Hatua ya 2: Dar – Morogoro – Dodoma paka musom final destination
Safari ilianza saa 4 :45 alfajiri. Kabla ya kutoka Dar: maeneo ya airpot
Tuliweka full tank (~60 litres) kwa Tsh 180,000
Ilitufikisha maeneo ya karibu na Dodoma (~600km) kwa consumption ya wastani wa 10km/litre
Matukio:
Barabara ya Dar hadi Morogoro iko safi.
Tulipumzika Morogoro kwa chai na kuendelea hadi Dodoma.
Tulifika Dodoma mida ya saa 9 alasiri – gari ilikuwa bado stable, consumption iko poa.
Hatua ya Pili: Dodoma – Singida – Nzega – Bariadi – Bunda – Musoma
Baada ya mapumziko mafupi Dodoma, safari iliendelea:
Nzega: Tuliweka mafuta ya Tsh 90,000 (30 litres)
Bunda: Tukaongeza Tsh 45,000 (15 litres)
Jumla ya mafuta njiani: Tsh 135,000
Pamoja na full tank ya Dar: Tsh 180,000
Jumla ya mafuta yote: Tsh 315,000 (lita 105)
Takribani masaa 18 paka 20 kama ni non stop Matukio:
Tulisaidia jamaa mmoja aliyeishiwa jack – tukampatia yetu.
Askari wa doria maeneo ya Bunda walitupokea vizuri na kututakia heri.
Tulifika Musoma saa 4 asubuhi maana tulilala safari ilikua na uchovu atari
Breakdown ya Gharama ya Safari 3 Watu na mizigo kadhaa
Je, Full Tank Inatosha Dar hadi Musoma?
Hapana.
Full tank ya lita 60 inakufikisha takriban 600km pekee.
Safari yote ni kama na zaid~1,300km, hivyo unahitaji 2 full tanks na ujazo wa lita 15 hivi kufika salama.
Ushauri kwa Wasafiri Wengine:
Hakikisha una spare tyre, jack nzuri, triangle, fire extinguisher, na maji ya akiba.
X-Trail T31 ilijitahidi – hata kwenye barabara za vumbi na rough.
Roadtrip kama hii inahitaji uvumilivu na kujipanga – lakini inafundisha mengi.