Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Mwaka 2007 niliandika mara mbili katika barua za wasomaji katika gazeti lililokuwa likiitwa Spoti Starehe, gazeti dada la Majira. Sijui liko wapi gazeti lile siku hizi. Huenda ushindani wa kibiashara umeliondoa sokoni kama ilivyokuwa kwa Alasiri, Dar Leo, Kasheshe na magazeti mengine. Chini ya barua zile za wasomaji niliweka namba yangu ya simu na baada ya maoni yale kutoka nilipigiwa simu na watu wengi sana. Maoni yangu katika gazeti lile mara zote mbili yalihusu kwenda kwenye michuano ya AFCON nchini Ghana mwaka 2008.
Katika makala ya kwanza niliandika kuhusu kujiandaa mapema kama kweli tunataka kwenda Afcon Ghana. Katika makala ya pili nilizungumzia kuhusu "KANZU YA OUAGADOUGOU BURKINAFASO NA DHARAU ZETU KWA MSUMBIJI.
Nilisema kama kweli tunataka kwenda katika afcon lazima tufanye maandalizi ya kina lakini kama hatutafanya maandalizi hayo basi miji ya Accra, Kumasi, Tamale, Sekondi-Takoradi na mingine tutaisikia bombani.
Makala ya pili, niliandika baada ya watanzania wapenda soka wengi wao kuanza dharau baada ya Erasto Nyoni kumvika kanzu mchezaji wa timu ya Taifa ya Waburkinabe pale Ouagadougou, na kisha kuupeleka mpira kule anakotagia njiwa na Stars kushinda kwa bao 1-0 huku wakiwa pungufu baada ya nahodha Shadrack Nsajigwa kupewa kadi nyekundu.
Baada ya mechi ile kila mtu alikuwa anaamini kuwa Mamba wa Camarada Eduado Mondlane na Samora Moises Machel watafia katika dimba la Mkapa pale Temeke.
Matokeo yake jamaa mmoja hivi Mkongwe wa kuitwa Tico Tico akaunyamazisha uwanja mkuu wa Taifa. I was in the stadium that day.
Sasa tumesahau tena. Naona watu wameshaanza kupiga hesabu kama za mwaka 2007. Kuwa tungekwenda Ghana. Hatukwenda. Walikwenda watu wachache kama mashabiki tu na waandishi wa habari akiwemo mdogo wangu Edo Kumwembe ambaye akiwa huko akakutana na Rotter Mathews mchezaji fundi wa timu ya Taifa ya Ujerumani zamani. Taifa Stars yetu iliishia kwenda bungeni Dodoma tu.
Safari hii hatutakwenda Cameroon. Kwa nini? Kwa sababu tayari naona tumeshaanza kuona kuwa vijana kutoka Maseru na Korongo wa Entebbe ndiyo watatufanyia kazi ya sisi kwenda Yaounde na Douala. Watu wanapiga hesabu kuwa tunaenda kumpiga Lesotho kule Maseru kisha ndugu zake na Hamisi Kiiza Diego tunawakalisha pale kwenye wanja la Mchina! As simple as that. Yaani tunaona rahisi kabisa aisee.
International matches siyo kama mechi za Simba na Yanga kuwa wanapocheza na matawi yao kwamba Toto Africa ya Mwanza ipo tayari kumuachia Yanga aifunge ili Yanga achukue ubingwa hata kama wao vijana kutoka Kishamapanda wako hatarini kushuka daraja. Au Simba inapoamua kubebana na Tukuyu Stars na kutoka sare ya 5-5 ili timu nyingine ishuke daraja na wao wasalimike.
Uganda kama Uganda, Lesotho kama Lesotho na Cape Verde kama Cape Verde watataka heshima ya nchi zao. Mechi hizo ni ngumu sana kuliko vile baadhi ya watu wanavyofikiria.
Chondechonde wadau wa soka msije mkawaingiza wachezaji katika mkumbo huo kwa sababu umekuwa ukiwaathiri wachezaji. Mwaka 1980 katika kuwania nafasi ya kwenda fainali za Kombe la Dunia nchini Hispania zilizofanyika baadaye mwaka 1982, tulitoka sare ya goli 1-1 na Nigeria kule Surulele jijini Lagos Nigeria. Baada ya sare ile gazeti la Uhuru au Mzalendo kama sijakosea liliandika kuwa uwezo wa kuwafunga Nigeria tunao tena si chini ya bao 2-0. Badala ya kujiandaaa kwa ajili ya mechi ya marudiano tukabaki kusema Nigeria wakija hapa tutawafunga si chini ya bao mbili. The Green Eagles (wakiitwa hivyo wakati huo) walikuja na maji yao, vyakula vyao wapishi wao na wakawaita wachezaji wao waliokuwa wanacheza Ulaya mmoja wao namkumbuka akiitwa Babatunde Mudalwala. Matokeo yake tukapigwa sisi bao mbili huku Marquiz na DDC wakiwa ndani ya uwanja wa Uhuru wakihanikiza tuzipate zile bao mbili. Vyombo vya muziki vilikuwa vizito kwa bendi zote mbili. That was in 1980.
Mwaka 1984 kule Uganda kwenye Challenge Cup tulitakiwa tupate bao moja ili tuingie robo fainali katika mechi yetu na Uganda matokeo yake tulipigwa 4-0. Mmesahau? Waliuzeni Steven Nemes na Charles Boniface Mkwasa.
Tunataka kwenda kwa kina Etoo? Hapa lazima tukubali kuwa huenda tiketi yetu tuliiacha Chamazi siku ile usiku wa mechi yetu na Lesotho.
Cape Verde nao wanaweza kupindua meza Kibabe pale Nelson Mandela Stadium Namboole Kampala Uganda.
Tutegemee tulichonacho mkononi tusitegemee watakachotutafutia wenzetu.
Naomba msamaha kama kuna watu hawatanielewa au pengine nitakuwa nimewakwaza kwa njia moja ama nyingine kwa kusema hatutakwenda Cameroon.
Asanteni.
Dar es salaam, Tanzania