Safari fupi ya kuzimu. Sijutii maisha yangu

Safari fupi ya kuzimu. Sijutii maisha yangu

Sehemu ya 7
Maisha yalizidi kusonga kama kawaida, namimi kiujumla nilizidi kushamiri kwenye biashara. Kadiri siku zinavyoenda na ushindani unaongezeka, hivyo kuna msukuma aliingia mjini kwa fujo sana akifahamika kwa jina la King. Yeye alikuwa muuzaji wa mbao za mninga na vifaa vya hardware. Aliongeza ubunifu kwa kuanza kuchukua tenda za kujengea watu majumba kwakuwa alikuwa na mtaji mkubwa. Hii haikukaa sawa kwangu na ilitishia mustakabali wa biashara yangu. Kwakuwa tayari nilishakuwa na umaarufu flani pale town na connection, niliazimia kumtoa kwenye reli ya biashara. Hizi biashara mara nyingi lazima ujisindike haswa na mimi nilijisindika kweli kweli.

Ila huyu bwana King alikuwa wa moto maana kila nikijaribu kwenye njia za giza nikama nagonga mwamba. Hivyo nikaamua kumuuzia ya tenda ya kujenga gorofa huko kinondoni kwa madai mimi kwa sasa siko vizuri kimtaji. Nakwakua aliona inalipa na pesa niliyomtajia ni kubwa akakubali kwa mapatano ya asilimia 25 kila hatua ya jengo hilo. Alipambana na ilipofika asilimia 25 nilimpa hela akaendelea ila kila anapofika asilimia ya kulipwa mimi nakuwa naumwa hoi nakusafirishwa mpaka nje ya nchi. Mchezo ukawa huo mpaka gorofa lilipokamilika kwa asilimia 90 ndipo mzozo ukaanza wa ardhi, baada ya mtu kujitokeza na kudai eneo nilake. Na mimi kwakujua kinachoendelea niliamua kukomaa ili kesi iende mbele yaani mahakamani. Bwana King naye alikuwa akidai sana hela yake ndipo nilipoamua kumuita aje makambako tumalizane nusu ya hela anayodai.

Kweli alifika na mimi mpango ulikuwa ni mmoja tu, yaani kumuangamiza kabisa maana nilikuwa najua nipo uwanjanwa nyumbani. Niliandaa vijana na kusuka mpango kamili ili atakapofika kazi ifanyike bila dosari. Alipofika alifikia gesti hapo makambako ambayo niliijenga mimi mwenyewe naye alikuwa na vijana wake wawili ambapo huyo mmoja nimwanae wa kumzaa. Tulipoonana nilimpatia hundi ya pesa na mazumgumzo mengi na ahadi za kutosha. Wakati wa kutoka kuelekea eneo la gesti ilipo walipata ajali ya kugongana na isuzu lori ilikuwa mida ya saa moja usiku na wao walikuwa na gari aina ya nissan patrol. Hawakuumia sana ila wakati wakitaka kutoka kwenye gari ndipo Vijana wangu walichangamka na kuwakata na mapanga, maana hatukupenda milionya risasi isije ikaamsha hisia tofauti. Nakisha kwa kuchoma moto yale magari haraka na kuondoka eneo la tukio. Huwa wafanya tukio wakishaondoka kuna timu nyingine huwa inakuja kama mashuhuda wa ajali nakuanza kutoa stori za uwongo alimradi kuuficha ukweli.

Baada ya hapo inaingia timu ya tatu ambao ni wana usalama na kazi yao ni kuhakikisha ushahidi wowote ulioachwa nyuma wanaupoteza na timu ya 4 na ya mwisho ni vyombo vya habari haswa redio na magazeti ambapo huwa nina watu wangu kuhakikisha wanaandika story kwa jinsi navyotaka mimi haswa linalohusu biashara yangu au mimi mwenyewe. Mr King shughuli yake iliishia pale pale na vijana wake, hivyo nikarudi dar kwenda kuhamishia majeshi na kumgeuzia kibano mke wake kuwa nilimkopesha kujenga hilo gorofa nakwamba sijalipwa. Kwakuwa biashara nyingi zilikuwa ni za siri siri na mhusika kwasasa ni marehemu na watoto waliobaki wengine ni wadogo mimi niliongeza nguvu na vitisho kwa mjane huyo.

Baada ya familia ya marehemu king kuona nimewazidi nguvu na vita vyangu vimekuwa vya moto waliamua kuniachia hati miliki ya kiwanja huko tabata kinyerezi na nyumba ambayo alikuwa akiishi huko segerea. Hawakuchukua muda nao waliamua kuhama dar na kurudi mwanza. Mimi nilibaki mjini na niliendelea na biashara zangu huku nikijitanua zaidi na kuvuta watu wengi karibu yangu. Ijapokuwa minong'ono ya hapa na pale haikosekani na wengi walikuwa wakiniona kama gaidi maana nilikuwa sina utani au masikhara kwenye biashara zangu. Kwa upande wangu mimi nilikuwa nataka kuingiza tuu, nasio kutoa. Hivyo wengi waliniona mtata hata wafanyakazi walikuwa hawadumu kutokana na ukali na ukorofi wangu.
Ila ndivyo biashara ilivokuwa inataka, kutokuendekeza ujinga wa aina yoyote.
Je? Nini kitafata usikose sehemu ya 8
 
Sehemu ya 8
Kutokana na kuanza kuwa na watu kila sekta nchini, haswa ukiwa na hela utashauriwa vingi sana. Hivyo niliamua kuingia kwenye biashara ya madini huko mahenge, kahama na mererani ambapo nilinunua migodi na pia kuanza kazi ya kuwa broker kwa wachimbaji wadogo wadogo. Hii kazi ilikuwa na ugumu na unafuj wake kwenye ugumu wake ulikuwa unaeza kuhudumia shimo hata miaka miwili na bado usiambulie kitu. Mfano mererani nilihudumia shimo miaka 4 bila kuambulia kitu. Kwenye unafuj wake ni kununua madini hayo kwa wachimbaji wadogo wadogo ambapo nilikuwa nikiwadhulumu kwa kuwapa bei ndogo isiyo endana. Hivyo ukipata faida unaizungusha tena huko huko kwa kuhudumia mashimo hayo.

Ni biashara za kuviziana sana na ukizubaa umeliwa. Unatakiwa uwe makini na kamili kila sekunde. Mimi kama kawaida nilikuwa lazima niwe na watu nyuma yangu ambao hao kazi yao ni kutafuta wadada warembo wakuwahadaa wachimbaji pindi wamepata mali na wengine walikuwa wakichimba nao pamoja na wengine wakipeleka huduma kwenye mashimo kama maji au chakula.

Shimo lile la mahenge baada ya kuona linazidi kula hela na hakuna kinachoingia niliamua kuachana nalo na kujikita zaidi huko kahama na mererani. Lile la mererani lilikuja tema mwaka wa 5 wakulihudumia, ambapo lilileta faraja ndani ya nafsi. Mawe nlipata na yaliniletea ukwasi zaidi na nilizidi kusimama wima haswa. Baada ya kuwa limetema tulifanya dawa kidogo, mambo yetu haya ya giza kwa kuchinja mbuzi. Haikupita muda lilileta balaa na watu kupoteza maisha humo shimoni. Wengi walisema ni kafara n.k Ila baada ya miezi kama 4 tulipata mkondo mzuri wa madini ambapo kwa asilimia kubwa wafanyakazi wapale shimoni walitoboa kimaisha.

Nilikuja kuamua kuliuza lile shimo baada ya kuugua sana na hivyo nikaona itakuwa nikuwafaidisha wengine. Hapo kwenye kuumwa nikwamba nilikutana na mtu mzito kidogo na alinitingisha sana ila mke wangu bi chaula alinihangaikia mpaka nikakaa sawa tena.

Kuna nyakati nakumbuka niliwahi kuvamiwa usiku na majambazi pale nyumbani kwangu kazamoyo mererani. Walifanikiwa kuniibia pesa taslimu milioni 30 na madini yenye thamani ya milioni 40 mpaka 50. Hili jambo liliniuma sana na niliapa kulipiza kisasi na kumjua mhusika wa hilo tukio. Baada ya ufatiliaji wa kina na wasiri sana nilikuja kumbaini tajiri mmoja ambaye alikuwa nyuma ya huo mpango. Ila niliamua kumuacha kwa ile imani kiporo hakichachi. Nayeye ndio sababu kubwa ya mimi kuachana na ile biashara ya madini. Aliniandama sana kwa kila hila na shari. Kule kahama niliendelea ila napo nilikuja kuacha baada ya kupinduka na gari na kuumia mguu wa kulia, hivyo mara nyingi nilikuwa nikitembea kwa kuchechemea au kama nadunda.

Niliamua kupumzisha akili na kufikiria biashara nyingine ya kufanya kwasababu kama hela ninayo yakutosha sana. Baada ya kushauriana na watu wangu wa karibu niliona wazo zuri ni mikopo ya kuwakopesha watu haswa wafanyabiashara. Nahii biashara niliipenda maana niliamini haina usumbufu na purukushani kama za madini.

Taratibu zote nilizifuata za kufungua kampuni yangu ya finance. Na ofisi tuliweka kariakoo dar, kirumba mwanza na mjini kati Arusha. Niliamua sasa kushirikiana na vijana wangu kwa ukaribu kwa kuhakikisha biashara hii ya mikopo inakuwa ya moto. Hivyo tuliizindika vya kutosha na pale ofisini ilikuwa kila mwaka lazima mfanyakazi avute kamba, inaweza kuwa ya ajali au kuumwa. Mishahara na marupurupu yalikuwa ni mengi hivyo ilinifanya nikatoa ajira rasmi na zisizo rasmi. Hivyo ofisi zote tatu kulikuw na pilikapilika nyingi sana. Inapotekea mfanyakazi kavuta basi huwa ofisi inagharamia mazishi yote. Hii ilikuwa ni lazima nifanye hivyo kwasababu lile gari ambalo lilikuwa linabebea maiti, likashamaliza shughuli zote linafagiliwa na ule mchanga wote unakusanywa na kuwekwa kwenye vyungu vya maua hapo ofisini. Hivyo kadiri yale maua yanavyomea ndivyo biashara navyo inazidi kumea zaidi.

Na mara nyingi ikifika mwisho wa mwaka basi huwa naandaa karamu ya kuchinja hapo ofisini, ilimradi damu imwagike hapo ofisini. Watu watakula na kunywa mpaka wasaze na mwisho yale maji ambayo watu huwa wananawia mikono kuna dawa inawekewa alafu yanamwagwa getini au langoni pakuingilia, hiyo huwa nikwaajili ya mvuto wa biashara na wateja kuongezeka zaidi.

Je? Nini kitafata usikose sehemu ya 9
 
Duh
 
Oya
Dah niliupoteza huu uzi
N
Nasubiri mwendelezo
 
Sehemu ya pili.
Mtaani hali ilianza kuwa ngumu kidogo hivyo nikaona nibadili upepo wa maisha na kuanza kuingia kwenye shughuli ya uchanaji wa mbao. Ilikuwa na unafuu kidogo japo ilikuwa risky, kutokana na kuingia mpaka maeneo ya hifadhi kutafuta miti ya kenfa ambayo ndio ilikuwa na hela zaidi.

Siku moja tukiwa pori tunachana, ikasemekana tajiri anakuja kununua miti zaidi na kutulipa hela zetu. Basi tukamsubiri sahiyo tushakaa kama wiki 3 bila bila. Kweli alikuja akapakia mbao zake na akanunua miti mingine. Kumhoji pesa zetu akasema ngoja arudi aende akatuongezee unga na dagaa wa hapo camp. Hiyo ikawa imekula na gia yake ya kuondokea.

Pale pori tukatoboa wiki 3 nyingine, tunaishi kama wanyama hakuna mwenye hata ndururu mfukoni. Kila mtu nyongo ya hasira ilianza kumpanda, tukagoma kuendelea kuchana mbao huku tukishauriana tutafute mteja wa zile mbao. Utasema alikuwa anatusikia, tajiri ghafla huyu hapa. Yule mzee nikama alikuwa anatumia madawa hivi, maana wote tuliingia baridi na tukasahau hata kama tunadai hela zetu.

Siku hiyo katununulia na kambuzi kakutudanganyishia na mchele. Mbao zikapakiwa akatuambia tupige hesabu tunamdai kiasi gani cha fedha, nasisi tukampa hesabu. Akachomoa kibunda akatupooza kidogo, yaani tushakaa wiki 7 katika hela tunayodai katulipa asilimia 5 alafu bado tuendelee kufanya kazi.

Nikaona huu sasa ni ujinga maana kila ukisema utafute mteja wa mbao hupati na ukimpata gari likija linakwama njiani. Fundi mmoja baada ya mwingine akaanza kuondoka bila ya kuaga. Kuja kushtuka nimeachiwa rengeta na chensoo niko mwenyewe. Nikajaa upepo sasa naondokaje na hapa kuna mali za watu. Tajiri naye baada ya siku mbili kaja kabeba mbao kaleta mafundi wengine. Namimi nikaondoka naye mpaka town, kanijizungusha wee mara aingilie huku mara atokee huku mwisho siku kaja kunilipa hela zangu zote saa 6 usiku.

Hela zilikuwa nyingi na nilipanga nianze biashara ya duka. Lakini hata wiki haikuisha hela zote zimekata ukiniuliza nilitumiaje mi mwenyewe sijuwi ila hela zilikata zote. Kesho yake nakutana naye mitaa ya majengo ananiambia ana kazi ya plasta nyumbani kwake niongozane naye, sahiyo nishasema sitofanya kazi naye tena ila nkajikuta kwake nimefika na kazi nimeanza ilikuwa kubwa ni ukuta wa uzio na vyumba 10 vya wapangaji huko shanti town.

Kazi niliuziwa hivyo nikaamua kulala hapo hapo saiti ila usiku ukilala unasikia mtu anabisha hodi, ukienda kufungua hakuna mtu mara unasikia milango mingine inafunguliwa yaani ni full mauzauza. Pesa za jamaa za moto, kazi yenyewe ya moto na hela nazitaka.

Nikasema acha nikomae mimi ni mtoto wakiume, lakini kila ukifanya kazi nikama haiendi vile unaeza ukachapia gara moja ukamaliza na kupiga kibao mara dongo lote linaachia ukutani. Au sanyingine uchapia dongo linaingia machoni macho yanawasha unaosha macho lakini wapi.

Msosi wa mchana ukila ukipumzika tu usingizi unakukamata kuja kushtuka unaamshwa ule cha usiku saa tatu usiku. Nikaomba nifungiwe taa ili niwe nakesha sasa usiku. Ila unaweza shangaa mara umeme umekatika nyumba nzima giza tupu kwa lisaa lizima, kwasababu ya uchovu unaamua kulala na kujipa matumaini kesho nayo siku. Ila ukilala tu unaota ndoto za ajabu ajabu sana sanyingine umetumbukia kwenye shimo la choo, mara ukabwe na jinamizi.

Siku hiyo ndo ilizidi kuwa mbaya maana baada ya mauza uza niliposhtuka nilikuta paka amekufa pembeni yangu na mimi nina chale mwilini. Usiku huo huo hata vifaa sikubeba niliondoka kurudi kwangu nakuona nikiendekeza tamaa ntauwawa huku.

Je, nini kitafuata usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Haya mambo ya kwenda ktk sherehe za wadau, ni hatari sana, tuwe makini, aisee jamaa ume pambana sana
 
Back
Top Bottom