Safari ni ndefu. Angalia Barua hii

Safari ni ndefu. Angalia Barua hii

Ipo siku mtakubaliana na Mwana Mtoka Pabaya kuhusu hizi kasumba zetu na ushabiki.

Hawa tunaowacheka wala si kosa lao kwa 100%, haya ni malezi na makuzi ya kijinga. Watoto hawa wakute kwenye dala dala uone wanasoma nini, kama sio MAGAZETI YA UDAKU. Hakyanani kama vijana wetu wataendelea kuwa wapumbavu wa kutojua nini kizuri kwao na nini kibaya, basi hawa ndio wahitimu.
 
Last edited by a moderator:
tatizo siyo chuo..tatizo ni mtu mwenyewe.....chuoni hatufundishi mtu kingereza..ni taaluma husika eg Accounting,Finance
etc..ubovu wa yeye kutojua kingereza ni tatizo la maandalizi toka elimu ya chini huko primary na secondari.
Sasa wewe kama umesoma miaka 7+6=13 primary mpaka form 6 hukujua kingereza iweje kwa mika 2 ya collage ajue..
msikikiponde chuo..mpondeni mwenyewe na alikosoma madarasa ya chini....NIMEMALIZA.
 
Ataandikaje Press Release!!! Yaani mwandishi ni mtu wa Lugha sanifu!!! Ndiyo sifa yao kuu!! Sasa hapa itakuwaje? Ila usishangae kimemo kitampa kazi!!! Wenye taaluma ya ukweli hola!!
 
Kijana ana maarifa ya kutosha tu, kingereza siyo ujuzi na lugha tu ya kutolea ujuzi. Wengine huku nao wamekuwa malimbukeni wa lugha, wanashabikia vya wenzao na kuvitukuza utadhani mazuzu. Hamasisheni kiswahili kitumike vizuri watu wapate maarifa kwa lugha ya kiswahili, Wengine kingereza hawakijui wala kiswahili hawakijui
 
Wanafunzi wa miaka hii wanapenda njia za mkato. "Twishen" kwa sana! Ukiwapa vitabu vya kiada (textbooks), unapoteza pesa tu kwani hawavihitaji. Wanapenda kutafuniwa na kulishwa -- wao wameze tu!

Wanasoma ili tu wapate vyeti. Wanapenda kujua Kiingereza lkn hawapendi kujifunza! Funny! Wanataka kufika peponi lkn hawataki kufa!

sio hivyo..ni TUISHIENI
 
Kuandika tu barua ya maombi ndio hawezi ila ana kipaji cha utangazaji mwenzenu, mkuu ungeweka na chuo ili kisaidie wengine wasije kukosea njia wakaingia hapo.

Hapana bwana sifongo, sidhani kama chuoni mtu ndo anaenda kujifunza lugha!
Elimu ya lugha mtu hujifunza awapo level za chini za shule. Vyuoni watu huenda kupata ujuzi zaidi wa kazi..
 
Last edited by a moderator:
Hapana bwana sifongo, sidhani kama chuoni mtu ndo anaenda kujifunza lugha!
Elimu ya lugha mtu hujifunza awapo level za chini za shule. Vyuoni watu huenda kupata ujuzi zaidi wa kazi..

Ni kweli bwana mkubwa lakini amepataje vyeti ikiwa lugha ya kujifunzia hakuwa anailewa vizuri? hembu tuchukulie ndio amepata hiyo kazi tayari na ikatokea anatakiwa amfanyie mtu interview kwa lugha hiyo aliyoboronga itakuwaje?
 
mhhh i see your point!
Are you insinuating na waalimu wake pia ni walakini!??:confused2:
 
Utakuta kuandika hawezi lakini ana maneno!!!! Kama yule jamaa yetu wa Clouds!
 
hmmm....mnaweza msiamin ila hadi chuo kikuu,maprofessor wanalalamika wanafunzi hawawezi kujieleza.....hyo barua kweli ni kielelezo tosha.....elimu ya tanzaniz inahitaji major reforms.....ila sijui zitakujaje kama waziri wa elimu mwenywe anasema Tanzania ilikuwa ni mjumuisho wa Tanganyika na Zimbambwe???..
 
mwaJ Nafikiri tatizo ni mfumo wetu wa kuchagua wenye low scores ndo wawe Walimu. Mwalimu mwingine hisabati au maarifa vinampiga chenga,atawezaje fundisha mwingine amwelewe? Igawaje waalimu wazuri wapo, tena wazuri hasa.
 
Last edited by a moderator:
mwaJ Nafikiri tatizo ni mfumo wetu wa kuchagua wenye low scores ndo wawe Walimu. Mwalimu mwingine hisabati au maarifa vinampiga chenga,atawezaje fundisha mwingine amwelewe? Igawaje waalimu wazuri wapo, tena wazuri hasa.

Tatizo wale wenye high scores hawataki kuwa waalimu kwa sababu mfumo tulionao hauthamini waalimu. Wengi wanaenda kuwa waalimu baada ya kukosa nafasi nyingine. Serikali inatakiwa kutambua umuhimu wa waalimu na kuwalipa vizuri, makazi yao yawe bora, shule ziwe na majengo bora, madawati, vitabu, maabara na vitendea kazi vingine. Hapo watu wengi waliofanya vizuri katika masomo yao watakuwa tayari kufanya kazi ya kufundisha.
 
Kijana ana maarifa ya kutosha tu, kingereza siyo ujuzi na lugha tu ya kutolea ujuzi. Wengine huku nao wamekuwa malimbukeni wa lugha, wanashabikia vya wenzao na kuvitukuza utadhani mazuzu. Hamasisheni kiswahili kitumike vizuri watu wapate maarifa kwa lugha ya kiswahili, Wengine kingereza hawakijui wala kiswahili hawakijui

Nadhani huelewi unachoandika..........kama kiingereza kingekuwa sio tatizo basi hata hiyo barua ingeandikwa kwa kiswahili. Huyo mwanafunzi kasoma masomo yote kwa lugha ya kiingereza. Kiswahili ni lugha ya mtaani lakini sio lugha ya ofisini. Serikali sio mwajiri tena, waajiri ndio wanapenda kiingereza sasa soma kiswahili subiri ukaajiriwe serikalini. Kiswahili kitakuwa na nguvu pale uchumi wetu nao utakapokuwa na mguvu
 
Kwani akiandika kwa lugha fasaha ya kina kamerun ndio atakuwa na ufanisi mzuri kazini?
 
Kijana ana maarifa ya kutosha tu, kingereza siyo ujuzi na lugha tu ya kutolea ujuzi. Wengine huku nao wamekuwa malimbukeni wa lugha, wanashabikia vya wenzao na kuvitukuza utadhani mazuzu. Hamasisheni kiswahili kitumike vizuri watu wapate maarifa kwa lugha ya kiswahili, Wengine kingereza hawakijui wala kiswahili hawakijui

Uliyoyasema ndiyo ukweli kwa vijana wanaomaliza shule siku hizi. Hawajui Kiingereza wala Kiswahili. Kama kijana anaonyesha cheti kinasema kuwa amesoma Kiswahili au Kiingereza, au amesoma Udaktari au Uhandisi kutumia lugha ya kiingereza lakini bado hawezi kuonyesha uwezo wa hiyo lugha aliyosomea basi nitatilia shaka kama kweli alikuwa anaelewa alichokuwa anasomea.

Katika dunia ya leo kazi zote zinahitaji ujuzi wa lugha ndiyo maana wageni wengi ni rahisi sana kupata kazai Tanzania kwani wasomi wake wengi hawajui Kiingereza.
 
ukisitaajabu ya musa utayaona ya filauni
 
Back
Top Bottom