi mtupu, Pakistan huwezi ifananisha na Iran, India Huwezi fananisha na China etc.

Cha muhimu Nchi iwe na mfumo unaokubalika na wananchi na Serikali iwatumikie wananchi, hakuna mfumo mmoja unaoweza leta maendeleo Dunia nzima.
Nakubaliana nawewe chamsingi mfumo ukubalike na raia na matokeo yaonekane hakuna shida,
 
Unaongelea Pakistan ya juzi hapa Jeshi kuchukua Nchi ila kabla ya hapo ilikua ni nchi ya Kati, ambayo kwa Nchi zetu hizi ilikua ikisifiwa, so is India.

Na Tunisia inasifika kwa Nchi za Kiarabu kuwa liberal country so excuse ya dini haiaplly huko, Ila still ina struggle. Ukiangalia matatizo Yao sasa hivi ni exactly matatizo wanayopata Nchi za Ki Africa zinazojinasibisha na Democracy kama Kenya na South Africa, security imekuwa ndogo, ukosefu wa Ajira unaongezeka, umasikini unaongezeka, matajiri wanaongezeka etc coincidence? Algeria sasa hivi percentage ya wananchi wenye kipato chini ya Dola 15 ni 1, Tunisia percentage ya wananchi wenye kipato chini ya Dola 5 ni zaidi ya 15.

Sometimes Sisi binadamu tunapenda vitu na kuwa huru, Ila inabidi vitu vingine tufanye hata kwa kulazimishwa ili kupata maendeleo, Nchi nyingi zinazopigia chapuo democracy na ubepari Pato Lao linatokana na kunyonya Nchi nyengine na sio mifumo ya Nchi zao ndani ni Bora.
Anti-democrats huwa mna uelewa finyu, hoja dhaifu sana na historia potoshi kuhusu demokrasia. Pakistan haijawahi kuwa nchi ya kidemokrasia au yenye utulivu wa kisiasa tangu kuuundwa kwake, muda wote imekuwa ikikabiliwa na mapinduzi ya kisiasa na utawala jeshi kuingilia siasa.

Demokrasia ya Kenya haizidi hata miaka 20 tena katika Taifa ambalo liliachwa na athari kubwa za ukabila, Africa Kusini utawala wa demokrasia wa watu weusi ni miongo mitatu baada ya utawala wa Apartheid wa ubaguzi wa Kizungu wa zaidi ya nusu Karne tena wakiwapa uhuru weusi huku bado wazungu wanahodhi sehemu kubwa ya uchumi ulitegemea nini kifuate.
 
Hoja imekaa kisomi
 
Kwa historia ya nchi yetu, hulka za viongozi wetu na wananchi.

Mfumo wa kuongozwa na kila kitu kuwa chini ya Mtu mmoja au Kikundi cha watu wachache haufai, mara mia Demokrasia.
Madhara ya kuiminya demokrasia kwenye nchi yeyote Dunia ni pale atokee kiongozi asiyefaa , faida ya kuiminya demokrasia ni pale kiongozi wa juu akiwa full package
 
Nilikutana na makala moja mtandaoni iliyokuwa inazungumzia utawala wa Sadam hussein , makala hiyo imenikumbusha mambo mengi ya Sadam hussein aliyekuwa kiongozi wa Iraq

Jamaa kitu kikubwa kilichomfanya awe adui wa Marekani ni kwasababu alikosa utii na unyenyekevu kwa Marekani , marekani wakamfanya adui yao wakamfanyia figisu na mizengwe ya kila aina mpk wakafanikiwa kuuangusha utawala wake ila jamaa alikuwa mwamba kweli kweli mpk alivyofikishwa mahakamani alibaki na msimamo wake ule ule

Iraq iliyokuja baada ya utawala wa Sadam hussein haitawaliki tena nchi imeoza haifai ndio kama kilicho tokea Libya kwa Gadafi

Kuna nchi zinahitaji viongozi ma dikteta wenye faida ili ziende

Sadam Hussein niliona kwenye makala alikuwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano hakuna mtu aliyekuwa anathubutu kukohoa au hata kupiga chafya , alikuwa akiku point utoke nje ya ukumbi ujue umekwisha
Kila dikteta ana mazuri yake na mabaya...uwiano ukoje?
 
Anti-democrats huwa mna uelewa finyu, hoja dhaifu sana na historia potoshi kuhusu demokrasia. Pakistan haijawahi kuwa nchi ya kidemokrasia au yenye utulivu wa kisiasa tangu kuuundwa kwake, muda wote imekuwa ikikabiliwa na mapinduzi ya kisiasa na utawala jeshi kuingilia siasa.

Demokrasia ya Kenya haizidi hata miaka 20 tena katika Taifa ambalo liliachwa na athari kubwa za ukabila, Africa Kusini utawala wa demokrasia wa watu weusi ni miongo mitatu baada ya utawala wa Apartheid wa ubaguzi wa Kizungu wa zaidi ya nusu Karne tena wakiwapa uhuru weusi huku bado wazungu wanahodhi sehemu kubwa ya uchumi ulitegemea nini kifuate.
Unaongea miaka 20 as if ni siku 5 Tu, Nchi yoyote serious miaka 20 tayari unaona muelekeo.

Nitajie wewe Africa hii ama Nchi zetu hizi ambayo inafuata Demokrasia huku haina umasikini wa kutupwa, iwe na population ya kutosha.
 
Nilikutana na makala moja mtandaoni iliyokuwa inazungumzia utawala wa Sadam hussein , makala hiyo imenikumbusha mambo mengi ya Sadam hussein aliyekuwa kiongozi wa Iraq

Jamaa kitu kikubwa kilichomfanya awe adui wa Marekani ni kwasababu alikosa utii na unyenyekevu kwa Marekani , marekani wakamfanya adui yao wakamfanyia figisu na mizengwe ya kila aina mpk wakafanikiwa kuuangusha utawala wake ila jamaa alikuwa mwamba kweli kweli mpk alivyofikishwa mahakamani alibaki na msimamo wake ule ule

Iraq iliyokuja baada ya utawala wa Sadam hussein haitawaliki tena nchi imeoza haifai ndio kama kilicho tokea Libya kwa Gadafi

Kuna nchi zinahitaji viongozi ma dikteta wenye faida ili ziende

Sadam Hussein niliona kwenye makala alikuwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano hakuna mtu aliyekuwa anathubutu kukohoa au hata kupiga chafya , alikuwa akiku point utoke nje ya ukumbi ujue umekwisha
Aliwai kumuadabisha mtoto ake mmoja kati ya UDAY AMA QUSAY..

Watoto wake walikua very notorious huwezi amini

Ila jamaa alikuaga very humble na alikua ni mwenye UTU SANA SANAAAAAA
 
Unaongea miaka 20 as if ni siku 5 Tu, Nchi yoyote serious miaka 20 tayari unaona muelekeo.

Nitajie wewe Africa hii ama Nchi zetu hizi ambayo inafuata Demokrasia huku haina umasikini wa kutupwa, iwe na population ya kutosha.
Huelewei unachosema, hata hizo nchi za middle east hazina population kubwa huku zikiwa na ukwasi wa mafuta na gesi, watawala wa Gulf states (GCC) wanachota pesa wanavyotaka wanaweka kwenye akaunti zao binafsi na bado zinabaki pesa nyingi sana za kufanya maendeleo na kuwafanya raia wasilipe kodi. Kenya haina utajiri wowote mkubwa wa rasilimali, kiongozi akiiba hata kidogo tu lazima pengo lionekane.
 
Nikipima kwenye mzani naona alikuwa na nia njema na Taifa lake ila Agenda zake hazikukubalika kimataifa
'Mama awalisha watoto sumu na yeye kajinyonga,' Inawezekana lengo la huyo mama ni zuri kabisa, hataki watoto wake wabak kwenye dunia yenye mateso...ila bado ni sahihi? Kuwa dikteta ni kujaribu ku dictate maisha ya watu kama huyo mama alivyowachagulia kifo watoto wake kwa lengo ambalo anaona ni zuri
 
Unaongea miaka 20 as if ni siku 5 Tu, Nchi yoyote serious miaka 20 tayari unaona muelekeo.

Nitajie wewe Africa hii ama Nchi zetu hizi ambayo inafuata Demokrasia huku haina umasikini wa kutupwa, iwe na population ya kutosha.
Africa nchi za demokrasia halisi ni chache sana. Ni Botswana, South Africa, Namibia, Mauritius, Ghana, Kenya, Cape Verde na Senegal.
 
Sadam Hussein niliona kwenye makala alikuwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano hakuna mtu aliyekuwa anathubutu kukohoa au hata kupiga chafya , alikuwa akiku point utoke nje ya ukumbi ujue umekwisha
Hii haipaswi kuwa hivi, hata kama utaleta maendeleo mara milioni lakini haipaswi kuminya wengine na kunyima fursa za watu kuwa huru kutoa maoni au kukukosoa unapokosea, kumbuka hakuna binadamu aliye mkamilifu, hakuna aliye na hati miliki ya nchi
 
Back
Top Bottom