Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Wanatukamata mkuu tukifanya hivyo.

Jana wamekamata watu Hospitali ya Temeke waliokuwa wanachangia damu
Tunakwenda bila kuonesha tunaandamana wa kama kundi ila baada ya damu kupatikana watatoa taarifa ya kiasi cha damu na ndipo kampeni yetu itakuwa imefanikiwa......
 
Tunakwenda bila kuonesha tunaandamana wa kama kundi ila baada ya damu kupatikana watatoa taarifa ya kiasi cha damu na ndipo kampeni yetu itakuwa imefanikiwa......
Ahaaa.

Hapo sawa
 
Ndungai nakumbuka alivyomchapa bakora mwana ccm mwenzake kwenye kura za maoni niliangalia huyu MTU ana elimu gani ? Nikaona ni bwana mifugo/agromechanics na kuoña na ule mhimili mwingiñe umeshikwa na mtaalamu wa bansen burner nikajuwa tumekwisha kama nchi
 
Halafu Ndugai ni very bright toka high school nilishasikia simuliz zake kutoka kwa masela. Naskia darasan zilikuwa zinacharge balaa. Nikati ya wakufunzi wachache tunao bongo. Tatizo sasa tunasoma tupite mitihani siyo kuelimika.

Mbaff!
ADUI wa NCH hii ni CCM Sema watu hawataki kuelewa
 
Nasubiria kumwona Mh. Supika akimjibu [HASHTAG]#barafu[/HASHTAG] leo
 
Ndugu Barafu katika uzi huu umeandika kwa hisia sana, pole na wewe pia kwa uchungu ulionao juu ya haya mambo. Tuendelee kumuombea TL.
Mkuu,hata kama wengine sisi sio wanasiasa na kuna wakati hatukubaliani na Tundu Lissu,lakini ubinadamu kitu cha muhimu sana...Kabla ya vyeo na mali,tulianza kwanza kuwa binadamu!!Ubinadamu uanze,mengine yawe kwa ziada
 
Kumbuka LISU hakuwa anaumwa MARALIA.....kwa muono wako Zuri lipi taratibu za Bima ya AFYA zafuatwe LISU afe au zisifuatwe kama ilivyofanyika Aishi Kama ilivyosasa Msifanye Utani na Maisha ya watu.....! Sisi tutachanga na atatibiwa atapona kabisa.. aturudi mjini kuendelea na Harakati zake mtaaibika sana...
 
Huu nao ni ujinga ugonjwa unaulinganisha na shule...
 
Halafu kama wamelipa jana kwa nin invoice imeankwa tarehe 7/9/2017?
 
RESPECT! Heshima kwa mkuu Barafu! Kama ni nondo basi viwango vyake si vya sayari hii! Ni vya sayari nyingine kabisa! Ni nondo za kufunga vinywa na mjadala! Once again high RESPECT! Nondo zilizojaa utu!
 
Acha kujifanya huelewi, na kama huelewi uombe ufahamishwe uache ubishi usio na msingi, Muhimbili au Agakhan kwa sasa ni Hospital bora kuliko zote katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, hat huko Nairobi walikompeleka kwa sasa tunapokea wagonjwa wengi kutoka kwenye nchi hizo kuja kuhudumiwa hapa Tanzania, nenda Jakaya Kikwete Cardiac Institute, au Ocean road cancer institue, au KCMC uone na uzungumze na wakenya walivyojazana kufuata huduma. Acha kuishi kizamani, kwa sasa Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika fani ya tiba kuliko nchi zote za ukandaa huu, na kama ulimsikiliza vizuri Mbowe alisema hana wasiwasi wowote na ubora za huduma hapa nchini, kilichowafanya waende Kenya ni sababu za kiusalama, sasa kwanini wasitumie blue guards na walinzi wengine wa chadema kumlnda kipindi chote akiwepo hapo Hospitalini?, Mbona yule Generali wa jeshi aliyepigwa risasi anahudumiwa Lugalo na hali yake inaendelea vizuri?

Kwa taarifa yako, kama risasi hazijapiga kichwani, shingoni, kifuani au kuchanachana Ini, basi mgonjwa hayuko katika hatari sana hasahasa akiwaishwa Hospitalini na kuwekewa damu haraka kama ilivyofanyika kwa Lisu na yule jenerali mstaafu, wakati anapelekwa Nairobi tayari hali yake ilikuwa stable(all vital signs were stable), kwamba BP ilikua normal, oxygen concentration, breathing parten, kidogo renal functions zilikua altered kwa sababu ya less renal poerfussion because of bleeding, lakini baada ya kumuwekea damu na maji ikajirekebisha.

Nani amewakataza msimuhudumie, fanyeni mpendavyo ila msilalamikie mtu, mkitaka ahudumiwe na serikali ni lazima sheria na taratibu za nchi zifuatwe, sheria tumejiwekea lazima zifuatwe, kungeonekana kwamba maisha ya Lisu yapo hatarini wala asingepelekwa Kenya, angepelekwa India, kwa sababu hao wakenya wenyewe hawaendi hapo alipopelekwa Lisu, wao pia hukimbilia India viongozi wao wakihitaji matibabu, wanawashangaa walioamua kumpeleka Kenya
 
Huu nao ni ujinga ugonjwa unaulinganisha na shule...
Akili ndogo kamwe haziwezi kuelewa mithali za kiutu uzima, tukisema mpanda farasi wawili hupasuka msamba, ulishawahi kuona mtu anayepanda farasi wawili kwa wakati mmoja?, sasa kama ubongo wako umelala kiasi hicho cha kushindwa kutumia mifano na kuirudisha katika mada tukusaidieje?
 
Halafu kama wamelipa jana kwa nin invoice imeankwa tarehe 7/9/2017?
Tatizo lako wewe huna uelewa wa basic knowledge kabisa unaendekeza ubishi badala ya kutaka ueleweshwe, invoice is request for payment, while receipt is the proof for payment, mwambie huyo Msigwa aonyeshe risiti waliyolipia hiyo $9,200 tuone tarehee yake. Tatizo la watanzania wengi ni kutosumbua vichwa vyao katikw kufikiria kwa undani wanaendeshwa na ushabiki na kusikiliza maneno ya mitaani, tubadilikeni dunia inatuacha
 
[emoji90]
 
Umeshaeleweka!!Punguza kumjadili sana na kusimanga hali ya ugonjwa wa mtu
 
Daah! inasikitisha sana hasa hapo ambapo kitanda cha mgonjwa kinachezacheza huku drip ikiwa imeshikiliwa na daktari.

Hii itakua iliwaweka katika hali ya wasiwasi sana akina Mbowe na wenzake juu ya hali ya mgonjwa.

Mungu amponye Lissu.
 
barafu bna .unajuaga kunihuzunisha ila nikikuomba unitoe hapa nchini hata nikawe beki tatu kwa dk slaa huko hutaki.sawa tu acha nife katika udhalimu

Aise nilikuwa na huzuni karibu kulia nilipomsoma barafu ila nimefika hapa kwako ilibidi nicheke tu!jamani kuna watu mnajua kuchomekea vitu...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…