Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
_
Mwenyekiti wa MECIRA asema matunda ya safari ya Moscow na St. Petersburg yataonekana kupitia biashara, teknolojia, elimu, uwekezaji, ajira na masoko mapya ya bidhaa za Tanzania
MWENYEKITI wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jamvi Media Group, Habibu Mchange, ameipongeza ziara ya siku tatu ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi akisema ni miongoni mwa safari za kimkakati zenye uwezo wa kuifungulia Tanzania fursa mpya za biashara, uwekezaji, teknolojia, elimu na maendeleo ya kiuchumi kwa miaka mingi ijayo.
Mchange amesema ziara hiyo haipaswi kutazamwa kama ziara ya kawaida ya kiserikali, bali kama sehemu ya mkakati mpana wa diplomasia ya uchumi unaolenga kuitafutia Tanzania washirika wapya wa maendeleo, masoko mapya ya bidhaa zake na mitaji mipya ya uwekezaji.
“Safari ya Dk. Samia nchini Urusi ni zaidi ya ziara za kawaida, ni fursa, ni uwekezaji na ni sehemu ya kujenga mustakabali wa Tanzania katika dunia yenye ushindani mkubwa wa kiuchumi.
Tunapaswa kuitazama kwa jicho la maendeleo na si kwa jicho la matukio ya siku moja,” amesema Mchange.
Amesema ziara hiyo imefanyika katika wakati muhimu ambapo mataifa duniani yanazidi kutafuta masoko mapya, teknolojia mpya, washirika wapya wa maendeleo na njia mbadala za kukuza uchumi wao katika mazingira ya mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi duniani.
Kwa mujibu wa Mchange, Tanzania imeendelea kunufaika na sera ya diplomasia ya uchumi inayotekelezwa na Rais Samia, ambapo mahusiano ya kimataifa yanatumika kama nyenzo ya kuvutia uwekezaji, kuongeza biashara, kutafuta teknolojia na kufungua masoko mapya kwa bidhaa za Tanzania.
“Leo dunia imebadilika, nchi zinazofanikiwa si zile zinazojifungia ndani ya mipaka yake, bali zile zinazotafuta fursa kila mahali duniani. Hii ndiyo sababu tunaona Tanzania ikiendelea kujenga ushirikiano na mataifa mbalimbali makubwa duniani kwa lengo la kunufaisha wananchi wake,” amesema.
Mchange amesema moja ya mambo makubwa yaliyoifanya safari hiyo kuwa ya kihistoria ni ukweli kwamba imefanyika takribani miaka 57 baada ya ziara ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, nchini humo mwaka 1969, huku ikifanyika pia katika kipindi ambacho Tanzania na Urusi zinaendelea kuimarisha mahusiano yao ya muda mrefu ya kidiplomasia.
Amesema akiwa jijini Moscow, Rais Samia alipata nafasi ya kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, pamoja na viongozi wengine wa serikali ya Urusi kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Kwa mujibu wa Mchange, mazungumzo hayo yaligusa maeneo muhimu yanayoweza kuleta manufaa makubwa kwa Tanzania ikiwemo biashara, uwekezaji, nishati, madini, kilimo, elimu, sayansi, teknolojia, utalii na maendeleo ya miundombinu.
“Tunapozungumzia Urusi tunazungumzia moja ya mataifa makubwa duniani yenye uchumi unaozidi dola trilioni mbili za Marekani, watu zaidi ya milioni 140 na uwezo mkubwa katika sayansi, teknolojia, nishati, madini na viwanda, hivyo, kila hatua ya kuimarisha ushirikiano na taifa hilo inafungua milango mipya ya fursa kwa Tanzania,” amesema.
Mchange amesema moja ya matukio muhimu zaidi katika ziara hiyo ilikuwa ushiriki wa Rais Samia katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF), ambalo ni miongoni mwa majukwaa makubwa zaidi duniani yanayowakutanisha viongozi wa serikali, wawekezaji, wafanyabiashara wakubwa na taasisi za fedha kutoka mataifa mbalimbali.
Amesema kupitia jukwaa hilo, Tanzania ilipata fursa ya kuwasilisha mbele ya dunia maeneo yake ya kimkakati ya uwekezaji na biashara, huku ikijitangaza kama moja ya nchi zenye mazingira mazuri zaidi ya uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“SPIEF si mkutano wa kawaida huko ndiko makampuni makubwa yanakutana, wawekezaji wanatafuta fursa na nchi zinajiuza kwa ulimwengu.
Soma Pia: Rais Samia aziwasilisha fursa kubwa kutoka kwenye sekta tano kwenye jukwaa la kiuchumi Urusi
Uwepo wa Tanzania katika jukwaa hilo ni jambo kubwa kwa sababu unaipa nchi yetu nafasi ya kuonekana na kusikika mbele ya wadau muhimu wa maendeleo ya uchumi wa dunia,” amesema.
Mchange amesema biashara kati ya Tanzania na Urusi bado iko chini ya uwezo wa mataifa hayo mawili licha ya kuendelea kukua kila mwaka. Kwa sasa, thamani ya biashara baina ya nchi hizo mbili inakadiriwa kufikia zaidi ya dola za Marekani milioni 300 kwa mwaka, kiwango ambacho amesema kinaweza kuongezeka mara kadhaa ikiwa fursa zilizopo zitatumika kikamilifu.
“Ukichukua ukubwa wa uchumi wa Urusi wenye zaidi ya dola trilioni mbili na soko la watu milioni 140, utaona wazi kwamba bado kuna nafasi kubwa sana ya kukuza biashara kati ya nchi hizi mbili, hii ndiyo sababu ziara ya Rais Samia ni muhimu kiuchumi,” amesema.
Kwa mujibu wa Mchange, Tanzania ina bidhaa nyingi zinazoweza kupata soko kubwa nchini Urusi ikiwemo kahawa, chai, korosho, tumbaku, pamba, katani, viungo, matunda ya kitropiki, samaki na mazao mengine ya baharini.
“Leo Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa korosho duniani. Tuna kahawa inayoheshimika duniani, tuna chai, viungo vya Zanzibar, matunda na mazao mengi ya kilimo.
Tukipata hata sehemu ndogo ya soko la Urusi, wakulima wetu wataona matokeo yake moja kwa moja kupitia ongezeko la mahitaji na bei nzuri za mazao yao.”
Amesema faida kwa Tanzania haitaishia kwenye kuuza mazao ghafi pekee bali itaongezeka zaidi iwapo taifa litawekeza katika kuongeza thamani ya mazao hayo kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
“Tunataka kuuza kahawa iliyochakatwa, korosho zilizoongezwa thamani, matunda yaliyosindikwa na bidhaa nyingine za viwandani.
Hapo ndipo ajira nyingi na mapato makubwa yanapatikana.”
Kwa upande mwingine, amesema Tanzania inaweza kunufaika kwa kupata teknolojia za kisasa, mashine za viwandani, utaalamu wa uzalishaji pamoja na pembejeo muhimu za kilimo kutoka Urusi.
Katika sekta ya kilimo, Mchange amesema ushirikiano na Urusi unaweza kusaidia kuongeza upatikanaji wa mbolea kwa bei nafuu na kwa uhakika zaidi kutokana na nafasi ya nchi hiyo kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mbolea duniani.
“Wakati dunia ikikabiliwa na changamoto za upatikanaji wa pembejeo za kilimo kutokana na migogoro ya kimataifa, Tanzania inahitaji kujenga ushirikiano wa muda mrefu utakaosaidia wakulima kupata mbolea kwa uhakika na kwa gharama zinazoweza kumudu.”
Amesema sekta ya nishati nayo ni eneo muhimu ambalo Tanzania inaweza kunufaika kutokana na uzoefu mkubwa wa Urusi katika mafuta, gesi asilia, uzalishaji wa umeme na teknolojia za nishati.
Kwa mujibu wake, Tanzania ambayo tayari ina akiba ya gesi asilia inayokadiriwa kufikia futi za ujazo trilioni 57.5 pamoja na mipango ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa LNG, inahitaji ushirikiano wa karibu na mataifa yenye teknolojia na uzoefu mkubwa ili kuongeza thamani ya rasilimali hizo.
Katika sekta ya madini, Mchange amesema Tanzania ina utajiri mkubwa wa dhahabu, grafaiti, nickel, almasi, makaa ya mawe, uranium pamoja na madini adimu yanayotumika katika teknolojia za kisasa na uzalishaji wa betri za magari ya umeme.
“Urusi ina uzoefu mkubwa katika uchimbaji, usafishaji na uchakataji wa madini.
Ushirikiano katika eneo hili unaweza kusaidia kuongeza thamani ya madini yetu kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, jambo ambalo linaweza kuongeza mapato ya taifa na ajira kwa Watanzania.”
Mchange amesema ushirikiano huo si wa upande mmoja kwa sababu Urusi nayo itanufaika kwa kupata soko jipya la bidhaa zake pamoja na mshirika muhimu katika Afrika.
Ameeleza kuwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, Reli ya Kisasa ya SGR pamoja na nafasi ya Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Tanzania inaweza kuwa lango muhimu kwa biashara za Urusi kuingia katika soko la zaidi ya watu milioni 500 wa Afrika Mashariki na Kusini.
“Urusi inahitaji masoko mapya, washirika wapya na njia mpya za kufikisha bidhaa zake katika masoko ya Afrika.
Tanzania inahitaji teknolojia, mitaji na uwekezaji hapo ndipo ushirikiano wa kweli wa pande zote mbili unapopatikana,” amesema.
Amesema eneo lingine muhimu ni elimu na maendeleo ya rasilimali watu ambapo kwa miaka mingi Urusi imekuwa ikitoa mafunzo kwa wanafunzi kutoka Tanzania katika taaluma za uhandisi, tiba, sayansi, jiolojia, teknolojia na sekta nyingine muhimu za maendeleo.
Kwa mujibu wa Mchange, kutunukiwa kwa Rais Samia Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi (RUDN) ni ishara ya heshima ambayo Tanzania inaendelea kuijenga katika jukwaa la kimataifa na inaweza kuwa daraja la kuimarisha zaidi ushirikiano wa elimu kati ya nchi hizo mbili.
“Diplomasia hufungua mlango, lakini uchumi huingia kupitia mlango huo, kazi iliyobaki sasa ni kwa taasisi zetu, wafanyabiashara wetu na wawekezaji wetu kuhakikisha kuwa fursa zilizofunguliwa Moscow na St. Petersburg zinageuzwa kuwa miradi halisi, biashara halisi, ajira halisi na maendeleo halisi kwa Watanzania,” amesema.
Amesisitiza kuwa historia ya ziara hiyo haitahukumiwa kwa yaliyotokea ndani ya siku tatu pekee, bali kwa matokeo yatakayoonekana katika miaka ijayo kupitia ongezeko la uwekezaji, biashara, ajira, teknolojia na ukuaji wa uchumi wa taifa.
“Ndiyo maana nasema safari hii ni zaidi ya ziara za kawaida. Ni fursa, ni uwekezaji, na inaweza kuwa moja ya hatua muhimu katika kujenga Tanzania ya kesho,” amesema Mchange.