Safari ya Dar es Salaam

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kuna bwana mmoja alikuwa na shauku ya kufika Dar. Katika umri wa miaka 30+ hajawahi kuliona jiji la Bashite.

Aliuza mazao yake na akiba aliyokuwa nayo na kukata ticket ya train. Akiwa njiani aliona nguo alizovaa hazistahili kuingia mjini.

Train ilisimama kituoni abiria washuke na kupanda. Jamaa aliwahi dukani kununua suruali, shati, boxer na t-shirt. Alilipa pesa na kufungiwa nguo kwenye Rambo.

Aliingia choo cha train na kuvua nguo zake na kuzitupa dirishani train ikiwa kwenye mwendo.

Alifungua Rambo na kukuta amefungiwa mashati manne tu.

Unafikiria alifanya nini?
 
[emoji1] [emoji1] [emoji23] [emoji23]
Huyo ni nani? Sio naniiii [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Hahahaha huyo aliendelea kua nzi wa choon[emoji23] [emoji23]
 
Kwa sababu hakuna anayemjua mjini,hapo naona angejifanya chizi tu ili mambo yaende sawa,Au mwana fashoooooooooooo....in nani sijui wa Nivãna voice'
 
Umenikumbusha story nilizowahi kusikia za Kariakoo Dar. Unaonyeshwa raba mtoni moja kali sana lakini ya mguu mmoja. Ukiamua kununua wanakufungia pembeni na kuhakikisha huoni na kukuonya usifungue kwani ukikamatwa na polisi utanyang’anywa. Ukifika home fungua viatu vyako ili ujinome ndiyo unakutana na bomu la uchafu uliofungiwa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…