Safari ndefu ya Sheikh Ponda

Safari ndefu ya Sheikh Ponda

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Naangalia picha hiyo hapo chini ya Sheikh Ponda akiwa katika mkutano wa Vijana wa Kiislam uliofanyika Chuo Cha Biashara Dodoma (CBE) mwaka wa 1988 na naangalia video za Kampeni ya Uchaguzi 2020 Sheikh Ponda akisimama jukwaa moja na Maalim Seif na Tundu Lissu.

Narejea nyumna najikumbusha mengi aliyopitia Sheikh Ponda katika kupigania haki.

Leo kwenye Group moja ya rafiki zangu toka tuko shule ya msingi nimepewa onyo kuwa hawapendi wao kusoma habari za Ponda kwa hiyo kuna uwezekano wakanipumzisha wanasema hawataki siasa.

Jibu langu kwa Admin lilikuwa mbona kabla ya mimi kumweka Sheikh Ponda imewekwa picha ya Dr. Hussein Mwinyi ikiwa Group hii hiataki siasa?

Nikamuuliza Admn mbona ulikuwa kimya?

Basi kwa kutokuwa bughdha kwa wenzangu na katika kujiondolea fedheha ya kufukuzwa nikajipumzisha mimi mwenyewe yaani nika-''exit.''

Sheikh Ponda...
Screenshot_20201022-150716.jpg
 
Sheikh ponda ameamua kuimalizia heshima ndogo aliyobaki nayo

Ameamua kulamba matapishi yake ili mkono uende kinywani
Mkuu,Utafiti unaonesha tofauti. Uzoefu unaonesha tofauti. Ponda ameamua kuonesha msimamo wake wa wazi kama ambavyo wewe umeonesha wako kwa uwazi. Binafsi naamni kwamba JPM ana uzuri wake lakini hio haimaanishi kwamba wananchi lazima wamachague hapana. Kama wananchi wakiamua kumchagua LISSU sioni Tatizo isipokuwa kwa watu kama wewe ambao mnafikiri ni tatizo.

Tutambue kwamba mwisho wa siku hii ni nchi yetu wote na ni lazima tujadiliane namna tunataka itawaliwe na kuongozwa. Ni wajibu wetu.
 
Mkuu Tanzania hatuwezi kuongozwa na msaliti wa Nchi Lissu hiyo haitatokea hata mbingu zigeuke

Pia Tanzania hatutaki ushoga,
Mkuu unajua na kuelewa ushoga nini?Unajua na kuelewa msaliti ni mtu wa aina gani?
 
Ndio kama huu Mkuu, kwa taarfa yako kwa hii kasi ya Magufuli miaka mitano ijayo tutaipiku south Africa

Rais Magufuli ni mbeba maono ya Watanzania
Watu wananishi kwa vipande vya mihogona kachumbari,Nafasi moja ya ajira inakuwa na waombaji 10,000,Hospitali watu wanakufa kwa kukosa huduma.Mfumo wa huduma serikali umekuwa kama labour camp,wafanyakazi hawajongezewa mshahara hata senti tano pamoja na inflatio kuwa kubwa kwa miaka mingi.Katika yote hayo unaona kwamba tuko uchumi wa kati au tunarudi uchumi wa kijima?

Umetembea Posa uone maofisi yalivyobaki na BUndi na POPO.Umeenda kariako ulivyoona wamejaa wamchinga na mama ntilie fremu zoet zimefungwa?Unaona kweli au unahisi unaona.Ni kweli kwamba Kuna mambo Magufuli kafanya vyema lakini si kweli kwamba hakuna mwingine anayefaa kuwa RAIS wa hii nchi.SI KWELI kabisa.Lazima tukubali hilo ni tuache wananchi wafanye uamuzi kwa uhuru.
 
Nyie chadema kweli giza kichwani

Kula mihogo Ndio umasikini ? Unataka mtu ale mavyakula ya viwandani ndio useme anakula vizuri ?

Tatizo la ajira lipo hadi kwa Mabeberu mnaowaabudu

Ndio maana kwa kuona hilo Rais Magufuli ameamua kujenga miradi mikubwa itakayowezesha vijana kujiajiri

Hakuna serkali inayoajiri watu wote duniani fanya utafiti, ila inawawekea mazingira bora ya kujiajiri.
 
Nyie chadema kweli giza kichwani

Kula mihogo Ndio umasikini ? Unataka mtu ale mavyakula ya viwandani ndio useme anakula vizuri ?

Tatizo la ajira lipo hadi kwa Mabeberu mnaowaabudu

Ndio maana kwa kuona hilo Rais Magufuli ameamua kujenga miradi mikubwa itakayowezesha vijana kujiajiri

Hakuna serkali inayoajiri watu wote duniani fanya utafiti, ila inawawekea mazingira bora ya kujiajiri
Mkuu, Kwa hio ile miradi mikubwa imetoa ajira za kutosha kabisa?Miradi yenye si inasuasua mpaka imepoka pesa mtaani na kuzifungia chini? Matokeo yake mazingira ya ajira yameharibika. Kwa hio kwa sababi kwa mabeberu hakuna ajira basi na huyo Magufuli ni beberu pia?Kwa hio unataka watu wawe wankula mihogo ka nguchiro wakati wengine wanakula raha? Ndi sera yenu kama Chama?Ndio manchotaka watanzania wachague?Ndio ajenda yenu kwa miaka mitano ijayo na bado manumia kukiwa na mjadala wazi na wa uhuru? Kweli?
 
Miradi mikubwa imeanza kutoa matunda Kumbuka miradi mikubwa haichukui siku moja

Miradi mikubwa ikikamilika uwezo wa kujiajiri kwa kiwango kikubwa

Muwe mnawaambia viongozi wenu wa chadema wasiwe wanawadanganya
Mkuu,Kwa hio ile miradi mikubwa imetoa ajira za kutosha kabisa?Miradi yenye si inasuasua mpaka imepoka pesa mtaani na kuzifungia chini?Matokeo yake mazingira ya ajira yameharibika.Kwa hio kwa sababi kwa mabeberu hakuna ajira basi na huyo Magufuli ni beberu pia?Kwa hio unataka watu wawe wankula mihogo ka nguchiro wakati wengine wanakula raha?Ndi sera yenu kama Chama?Ndio manchotaka watanzania wachague?Ndio ajenda yenu kwa miaka mitano ijayo na bado manumia kukiwa na mjadala wazi na wa uhuru?Kweli?
 
Miradi mikubwa imeanza kutoa matunda Kumbuka miradi mikubwa haichukui siku moja

Miradi mikubwa ikikamilika uwezo wa kujiajiri kwa kiwango kikubwa

Muwe mnawaambia viongozi wenu wa chadema wasiwe wanawadanganya
Mkuu,Kwa mfano mradi wa SGR utazalisha ajira kias gani ukikamilika? Mradi wa stiegler Je utazalisha ajira kiasi gani? Takwimu zipo?
 
Watanzania hatuwezi kuongozwa na msaliti wa Nchi Lissu hiyo haitatokea hata mbingu zigeuke
Watanzania wamechoka kuongozwa na mtu mshamba (hii siyo mimi nasema, ni Nape Nnauye!).
 
SGR itazalisha ajira zaidi ya million 25

Na Mradi wa Stigila utazalisha ajira zaidi ya milion 15
Ajira Milioni 40?TAZARA NA TRC KWA PAMOJA ZIMESHINDWA KUZALISHA AJIRA 10,000 we unazungumzia ajira nyingi kulika labour force ya nchi.Kweli Tanzania tunasafari ndefu kama aina ya fikra kama hizi ndio inataka kutashawishi tupige kura kwa nani.Unaokuwa unamfanyia mgombea kampeni usifikir tu masalhi yako unayopata.Lazima uelewa sera za magombea wako uziamini na uzitete ukiwa na facts zaote.

Pembeni ya hapo unaweza kusababisha watu wamkatae kwa sababu tu ya uwezo wako mdogo wa kumtetea.ILA unajitahidi kubishana.Mimi nitampa kura Magufuli sio kwa sababu anafaa ila kwa sababu bado TUNDU LISU na CDM hawajakamilika kitaasisi.ILA KAMPENI YANGU NITAMPIGIA TUNDU LISU KWA SABABU NAAMINI KWAMBA LAZIMA TUWAPE NAFASI ILA YEYE PAMOJA NA CHAMA CHAKE WAJIJENGE WAKIWA NDANI YA DOLA.
 
Safari ndefu ya Ponda iko wapi?
 
Safari ndefu ya Ponda iko wapi?
"Naangalia picha hiyo hapo chini ya Sheikh Ponda akiwa katika mkutano wa Vijana wa Kiislam uliofanyika Chuo Cha Biashara Dodoma (CBE) mwaka wa 1988 na naangalia video za Kampeni ya Uchaguzi 2020 Sheikh Ponda akisimama jukwaa moja na Maalim Seif na Tundu Lissu.

Narejea nyumna najikumbusha mengi aliyopitia Sheikh Ponda katika kupigania haki.

Leo kwenye Group moja ya rafiki zangu toka tuko shule ya msingi nimepewa onyo kuwa hawapendi wao kusoma habari za Ponda kwa hiyo kuna uwezekano wakanipumzisha wanasema hawataki siasa.

Jibu langu kwa Admin lilikuwa mbona kabla ya mimi kumweka Sheikh Ponda imewekwa picha ya Dr. Hussein Mwinyi ikiwa Group hii hiataki siasa?

Nikamuuliza Admn mbona ulikuwa kimya?

Basi kwa kutokuwa bughdha kwa wenzangu na katika kujiondolea fedheha ya kufukuzwa nikajipumzisha mimi mwenyewe yaani nika-''exit.''"

Safari ya Sheikh Ponda kwangu mimi inaanza 1988 tulipofahamiana sote tukiwa vijana wadogo hadi leo mwaka wa 2020 namuona Ponda jukwaani anahutubia maelfu kwa maelfu ya Watanzania Ponda akiwa amebeba mgongoni kwake maelfu ya kura.

Hapa katikati ya miaka hiyo Sheikh Ponda kapigania haki za Waislam kiasi leo Waislam wanamtambua ndiye kiongozi wao kwani hakupata kuwa mzigo wa misumari kwao.

Gunia la misumari halibebeki kama walivyo masheikh wengine ambao kwa kuhofu kusimamia haki Waislam wamewapuuza.

Chadema na ACT Wazalendo wanaujua uwezo, nguvu na ushawishi alionao Sheikh Ponda na hii ndiyo sababu leo yuko jukwaani bega kwa bega na Tundu Lissu na Maalim Seif.

Hii ni safari ndefu.
 
Mkuu,Utafiti unaonesha tofauti. Uzoefu unaonesha tofauti. Ponda ameamua kuonesha msimamo wake wa wazi kama ambavyo wewe umeonesha wako kwa uwazi. Binafsi naamni kwamba JPM ana uzuri wake lakini hio haimaanishi kwamba wananchi lazima wamachague hapana. Kama wananchi wakiamua kumchagua LISSU sioni Tatizo isipokuwa kwa watu kama wewe ambao mnafikiri ni tatizo.

Tutambue kwamba mwisho wa siku hii ni nchi yetu wote na ni lazima tujadiliane namna tunataka itawaliwe na kuongozwa. Ni wajibu wetu.
Historia ya ponda Ingefaa uianzie kwa wazazi wake me asili yake ili tumuelewe vizuri
 
Historia ya ponda Ingefaa uianzie kwa wazazi wake me asili yake ili tumuelewe vizuri
Asili yake??Kama kawaida mtu akidai haki aitwa si Mtanzania.Swali ni Je PONDA anasimamia nini?Kama kile anachosimamia ni halali basi haijalishi asili yake ni IPI.Nafikiri ni wakati sasa tuanze kuitazama nchi yetu kama nchi yetu na sio kama nchi ambayo sio yetu
 
Back
Top Bottom