Saed Kubenea aachiwa kwa dhamana

Saed Kubenea aachiwa kwa dhamana

Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo na ameachiwa kwa dhamana

Kubenea alikamatwa Septemba 07, 2020 na kutuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo utakatishaji fedha, kukiuka Sheria za kuvuka mpaka kwenda Kenya na kurejea nchini kwa kutumia njia zisizo rasmi

Baada ya kukamatwa alifikishwa Mahakamani na kisha kurudishwa rumande kutokana na makosa ya utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana




Pia, Soma: Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Hee, nafurahi wamemwachia lkn Kumbe Kosa la Utakatishaji pesa lina dhamani sasa? Vp akina Tito Magoti
 
Chama cha ACT-Wazalendo kinapenda kuutaarifu umma wa Watanzania na wananchi wa Kinondoni kwamba, Mgombea wetu wa Ubunge Jimbo la Kinondoni, Ndugu Saed Ahmed Kubenea amepata dhamana ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Septemba 11, 2020 baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria katika kesi inayomkabili.

ACT-Wazalendo tunawapongeza kwa dhati kabisa mawakili waliofanikisha hatua hiyo ya mgombea wetu kupata dhamana wakiongozwa na Sheki Mfinanga na Allute Mughway.

Pia tunawashukuru wanachama, wapenzi na mashabiki wa ACT- Wazalendo kwa kututia moyo kwa njia mbalimbali ikiwamo ya maombi na sala na hatimaye mgombea wetu kupata dhamana.

Baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, tunawasihi wanachama, wapenzi na wapiga kura wetu wa Jimbo la Kinondoni kufuatilia ratiba ya mikutano ya kampeni ya Ndugu Saed Ahmed Kubenea ili wakasikilize sera na ahadi zilizomo kwenye Ilani ya ACT-Wazalendo kwa jimbo hilo na Taifa kwa ujumla.

Aidha Ndugu Saed Ahmed Kubenea anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari katika siku za karibuni juu ya suala hili.

Imetolewa na:

Janeth Joel Rithe

Naibu/Katibu Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma

Leo Septemba 11, 2020
 
'Kazi na Bata' hii kauli mbiu Hata Kiongozi mkuu wa Chama cha ACT anaitumia?
 
Back
Top Bottom