Safari ya Cameroon hatwendi: Watanzania wepesi wa kusahau

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Mwaka 2007 niliandika mara mbili katika barua za wasomaji katika gazeti lililokuwa likiitwa Spoti Starehe, gazeti dada la Majira. Sijui liko wapi gazeti lile siku hizi. Huenda ushindani wa kibiashara umeliondoa sokoni kama ilivyokuwa kwa Alasiri, Dar Leo, Kasheshe na magazeti mengine. Chini ya barua zile za wasomaji niliweka namba yangu ya simu na baada ya maoni yale kutoka nilipigiwa simu na watu wengi sana. Maoni yangu katika gazeti lile mara zote mbili yalihusu kwenda kwenye michuano ya AFCON nchini Ghana mwaka 2008.
Katika makala ya kwanza niliandika kuhusu kujiandaa mapema kama kweli tunataka kwenda Afcon Ghana. Katika makala ya pili nilizungumzia kuhusu "KANZU YA OUAGADOUGOU BURKINAFASO NA DHARAU ZETU KWA MSUMBIJI.
Nilisema kama kweli tunataka kwenda katika afcon lazima tufanye maandalizi ya kina lakini kama hatutafanya maandalizi hayo basi miji ya Accra, Kumasi, Tamale, Sekondi-Takoradi na mingine tutaisikia bombani.
Makala ya pili, niliandika baada ya watanzania wapenda soka wengi wao kuanza dharau baada ya Erasto Nyoni kumvika kanzu mchezaji wa timu ya Taifa ya Waburkinabe pale Ouagadougou, na kisha kuupeleka mpira kule anakotagia njiwa na Stars kushinda kwa bao 1-0 huku wakiwa pungufu baada ya nahodha Shadrack Nsajigwa kupewa kadi nyekundu.
Baada ya mechi ile kila mtu alikuwa anaamini kuwa Mamba wa Camarada Eduado Mondlane na Samora Moises Machel watafia katika dimba la Mkapa pale Temeke.
Matokeo yake jamaa mmoja hivi Mkongwe wa kuitwa Tico Tico akaunyamazisha uwanja mkuu wa Taifa. I was in the stadium that day.
Sasa tumesahau tena. Naona watu wameshaanza kupiga hesabu kama za mwaka 2007. Kuwa tungekwenda Ghana. Hatukwenda. Walikwenda watu wachache kama mashabiki tu na waandishi wa habari akiwemo mdogo wangu Edo Kumwembe ambaye akiwa huko akakutana na Rotter Mathews mchezaji fundi wa timu ya Taifa ya Ujerumani zamani. Taifa Stars yetu iliishia kwenda bungeni Dodoma tu.
Safari hii hatutakwenda Cameroon. Kwa nini? Kwa sababu tayari naona tumeshaanza kuona kuwa vijana kutoka Maseru na Korongo wa Entebbe ndiyo watatufanyia kazi ya sisi kwenda Yaounde na Douala. Watu wanapiga hesabu kuwa tunaenda kumpiga Lesotho kule Maseru kisha ndugu zake na Hamisi Kiiza Diego tunawakalisha pale kwenye wanja la Mchina! As simple as that. Yaani tunaona rahisi kabisa aisee.
International matches siyo kama mechi za Simba na Yanga kuwa wanapocheza na matawi yao kwamba Toto Africa ya Mwanza ipo tayari kumuachia Yanga aifunge ili Yanga achukue ubingwa hata kama wao vijana kutoka Kishamapanda wako hatarini kushuka daraja. Au Simba inapoamua kubebana na Tukuyu Stars na kutoka sare ya 5-5 ili timu nyingine ishuke daraja na wao wasalimike.
Uganda kama Uganda, Lesotho kama Lesotho na Cape Verde kama Cape Verde watataka heshima ya nchi zao. Mechi hizo ni ngumu sana kuliko vile baadhi ya watu wanavyofikiria.
Chondechonde wadau wa soka msije mkawaingiza wachezaji katika mkumbo huo kwa sababu umekuwa ukiwaathiri wachezaji. Mwaka 1980 katika kuwania nafasi ya kwenda fainali za Kombe la Dunia nchini Hispania zilizofanyika baadaye mwaka 1982, tulitoka sare ya goli 1-1 na Nigeria kule Surulele jijini Lagos Nigeria. Baada ya sare ile gazeti la Uhuru au Mzalendo kama sijakosea liliandika kuwa uwezo wa kuwafunga Nigeria tunao tena si chini ya bao 2-0. Badala ya kujiandaaa kwa ajili ya mechi ya marudiano tukabaki kusema Nigeria wakija hapa tutawafunga si chini ya bao mbili. The Green Eagles (wakiitwa hivyo wakati huo) walikuja na maji yao, vyakula vyao wapishi wao na wakawaita wachezaji wao waliokuwa wanacheza Ulaya mmoja wao namkumbuka akiitwa Babatunde Mudalwala. Matokeo yake tukapigwa sisi bao mbili huku Marquiz na DDC wakiwa ndani ya uwanja wa Uhuru wakihanikiza tuzipate zile bao mbili. Vyombo vya muziki vilikuwa vizito kwa bendi zote mbili. That was in 1980.
Mwaka 1984 kule Uganda kwenye Challenge Cup tulitakiwa tupate bao moja ili tuingie robo fainali katika mechi yetu na Uganda matokeo yake tulipigwa 4-0. Mmesahau? Waliuzeni Steven Nemes na Charles Boniface Mkwasa.
Tunataka kwenda kwa kina Etoo? Hapa lazima tukubali kuwa huenda tiketi yetu tuliiacha Chamazi siku ile usiku wa mechi yetu na Lesotho.
Cape Verde nao wanaweza kupindua meza Kibabe pale Nelson Mandela Stadium Namboole Kampala Uganda.
Tutegemee tulichonacho mkononi tusitegemee watakachotutafutia wenzetu.
Naomba msamaha kama kuna watu hawatanielewa au pengine nitakuwa nimewakwaza kwa njia moja ama nyingine kwa kusema hatutakwenda Cameroon.
Asanteni.

Dar es salaam, Tanzania
 
Dah umenishinda kwenye Historia Mkuu, nimeishiwa hoja, ila kikubwa tuwaombee wafanye mazoezi vizuri wajiandae vizuri tupate matokeo kwa Lesotho na Uganda..there isno way eti Mganda atuachie kirahisi hivyo ili tushiriki AFCON...na ikitokea hivyo basi tutaondoka kwa aibu sana huko C'roon
 
Wewe ndio unawaza hivyo kuwa tunataka kufanyiwa kazi na vijana wa Maseru na Entebe, mawazo yako yasiwe ya taifa zima. Kaa nayo!
Kameruni tunaenda, uganda tutapambana nae hapa kwetu na lesotho titaenda jihad huko kwao.
 
inawezekana na isiwezekene. nadhani wao wenyewe wamepevuka.. wanapaswa kujua mpira uwanjani na si vinginevyo. bahati nzuri vyomba vya habari kama viwili nimesikia vimesisitiza ukimtoa uganda. kwa wengine group letu bado liko wazi kwenye nafasi ya pili. so kila mchezaji wa tz anapaswa kujua hilo.
 
Dah umenishinda kwenye Historia Mkuu, nimeishiwa hoja, ila kikubwa tuwaombee wafanye mazoezi vizuri wajiandae vizuri tupate matokeo kwa Lesotho na Uganda..there isno way eti Mganda atuachie kirahisi hivyo ili tushiriki AFCON...na ikitokea hivyo basi tutaondoka kwa aibu sana huko C'roon
Mbona Museveni alisema Tanzania and Uganda is one country tulipotoa sare pale Nambole!!! Au alikuwa anatutania.
 
Unachokisema kiko sahihi na ni angalizo zuri.Lakini that was then and this is now.Ninachokubaliana na wewe ni kwamba tusitegemee Uganda sijui atufungie Cape hao sisi akili yote tuielekeze kwa Kuwafunga Lesotho bila Samatta,wachezaji wazoeshwe kushinda bila Samatta (Hilo la muhimu sana).Good news ni kwamba CAF wametoa ratiba mpya ambapo Uganda vs Cape ni 17 Nov halafu Tanzania vs Lesotho ni 18 Nov tukiwa tayari na matokeo ya Kampala,Rais wa CAF anatoka ukanda huu!!!!
 
Mwaka 2007 niliandika mara mbili katika barua za wasomaji katika gazeti lililokuwa likiitwa Spoti Starehe, gazeti dada la Majira. Sijui liko wapi gazeti lile siku hizi. Huenda ushindani wa kibiashara umeliondoa sokoni kama ilivyokuwa kwa Alasiri, Dar Leo, Kasheshe na magazeti mengine. Chini ya barua zile za wasomaji niliweka namba yangu ya simu na baada ya maoni yale kutoka nilipigiwa simu na watu wengi sana. Maoni yangu katika gazeti lile mara zote mbili yalihusu kwenda kwenye michuano ya AFCON nchini Ghana mwaka 2008.
Katika makala ya kwanza niliandika kuhusu kujiandaa mapema kama kweli tunataka kwenda Afcon Ghana. Katika makala ya pili nilizungumzia kuhusu "KANZU YA OUAGADOUGOU BURKINAFASO NA DHARAU ZETU KWA MSUMBIJI.
Nilisema kama kweli tunataka kwenda katika afcon lazima tufanye maandalizi ya kina lakini kama hatutafanya maandalizi hayo basi miji ya Accra, Kumasi, Tamale, Sekondi-Takoradi na mingine tutaisikia bombani.
Makala ya pili, niliandika baada ya watanzania wapenda soka wengi wao kuanza dharau baada ya Erasto Nyoni kumvika kanzu mchezaji wa timu ya Taifa ya Waburkinabe pale Ouagadougou, na kisha kuupeleka mpira kule anakotagia njiwa na Stars kushinda kwa bao 1-0 huku wakiwa pungufu baada ya nahodha Shadrack Nsajigwa kupewa kadi nyekundu.
Baada ya mechi ile kila mtu alikuwa anaamini kuwa Mamba wa Camarada Eduado Mondlane na Samora Moises Machel watafia katika dimba la Mkapa pale Temeke.
Matokeo yake jamaa mmoja hivi Mkongwe wa kuitwa Tico Tico akaunyamazisha uwanja mkuu wa Taifa. I was in the stadium that day.
Sasa tumesahau tena. Naona watu wameshaanza kupiga hesabu kama za mwaka 2007. Kuwa tungekwenda Ghana. Hatukwenda. Walikwenda watu wachache kama mashabiki tu na waandishi wa habari akiwemo mdogo wangu Edo Kumwembe ambaye akiwa huko akakutana na Rotter Mathews mchezaji fundi wa timu ya Taifa ya Ujerumani zamani. Taifa Stars yetu iliishia kwenda bungeni Dodoma tu.
Safari hii hatutakwenda Cameroon. Kwa nini? Kwa sababu tayari naona tumeshaanza kuona kuwa vijana kutoka Maseru na Korongo wa Entebbe ndiyo watatufanyia kazi ya sisi kwenda Yaounde na Douala. Watu wanapiga hesabu kuwa tunaenda kumpiga Lesotho kule Maseru kisha ndugu zake na Hamisi Kiiza Diego tunawakalisha pale kwenye wanja la Mchina! As simple as that. Yaani tunaona rahisi kabisa aisee.
International matches siyo kama mechi za Simba na Yanga kuwa wanapocheza na matawi yao kwamba Toto Africa ya Mwanza ipo tayari kumuachia Yanga aifunge ili Yanga achukue ubingwa hata kama wao vijana kutoka Kishamapanda wako hatarini kushuka daraja. Au Simba inapoamua kubebana na Tukuyu Stars na kutoka sare ya 5-5 ili timu nyingine ishuke daraja na wao wasalimike.
Uganda kama Uganda, Lesotho kama Lesotho na Cape Verde kama Cape Verde watataka heshima ya nchi zao. Mechi hizo ni ngumu sana kuliko vile baadhi ya watu wanavyofikiria.
Chondechonde wadau wa soka msije mkawaingiza wachezaji katika mkumbo huo kwa sababu umekuwa ukiwaathiri wachezaji. Mwaka 1980 katika kuwania nafasi ya kwenda fainali za Kombe la Dunia nchini Hispania zilizofanyika baadaye mwaka 1982, tulitoka sare ya goli 1-1 na Nigeria kule Surulele jijini Lagos Nigeria. Baada ya sare ile gazeti la Uhuru au Mzalendo kama sijakosea liliandika kuwa uwezo wa kuwafunga Nigeria tunao tena si chini ya bao 2-0. Badala ya kujiandaaa kwa ajili ya mechi ya marudiano tukabaki kusema Nigeria wakija hapa tutawafunga si chini ya bao mbili. The Green Eagles (wakiitwa hivyo wakati huo) walikuja na maji yao, vyakula vyao wapishi wao na wakawaita wachezaji wao waliokuwa wanacheza Ulaya mmoja wao namkumbuka akiitwa Babatunde Mudalwala. Matokeo yake tukapigwa sisi bao mbili huku Marquiz na DDC wakiwa ndani ya uwanja wa Uhuru wakihanikiza tuzipate zile bao mbili. Vyombo vya muziki vilikuwa vizito kwa bendi zote mbili. That was in 1980.
Mwaka 1984 kule Uganda kwenye Challenge Cup tulitakiwa tupate bao moja ili tuingie robo fainali katika mechi yetu na Uganda matokeo yake tulipigwa 4-0. Mmesahau? Waliuzeni Steven Nemes na Charles Boniface Mkwasa.
Tunataka kwenda kwa kina Etoo? Hapa lazima tukubali kuwa huenda tiketi yetu tuliiacha Chamazi siku ile usiku wa mechi yetu na Lesotho.
Cape Verde nao wanaweza kupindua meza Kibabe pale Nelson Mandela Stadium Namboole Kampala Uganda.
Tutegemee tulichonacho mkononi tusitegemee watakachotutafutia wenzetu.
Naomba msamaha kama kuna watu hawatanielewa au pengine nitakuwa nimewakwaza kwa njia moja ama nyingine kwa kusema hatutakwenda Cameroon.
Asanteni.

Dar es salaam, Tanzania
Wewe utakuwa unatokea Togo . Umeandika mambo mengi sana kiasi kwamba unajichanganya mwenyewe. Kocha na wachezaji wanajua wanafanya wanachokifanya . Achani kuleta porojo nyingi . Manabore sana .Cameroon tunaenda .
 
Mleta Uzi umefanya vema, tunahitaji kujiandaa haswa kama kweli Hugo nafasi tunaihitaji, habari ya kurahisishiwa Nazi na watu Fulani tusahau. Tuwaandae vijana wetu kisaiklojia kwenda kupambana. Ikibidi hata sisi twende na vyakula na vinywaji vyetu kama njia ya kujihami mambo ya nje ya uwanja. Sijui Tff uwaga na kawaida ya kupita humu? Huo ndiyo wasiwasi wangu
 
Mwaka 2007 niliandika mara mbili katika barua za wasomaji katika gazeti lililokuwa likiitwa Spoti Starehe, gazeti dada la Majira. Sijui liko wapi gazeti lile siku hizi. Huenda ushindani wa kibiashara umeliondoa sokoni kama ilivyokuwa kwa Alasiri, Dar Leo, Kasheshe na magazeti mengine. Chini ya barua zile za wasomaji niliweka namba yangu ya simu na baada ya maoni yale kutoka nilipigiwa simu na watu wengi sana. Maoni yangu katika gazeti lile mara zote mbili yalihusu kwenda kwenye michuano ya AFCON nchini Ghana mwaka 2008.
Katika makala ya kwanza niliandika kuhusu kujiandaa mapema kama kweli tunataka kwenda Afcon Ghana. Katika makala ya pili nilizungumzia kuhusu "KANZU YA OUAGADOUGOU BURKINAFASO NA DHARAU ZETU KWA MSUMBIJI.
Nilisema kama kweli tunataka kwenda katika afcon lazima tufanye maandalizi ya kina lakini kama hatutafanya maandalizi hayo basi miji ya Accra, Kumasi, Tamale, Sekondi-Takoradi na mingine tutaisikia bombani.
Makala ya pili, niliandika baada ya watanzania wapenda soka wengi wao kuanza dharau baada ya Erasto Nyoni kumvika kanzu mchezaji wa timu ya Taifa ya Waburkinabe pale Ouagadougou, na kisha kuupeleka mpira kule anakotagia njiwa na Stars kushinda kwa bao 1-0 huku wakiwa pungufu baada ya nahodha Shadrack Nsajigwa kupewa kadi nyekundu.
Baada ya mechi ile kila mtu alikuwa anaamini kuwa Mamba wa Camarada Eduado Mondlane na Samora Moises Machel watafia katika dimba la Mkapa pale Temeke.
Matokeo yake jamaa mmoja hivi Mkongwe wa kuitwa Tico Tico akaunyamazisha uwanja mkuu wa Taifa. I was in the stadium that day.
Sasa tumesahau tena. Naona watu wameshaanza kupiga hesabu kama za mwaka 2007. Kuwa tungekwenda Ghana. Hatukwenda. Walikwenda watu wachache kama mashabiki tu na waandishi wa habari akiwemo mdogo wangu Edo Kumwembe ambaye akiwa huko akakutana na Rotter Mathews mchezaji fundi wa timu ya Taifa ya Ujerumani zamani. Taifa Stars yetu iliishia kwenda bungeni Dodoma tu.
Safari hii hatutakwenda Cameroon. Kwa nini? Kwa sababu tayari naona tumeshaanza kuona kuwa vijana kutoka Maseru na Korongo wa Entebbe ndiyo watatufanyia kazi ya sisi kwenda Yaounde na Douala. Watu wanapiga hesabu kuwa tunaenda kumpiga Lesotho kule Maseru kisha ndugu zake na Hamisi Kiiza Diego tunawakalisha pale kwenye wanja la Mchina! As simple as that. Yaani tunaona rahisi kabisa aisee.
International matches siyo kama mechi za Simba na Yanga kuwa wanapocheza na matawi yao kwamba Toto Africa ya Mwanza ipo tayari kumuachia Yanga aifunge ili Yanga achukue ubingwa hata kama wao vijana kutoka Kishamapanda wako hatarini kushuka daraja. Au Simba inapoamua kubebana na Tukuyu Stars na kutoka sare ya 5-5 ili timu nyingine ishuke daraja na wao wasalimike.
Uganda kama Uganda, Lesotho kama Lesotho na Cape Verde kama Cape Verde watataka heshima ya nchi zao. Mechi hizo ni ngumu sana kuliko vile baadhi ya watu wanavyofikiria.
Chondechonde wadau wa soka msije mkawaingiza wachezaji katika mkumbo huo kwa sababu umekuwa ukiwaathiri wachezaji. Mwaka 1980 katika kuwania nafasi ya kwenda fainali za Kombe la Dunia nchini Hispania zilizofanyika baadaye mwaka 1982, tulitoka sare ya goli 1-1 na Nigeria kule Surulele jijini Lagos Nigeria. Baada ya sare ile gazeti la Uhuru au Mzalendo kama sijakosea liliandika kuwa uwezo wa kuwafunga Nigeria tunao tena si chini ya bao 2-0. Badala ya kujiandaaa kwa ajili ya mechi ya marudiano tukabaki kusema Nigeria wakija hapa tutawafunga si chini ya bao mbili. The Green Eagles (wakiitwa hivyo wakati huo) walikuja na maji yao, vyakula vyao wapishi wao na wakawaita wachezaji wao waliokuwa wanacheza Ulaya mmoja wao namkumbuka akiitwa Babatunde Mudalwala. Matokeo yake tukapigwa sisi bao mbili huku Marquiz na DDC wakiwa ndani ya uwanja wa Uhuru wakihanikiza tuzipate zile bao mbili. Vyombo vya muziki vilikuwa vizito kwa bendi zote mbili. That was in 1980.
Mwaka 1984 kule Uganda kwenye Challenge Cup tulitakiwa tupate bao moja ili tuingie robo fainali katika mechi yetu na Uganda matokeo yake tulipigwa 4-0. Mmesahau? Waliuzeni Steven Nemes na Charles Boniface Mkwasa.
Tunataka kwenda kwa kina Etoo? Hapa lazima tukubali kuwa huenda tiketi yetu tuliiacha Chamazi siku ile usiku wa mechi yetu na Lesotho.
Cape Verde nao wanaweza kupindua meza Kibabe pale Nelson Mandela Stadium Namboole Kampala Uganda.
Tutegemee tulichonacho mkononi tusitegemee watakachotutafutia wenzetu.
Naomba msamaha kama kuna watu hawatanielewa au pengine nitakuwa nimewakwaza kwa njia moja ama nyingine kwa kusema hatutakwenda Cameroon.
Asanteni.

Dar es salaam, Tanzania
Ni kwel kabisa safari ya kwenda Cameroon sio rahis kama tunavyodhani ukizingatia lesotho wamezidi kuimarika vzr licha ya juzi kufungwa na Uganda cha msingi game na lesotho maandaliz yaanze wiki mbili kabla ya match labda tunaweza kwenda kushinda au droo
 
Acha uchawi, historia zinawekwa na kuvunjwa
 
Tulizingua sana kutoa draw na hawa lesotho wabovu
 
Hatutegemei mtu.... njia pekee ya sisi kufuzu ni kushinda michezo yote ilio baki... kama iki tokea uganda aka mfunga cape verde basi itakua ni bahati pia kwetu... nili msikiliza samatta ana sema kinacho takiwa mi kushinda mechi zote
..hatu tegemehi uganda mkuu nafikiri ulitupata vibaya katika hili
 
Kwa bahati kivipi kwani tunapewa ushindi wa mezani au?
starz kwenda mataifa africa.. inawezekana.. ila ni kwa bahati tu.. sio kwa mpira wa uwanjani...

hatuma timu yenye kiwango cha kwenda mataifa africa... ila kwa bahati tunaweza kwenda
 
Back
Top Bottom