Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kuna bwana mmoja alikuwa na shauku ya kufika Dar. Katika umri wa miaka 30+ hajawahi kuliona jiji la Bashite.
Aliuza mazao yake na akiba aliyokuwa nayo na kukata ticket ya train. Akiwa njiani aliona nguo alizovaa hazistahili kuingia mjini.
Train ilisimama kituoni abiria washuke na kupanda. Jamaa aliwahi dukani kununua suruali, shati, boxer na t-shirt. Alilipa pesa na kufungiwa nguo kwenye Rambo.
Aliingia choo cha train na kuvua nguo zake na kuzitupa dirishani train ikiwa kwenye mwendo.
Alifungua Rambo na kukuta amefungiwa mashati manne tu.
Unafikiria alifanya nini?