Safari moja nje ya nchi imenigharimu zaidi ya laki nne(400,000) kwenye vipimo vya Corona tu

Safari moja nje ya nchi imenigharimu zaidi ya laki nne(400,000) kwenye vipimo vya Corona tu

trplmike

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
701
Reaction score
777
Nilikuwa na safari moja nje ya nchi. Kabla ya kuanza safari, nilitakiwa kupima Corona hapa Tanzania ambayo ni dola 100 (231,000), nilivyofika kwenye ile nchi (West Africa). Sheria ya ile nchi ilinilazimu nifanye self isolation kwa siku 7, then nikaenda kupima ile rapid test (ilikuwa Bure)

Wakati wa kurudi Tz, sheria inasema ni lazima nikapime Corona (Certificate inatakiwa kuwa valid ndani ya masaa 72), nilivyokwenda kupima nikalipa dola 50 (~ 115,000)

Nilivyofika Dar Airport, nikatakiwa tena kupima Covid , Ni lazima hata kama una certifacate ya masaa 72, Charge ni dola 25 (57,500)
Kwa hiyo nimejikuta natumia zaidi ya laki 4 kwa return trip moja tuu

Niinaisihi serikali ifikirie kupunguza gharama za kupima Covid kwa wasafiri, Mfano ile dola 100 ni kubwa sana

Ningewashauri waweke dola 25, (kwa wafanyabiashara na wagonjwa na wanafunzi wanaokwenda nje ya nchi kwa kipindi hiki ni Mzigo mkubwa sana
 
kwa sasa kusafiri nje ya nchi kunataka ujipange haswa , na kama hakuna umuhimu ni bora kutulia tu
pole kwa kifo cha pesa , i hope the trip was worth more than what you spent
 
Kama serikali za mataifa ndo wanaweka tahadhari kuthibiti kusambaa kwa magonjwa, iweje mzigo wa gharama abebeshwe mtu anayesafiri.....hivi wanasheria mnakwama wapi? mbona watu wanaonewa nyie mmepiga kimya....
 
Back
Top Bottom