Safari moja nje ya nchi imenigharimu zaidi ya laki nne(400,000) kwenye vipimo vya Corona tu

Safari moja nje ya nchi imenigharimu zaidi ya laki nne(400,000) kwenye vipimo vya Corona tu

Nadhani gharama kubwa imewekwa ili kudiscourage safari za nje zisizo na lazima.. kama ni hivyo basi iendelee kua hivyo.

Safari za nje kwa sasa si risk kwa msafiri pekee bali na kwa nchi msafiri anazotembelea.
 
Naomba kuuliza hii covid certificate inakuwa valid kwamuda gani?

Na iyo certificate serikali si inatoa kwa sh 30 elfu.
 
Afadhari yako wewe ulikuwa unaenda mbali kidogo,wenzako wanakwenda hapo Nairobi nao wanatumia laki 4 kwa kupimana makohozi
 
Pole sana kiongozi

OP; wakati trump anabana matumizi US nilimuunga mkono, aliwithdraw pesa zake kwenye shirika la kimarekani lililokua linafadhili miradi ya contraceptives. Aisee, tangu siku iyo nilijua effect ya US kwa serikali na labda mtu mmoja mmoja kama mimi ambaye nilikua affected na panga lake ambapo pesa zilikauka kwenye NGOs zilizokua zinategemea full sponsorship

Back to a topic; kila jambo serikali inafanya inafaa izingatie multiplied effects kwenye jamii. Mfano hapo kuna utalii kuja mchini, kuna wanafunzi, wagonjwa, conference attendees nk. Wote hapo hakuna hata mmoja asiye na umuhimu na safari yake ikizingatiwa sasa kwa dunia ilipo si rahisi sana kuwa isolated
 
You said it all
 
Wizi MTUPU!
Nilikuwa na safari moja nje ya nchi. Kabla ya kuanza safari, nilitakiwa kupima Corona hapa Tanzania ambayo ni dola 100 (231,000), nilivyofika kwenye ile nchi (West Africa). Sheria ya ile nchi ilinilazimu nifanye self isolation kwa siku 7, then nikaenda kupima ile rapid test (ilikuwa Bure),
Wakati wa kurudi Tz, sheria inasema ni lazima nikapime Corona (Certificate inatakiwa kuwa valid ndani ya masaa 72), nilivyokwenda kupima nikalipa dola 50 (~ 115,000)
Nilivyofika Dar Airport, nikatakiwa tena kupima Covid , Ni lazima hata kama una certifacate ya masaa 72, Charge ni dola 25 (57,500)
Kwa hiyo nimejikuta natumia zaidi ya laki 4 kwa return trip moja tuu
Niinaisihi serikali ifikirie kupunguza gharama za kupima Covid kwa wasafiri, Mfano ile dola 100 ni kubwa sana,
Ningewashauri waweke dola 25, (kwa wafanyabiashara na wagonjwa na wanafunzi wanaokwenda nje ya nchi kwa kipindi hiki ni Mzigo mkubwa sana
 
Shida Ni gharama za hizo reagents...zipo juu sana
 
Then booking inakupa appointment instantly? Majibu yanachukua muda gani?
Kuna long queue?
Msaada please bas
Wewe mwenyewe ndio unachagua muda na kituo cha kufanya kipimo. Normally majibu ni ndani ya 24hours.. wanakutumia kwenye email yako. Kisha una print ukienda pale airport muda wa kusafiri kuna mtu wao pale. Atakugonge mhuri. Mwanzoni wakati sehemu ya kupimia ilikuwa moja tuu .. pale National Lab. MABIBO .. Ilikuwa foleni kubwa sana..ila baada ya kuwapa hosp nyingi nyingi kupima foleni imepungua sana.. jitahidi kabla ya saa 7 uwe umepimwa
 
Biashara hii ni balaa, hapa kuna madalali wa chanjo hawalali kwa kupigia debe hizo chanjo hewa
 
Then booking inakupa appointment instantly? Majibu yanachukua muda gani?
Kuna long queue?
Msaada please based on your experience.
Booking ni instantaneous ila ni booking ya siku nzima sio specific time, queue inategemea unaenda kupimia hospital gani, ukienda pale Mabibo foleni ni kubwa ila una uhakika wa kupata majibu mapema zaidi, ukienda hospital binafsi kama Aga Khah au hospital za pembeni Mwananyamala na Amana foleni si kubwa.
Majibu ukipimia Mabibo maabara kuu ni 24-36hrs, Hospitali za Dsm nyingine ni around 48hrs, hospital za mikoani 48hrs, majibu yote yanatumwa kwa simu na email then uta print mwenyewe.
 
Back
Top Bottom