Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Kuua sio tu kutoa roho ya mwanadamu kwa sumu,SMG au hata kwa moto au njia yoyote ile inayoonekana.Kuua huanza na fikra za kutoona umuhimu wa nafsi ya mwenzio kuishi. Vitendo vya mauaji huwa ni kilele tu cha kile kilichoko nafsi mwa mtu. Aina yoyote ile ya kutoguswa na uzima Wa mwanadamu mwenzio ni mauaji na hakuna lugha nyingine mbele ya Mungu.

Maneno ya Ndugai Mara zote ni kiashiria kuwa anatumia macho mawili na sio matatu katika kuyaangalia mambo. Nadhani ameshasahau jinsi moyo unavyouma ikiwa mauti yanakunyemelea. Madhali bado yuko hai, iko siku atafahamu tena kuwa kumbe kunyodolea wengine panapohusika uhai sio jambo la kujaribu kabisa.
Jana na leo kuna kauli amezitoa sio kauli zinazofaa kutolewa na kiongozi wa muhimili, tena mbaya zaidi ni tambo za kujigamba, na kujiona yeye ndio alpha na omega kwa wanao mzunguka mle mjengoni.
 
Ndugai kawa kama mtoto mdogo. Wenzake wanasikitika yeye ndiyo kwanza anapambanana na wabunge wenzake. Ndiyo maana walimwachia futari. Hana roho nzuri. Katikamajonzi hayo unawezajekupambana na wenzako ambao unajua wana huzuni kubwa hivyo. Nakujigamba kuwa aliyelipia ndege ni waccm. So what? Sisi wengine hatuna vyama lakini tunavijana wetu wengine wako ccm wengine opposition. Je tuwatenganishe? Ingekuwa wewe umesaidia mbona ungejigamba sana?
Acha utoto. Fanya kazi yako. Hata Tulia anakushinda kwa hekima sasa. Yeye siku hizi katulia kweli.
 
Kuna watu humu nimeona nao wanachangia kwa upotoshaji,akiwemo mtu anaitwa Tume ya Katiba juu ya namna Lissu alivyotoka Tanzania kwenda Nairobi.

Kwanza naomba ku-declare kuwa nilishiriki "indirectly" kuona namna gani usafiri wa kwenda Nairobi unapatikana,japo nilikuwa mbali na nyumbani,lakini niliwasiliana na wadau ili kuona huyu mtu anapata usafiri kufika eneo la matibabu baada ya kusikia uhitaji mkubwa ni kufika Nairobi usiku uleule.

Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge ilikuwa ni kumleta Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link na si ya NHIF kama anavyosema huyo Ndugai,ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link),bahati mbaya ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.

Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.

Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.

Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Turky wa Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi

Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Arena),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu ya "height" ya ndege,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.

Sijaelewa huu upotoshaji wa huyu Ndugai ameutoa wapi,kwamba kuna ndege ilikodiwa toka Nairobi?Hiyo ndege ni ipi?kwamba aliomba itumie "airspace" ya Tanzania kinyume na sheria za nchi?Kwani sheria za nchi zinavunjwaje kwa ndege iliyoomba kibali kutua Tanzania na ikaruhusiwa?

Huu uwongo ni wa nini?hiyo ndege mliyokodi toka Kenya ni ipi?Maana kila mtu hata siyekuwa Dodoma aliona ndege iliyoondoka na Lissu ni 5H-ETG mali ya kampuni ya FlightLink.

Hii ni kampuni ya Tanzania,ndio maana usajili wa ndege umeanza na "5H",ndege zote zilizosajiliwa Tanzania huanza na "5H",zile za Kenya huanza na "5Y" na majirani Uganda ni "5X"...Wewe Ndugai hiyo ndege ya Kenya mliyoiombea kibali cha kutumia "airspace" yetu tena kinyume cha sheria ni ipi?Na sheria zipi mlizovunja?

Sasa unaona mtu anakuja humu anasema eti Lissu alitoka na ndege Dodoma hadi Dsm then ndio akaenda Nairobi.Huu uwongo mnauzalisha toka wapi??Wacheni upumbavu katika uhai na maisha ya watu sbb ya siasa!!Eboooo!!!!

Nimemsikiliza Ndugai hapa Jf kwenye video,ameongea kwa uchungu na huzuni,sababu maneno ya Lema yamemuingia sana,amefikia hatua ya kusema kama CHADEMA wanataka kumpeleka Lissu India,bunge lipo tayari endapo Waziri atakubali.Maneno ya Lema yamegusa mfupa,Job anajua aliondoka na hali gani hapa nyumbani kwenda India,amekaa miezi kibao akiugua.

Kila aliyekuwa anasimama bungeni,kabla ya kuchangia,alimuombea Spika afya njema na arudi mzima nyumbani.Watu walisali...Kuna siku Bulaya aliongoza sala ya kuomba afya ya spika katika Canteen ya Bunge.

Malumbano yanayoanzishwa na Spika ndani ya bunge juu ya afya ya Lissu si afya kwa ubinadamu na utu.Kuanzia lile la kutofautiana idadi ya risasi na Kubenea mpaka kamati ya maadili,na lile la kusema Turky ndio kachangia.Turky ni muislam safi,sadaka isiyo na mawaa na yenye dhawabu haitangazwi.

Palipo na tendo jema,Mungu hufungua riziki...Kuitangaza sadaka ya Turky bungeni ni kumuondolea neema na thawabu kubwakubwa na ndogondogo mja wake aliyetoa sadaka.Mh.Spika,tumia busara kufunga malumbano ya afya ya Lissu Bungeni,wakati upo India,watu walijibiidisha kukuombea na si kujadili na kulumbana juu ya afya yako na matibabu yako.FUNGA MJADALA WA KUSIMANGANA BUNGENI KUHUSU AFYA NA HALI YA TUNDU LISSU...HUU SI UBINADAMU.

Kuna kijana sijui ni msemaji wa chama naye katoka kabisa na "Press Release" kupongeza hali ya Mbunge Turky,kutoa "mali kauli" ya safari ya ndege.Jamani mnaharibu sadaka za wenzenu.Turky mwenyewe amenukuliwa akisema;
" Mbowe akaniomba kwa kuwa nafahamiana nao (wenye ndege) niwadhamini wamuwahishe Lissu halafu wao watalipa. Na ndicho nilichofanya (kuwadhamini kwa mali kauli) na pesa hiyo imelipwa jana. Tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake” .Watu mnaharibu sadaka za watu bila kujua,nia njema ya Turky ipo katika hayo maneno yake ya mwisho yenye "bold".

Msaidieni Lissu kama nyie mlivyosaidiwa kwa kofia za ubunge na uspika wenu,wacheni masimango,tendeni kama vile mlivyotendewa,wengine mlikwenda India miguu haingii hata katika viatu,mlivaa suti na sandozi.Mungu amewaponya...Lipeni wema juu ya wema!!Mnaleta "urasimu" wa taratibu za matibabu nje ya nchi kwa mwili wa binadamu ulipigwa na kulowa rasasi zaidi ya 10?Ebooo!!HIZO PESA ZA MAMA ZENU?

We Live Once,but Legacy Lives forever!!
View attachment 588456
Juu ni ndege ya kampuni ya FlightLink(Tanzania) iliyompeleka Lissu Nairobi

View attachment 588458
Hii ni ndege ya Safari Air Link iliyokusudiwa kumleta Dsm ikashindikana

Hongera Mkuu, umefunga propaganda za Polepole na Ndg Supika.
Tujikite kumuombe rafiki yetu Lissu, ili Mwenyezi Mungu amponye katika maumivu anayopitia.

James 5:15; JVC - And the prayer of faith shall save the sick, and the Lord shall raise him up; and if he have committed sins, they shall be forgiven him.
 
Tatizo kubwa ninaloliona nchi hii

Ukiwa mzalendo wewe ni adui wa nchi ..

Serikali ya ccm imeamua kupandikiza uchama

Kama nchi nyingine zilivyo na ukabila na sasa Tanzania inatafunwa na uchama uccm ..

Ukitoa hoja unabatizwa kuwa wewe in chama Fulani nani katufikisha uko bila shaka ni watu wasioipenda tanzania wanajipenda wao kwanza kuliko nchi yetu sasa nchi imekuwa na watu waoga wanungunikaji na wasomi wasio na faida wasioweza kuhoji mambo makubwa ya kitaifa ..

Hakika tumepatikana kama nchi kuletewa utawala wa hovyo hovyo unapenda taarifa za uongo kuliko uhalisia...

Lissu ugua pole pona uje uendelee kuwatoe tongotongo watanzania .
Dawa tuifute ccm maana ndo adui wa Tanzania umasikini, ujinga, maradhi wa ugaidi, malaria na UKIMWI.
 
Barafu.....dah as if nilikuwa katika fikra zangu kwa jinsi ulivyoingia ndani ya akili zangu, umeandika huku ukionesha ukweli wa nafsi nimeburudika na andiko lako.

Jumamosi hii ya tarehe 16/09/2017 jamani Watanzania wote wenye mapenzi mema tukamshukuru Mungu kwa kumponya Lissu kwa kuchangia damu katika hospitali, vituo vya afya na dispensari popote pale Tanzania bila ya maandamano .....Baragu nisaidie kuweka bandiko la hii hoja tafadhali...
 
Malumbano wanaoanzisha ni chadema wenyewe..wakijibiwa wanaona wanaonewa..ndugai alielezea taifa wingi wa risasi alizopigwa lisu kwenye gari..kubenea akasema ndugai muongo..wakati kitendo tu cha kutaja wingi kule wa risasi ilibidi mumpongeze..maana angeweza pia kukaa kimya..kamsema zito bungeni..zito akagusia lisu..wakati lisu hausiki..Lema nae anamshutumu kuhusu lissu..
Sasa vitu mnaanzisha wenyewe..mkijibiwa mnasema malumbano..basi kaeni kimya uguzeni mgonjwa wenu..ila msidhani shughuli zitasimama kwa sababu ya ugonjwa au kifo cha lisu..hata vikao vya Acacia na timu ya magufuli havijasimama
Inawauma hajafa. Halafu umetoka nje ya mada kabisa. Mtoa post ametoa kwa evidence, wewe unaropoka, kwa hiyo kama ndugu yako Ndugai kadanganya unataka asiambiwe.
 
Hiyo nondo imetulia kwa kweli,,,Mungu ndio atatenda haki,,,,Na Malipo ni hapa hapa duniani,,,Mnaofanya haya mambo kumbukeni nyie sio mawe, mtakuja pia ondoka hapa duniani,,,kwa nini ukusudie kumuondosha mwenzako mapema???
 
Bahati nzuri tu ni kwamba Mungu anajitofautisha na mwanadamu katika masafa ya kufikiri na kutenda. Mara zote yeye anaanzia sisi tunapoishia. Vinginevyo tungeweza kuongea mangine kabisa muda huu.Kwa jinsi watu walivyomuombea Ndugai kwa sauti na ukimya halafu baada ya kupona eti amerudia jeuri zake nina imani Mungu angekuwa mwanadamu angefuta uponyaji aliomufanyia.

Kuna watu wanadharau sana Facility ya kuungama dhambi kwa Mamlaka ya Kanisa lakini Yesu alipoweka nafasi yeye kama hiyo alijua mambo kama haya ya akina Ndugai.Ndugai yangetokea.Alijua akili kama za akina Ndugai zipo duniani. Huyu Ndugai angekuwa ni mtu anatambua na anao uelewa mpana juu ya Sakramenti ya Upatanisho lazima angeenda kuungama hiyo dhambi. Bahati mbaya sana dhambi zake "anaungamia" kwenye kiti chake cha uspika.

Ndugai, uzima ulevya na ugonjwa ulegeza. Huna madaraka ya kutambia wenzio isipokuwa kama usilingalipewa na huyo akaaye Juu. Usingalivaa mavazi ya Kifalme kama Spika kama Yeye aliye mwanzo na mwisho Wa Ufalme asingalikupatia ufalme huo.
A Theological Advice!!!Deep inside a Moral Theology
 
Back
Top Bottom