Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Nimesikitika sana,sikutegemea mjomba wangu Ndugai aongee vile leo alivyoongea!!

Pia hakuna kitu kimeniuma sana kama nilivyosikia Ndugai alikuwa kwenye ile kamati ya bunge iliyokwenda nyamongo kisha kupindisha ukweli eti maji ya mto hayakuwa na sumu lakini wananchi walipowataka wabunge wa kamati ile waguse maji wabunge wote waligoma. Halafu leo hii Ndugai anasimama na kujifanya mzalendo eti anapigania raslimali za taifa huku akisahau Lissu ndio aliyekuwa akiwatetea wananchi wa nyamongo dhidi ya sumu ile kwenye mto. Halafu ukimsikia anavyozunguza kwa kejeli na ulevi wa madaraka huku akiwananga wapinzani kwamba ndio kipimo cha kutokuwa dhaifu. Yaani hajui hata udhaifu uko kwenye nini.
 
Safi sana Mkuu Barafu! Heshima mbele, endelea kunyoosha mambo. chukua KUMI zangu!!
 
Barafu, Mungu awabariki nyote ambao mlitoa michango ya namna mbalimbali kumfanya mpendwa wetu Lisu aweze kupata matibabu. Hatuna maneno mazuri ya kusema. Hamkutenda kwaajili ya Lisu bali kwaajili yetu sote tuliopatwa na simanzi kubwa katika tukio hili.

Mungu wetu tunaomba usikie maombi yetu, ni maombi yetu sisi wenye huzuni, siyo maombi ya Tundu Lisu. Kama ulimfufua Lazaro, kama uliwaponya viwete, vipofu na wengine wengi, kwa nini isiwezekane kwa Lisu? Tunajua katika wewe Mungu wetu hakuna usiloliweza, ukitaka, mpendwa wetu anaweza kusimama wakati wowote.

Wewe ulisema, 'Ombeni mtapewa', tunajua wewe ni mwaminifu katika ahadi zako. Tunaomba kwaajili ya uhai na afya ya Mpendwa wetu Tundu Lisu.

Tena ulisema, 'Tafuteni mtapata', tunakutafuta wewe uliye asili ya yote, umjalie uzima na afya ndugu yetu Tundu Lisu, aliyepo kitandani, si kwa mapenzi yako bali kwa mapenzi ya ibilisi.

Bwana wetu ulituambia, 'gongeni mtafunguliwa', tunagonga kwenye nyumba ya mamlaka yako ili mkono wako wenye nguvu ukamguse na kumnyanyua ndugu yetu Tundu Lisu.

Ni mapenzi yetu, ndugu yetu arejee katika hali yake lakini kwa mapenzi yako katika haya mateso anayoyapitia, unaweza kumvusha, hata akatoka akawa bora zaidi kama ilivyokuwa kwa Ayubu. Mapenzi yako yatimizwe, sasa na hata milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
barafu

Katika nchi inayofuata sheria, Ndugai alitakiwa kufungwa jela baada ya kumshambulia mtu kwa bakora katika kampeni.

Hakufaa kuwa hata mbunge,licha ya Spika. Alitakiwa kuwa jela.

Ila hapo Tanzania, chama kama CCM hakijui scandal ni nini, mtu kama Ndugai aliyetakiwa kwenda jela, sio tu kapewa nafasi kugombea ubunge,kapewa Uspika pia.

Mimi sishangai akiwa mzushi mzushi, mjivuni jivuni, limbukeni limbukeni, na muongo muongo.Vitendo vyake vya nyuma havinipi shaka kwamba anaweza kuwa hivi.
 
Nakumbuka Ndugai alivyotoka India, Mbowe alienda kumsalimia kabla ya viongozi wengine wa Ccm kwenda kumsalimia.
Utu ni kitu cha thamani sana, tatizo ulevi wa madaraka ndio unafanya watu wengine waonekane kama sio binadamu na hawafai kuishi.
Mungu ni mwema ndio maana mpaka sasa TL yuko hai na iko siku atasimama na kutaja jinsi Mwenyenzi Mungu alivyomuokoa kwenye dimbwi ka mauti.
 
Bahati nzuri tu ni kwamba Mungu anajitofautisha na mwanadamu katika masafa ya kufikiri na kutenda. Mara zote yeye anaanzia sisi tunapoishia. Vinginevyo tungeweza kuongea mangine kabisa muda huu.Kwa jinsi watu walivyomuombea Ndugai kwa sauti na ukimya halafu baada ya kupona eti amerudia jeuri zake nina imani Mungu angekuwa mwanadamu angefuta uponyaji aliomufanyia.

Kuna watu wanadharau sana Facility ya kuungama dhambi kwa Mamlaka ya Kanisa lakini Yesu alipoweka nafasi yeye kama hiyo alijua mambo kama haya ya akina Ndugai.Ndugai yangetokea.Alijua akili kama za akina Ndugai zipo duniani. Huyu Ndugai angekuwa ni mtu anatambua na anao uelewa mpana juu ya Sakramenti ya Upatanisho lazima angeenda kuungama hiyo dhambi. Bahati mbaya sana dhambi zake "anaungamia" kwenye kiti chake cha uspika.

Ndugai, uzima ulevya na ugonjwa ulegeza. Huna madaraka ya kutambia wenzio isipokuwa kama usilingalipewa na huyo akaaye Juu. Usingalivaa mavazi ya Kifalme kama Spika kama Yeye aliye mwanzo na mwisho Wa Ufalme asingalikupatia ufalme huo.
 
Sheiza, kama unaakili timamu utafuta huu uchafu uliouweka hapa na kumuomba radhi kila aliyeusoma! Tanzania ni ya watanzania na sio kikundi kidogo unachokishabikia, Ndugai na wote wanaodhani wanahati miliki ya uhai wanajidanganya. Hata hao waliopanga na kutekeleza shambulio dhidi ya Lisu dhamila zitawatesa mpaka wafe! Hawata kaa waonje raha na amani mioyoni mwao milele. Wewe unayeshangilia hapa kwa ujinga wako hutakaa ulione hilo kwani hawatakuambia mateso wanayo yapata.
 

Ndiyo maana ya uhuru wa kutoa maoni...

Angalia na soma tena na tena ulichokiandika, uone ambavyo huna tofauti na Job Ndugai na Spika wa bunge....

Lakini unaheshimiwa na tunaheshimu maoni yako....

Asante kwa kuja, na karibu tena wakati mwingine kutoa maoni yako...!!
 
Barafu,
Shukrani kwa kuweka mambo yote peupe na ndiyo maana Jamiiforums na wadau wake wenye nondo kali kama wewe mtandao wetu, Jamiiforums umekuwa kimbilio kwa wengi kupata habari sahihi zenye kila aina ya vithibitisho.
 
J shonza hand writing, hongera naona kwa sasa una ulinzi kama DAB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…