Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sehemu ya 5
Maisha yangu yalikuwa ni pale makambako kwa bibie chaula yaani ni pika pakua. Na kiujumla baada ya kuwa na yule mwanamke niseme tu mambo yalianza kuwa mazuri sana na yalininyookea haswa! Kuna wanawake ukiwa nao kwenye maisha ni kama bahati tena ile nzuri na kuna wengine ni mikosi tupu. Kwahuyu bibie chaula yeye alikuja na bahati sana kwangu. Ni mweusi kidogo, urefu wake kama nchi 5' na ana hips na kalio la kuzugia.
Hela zilikuwa zinanitembelea sana na mishe mishe zilianza kuwa nyingi kwa upande wangu. Nilifungua duka la vitu muhimu hivi vya majumbani mitaa ya lyamkena. Kwahyo mara moja moja nlikuwa nauza mimi ila muda mwingi alikuwa anauza yeye mwenyewe bibie chaula. Mimi nlikuwa naendelea na mishe mishe huko mtaani nikipata hela naongeza mtaji hapo dukani.
Majira ya masika ndio huyu bibie alijifungua mtoto wa kiume, kwangu mimi alikuwa ndio wa kwanza ila kwa upande wake yeye alikuwa wa pili. Hivyo familia iliongezeka na kuwa ya watoto wawili. Kwangu haikuwa shida maana hela ilikuwa hainipigi chenga. Kutokana na makambako kuwa highway magari yanapita mengi, huwa vitu vilikuwa vikiibiwa kwenye magari mara nyingi mimi ndio nlikuwa mnunuzi mkubwa, kwasababu jirani yetu kabisa kulikuwa na kilabu cha pombe hivyo vitu vya mishe vilikuwa vikipita mara kwa mara.
Nilianza kuwa mzoefu na sasa kazi yangu kubwa ilikuwa ni kununua vitu vya mishe na mtaji ulikuwa. Mpaka usiku mmoja naamshwa naambiwa oyaa! Mark. Kuna mzigo hapa wa maana, nilitoka nje nikiwa na lenge la usingizi. Nikaonyeshwa kopa ila nlikuwa sina uzoefu na kopa hivyo sikuwa nashawishika kununua haswa kulingana na bei pia niliona kubwa. Nikawaambia rudini asubuhi saivi sina hela. Asubuhi kulivokucha nikaununua ule mzigo wa kopa. Nilikaa nao mpaka nyakati nimeenda dar ndio niliuza huko ambako nlipata faida ila sio sana. Kule dar nilijifunza mambo mengi sana na ushauri wa kibiashara uliokuwa unataka moyo na ujasiri.
Niliporudi makambako niliamua sasa na mimi nitafte vijana wa kazi. Mpango wangu ulikuwa ni wakuteka mali kwenye malori makubwa, kama mahindi, petroli, kopa n.k. Wazo langu likawa niongea na Sanga kama atanikubalia tushirikiane pale Godown yake kuweka mizigo. Nilimfata na kweli akanikubalia na kunitajia gharama zake ntazokuwa nampa. Yeye hakujua kama zitakuwa ni mali za uwizi. Alichojua yeye ni kuwa saivi hela imenitembelea sishikiki. Ndani ya mwezi niliweza kupokea mizigo mingi haswa mahindi na maharage. Mafuta kwa uchache na vinginevyo. Na kutokana na uwizi kuwa ulishamiri kwenye highway na makachero walikuwa patrol mara kwa mara. Ila hawakuthubutu kunigusa maana nlikuwa nawashika mkono kidogo. Sikuwa na mkono wa birika.
Muda ulizidi kusonga na mimi kushamiri zaidi, ambapo sasa niliona kuna haja ya kutanua mbawa zangu na kuanza kuingia kwenye biashara ya mbao. Hilo halikuwa gumu haswa ukiwa na watu na mtaji yaani hela. Nilianza biashara ya mbao, haswa magogo ambayo nilikuwa nikiyaleta karakana na kuyachana. Kuna hela nilimkopesha mzee mmoja wa kibena akiwa anaumwa, na kumuandikisha sawmill yake na vimashine vingine vidogo. Yule mzee alipokuwa anakaribia kuvuta moto mimi nilifoji mkataba wa awali na kuwa sio mkopeshano tena bali ameniuzia mazima. Kwahyo hata watoto wa yule mzee baada ya msiba kuja kudai haki yao na umiliki wa sawmill na mashine nyingine mi niligoma na kutoa mkataba unaonyesha niliuziwa na baba yao. Nilitumia na nguvu ya ziada kidogo kuwatisha na kuichukua ile mali kimabavu. Hapo watu walianza sasa kuniogopa na kuona mimi ni katili.
Je! Nini kitafuata usikose sehemu ya 6
Itafika mpaka mwisho dr namugariUmalizagi story
subiri mwaka uishePoker muendelezo niaje??
😄😄 Nimeishajiandaa kiakilisubiri mwaka uishe
Ukiweka naomba nitagLeo jioni inshallah.
alhamdulillahLeo jioni inshallah.