Safari yangu ya kwenda magharibi ya Tanzania natarajia kuianza mwisho wa mwezi huu. Maandalizi ya safari yako kwenye hatua za mwisho mwisho na natarajia kutua Mwanza asubuhi kwenye saa 12 na kuunganisha kwa basi hadi Musoma kisha nitapita Tarime hadi Sirari.
Nitavuka mpaka na huenda nikalala Kisumu ili kesho yake niende Busia ambapo natarajia kuvuka mpaka wa Kenya kuingia Uganda. Hesabu zangu zinanionyesha kuwa ni mwendo wa masaa kati ya 12-14 kutoka Mwanza hadi kuipata Kampala....Tuombeane kheri.