Chama cha ACT-Wazalendo kinapenda kuutaarifu umma wa Watanzania na wananchi wa Kinondoni kwamba, Mgombea wetu wa Ubunge Jimbo la Kinondoni, Ndugu Saed Ahmed Kubenea amepata dhamana ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Septemba 11, 2020 baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria katika kesi inayomkabili.
ACT-Wazalendo tunawapongeza kwa dhati kabisa mawakili waliofanikisha hatua hiyo ya mgombea wetu kupata dhamana wakiongozwa na Sheki Mfinanga na Allute Mughway.
Pia tunawashukuru wanachama, wapenzi na mashabiki wa ACT- Wazalendo kwa kututia moyo kwa njia mbalimbali ikiwamo ya maombi na sala na hatimaye mgombea wetu kupata dhamana.
Baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, tunawasihi wanachama, wapenzi na wapiga kura wetu wa Jimbo la Kinondoni kufuatilia ratiba ya mikutano ya kampeni ya Ndugu Saed Ahmed Kubenea ili wakasikilize sera na ahadi zilizomo kwenye Ilani ya ACT-Wazalendo kwa jimbo hilo na Taifa kwa ujumla.
Aidha Ndugu Saed Ahmed Kubenea anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari katika siku za karibuni juu ya suala hili.
Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
Naibu/Katibu Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma
Leo Septemba 11, 2020