Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Kuna watu humu nimeona nao wanachangia kwa upotoshaji,akiwemo mtu anaitwa Tume ya Katiba juu ya namna Lissu alivyotoka Tanzania kwenda Nairobi.

Kwanza naomba ku-declare kuwa nilishiriki "indirectly" kuona namna gani usafiri wa kwenda Nairobi unapatikana,japo nilikuwa mbali na nyumbani,lakini niliwasiliana na wadau ili kuona huyu mtu anapata usafiri kufika eneo la matibabu baada ya kusikia uhitaji mkubwa ni kufika Nairobi usiku uleule.

Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge ilikuwa ni kumleta Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link na si ya NHIF kama anavyosema huyo Ndugai,ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link),bahati mbaya ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.

Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.

Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.

Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Turky wa Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi

Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Arena),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu ya "height" ya ndege,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.

Sijaelewa huu upotoshaji wa huyu Ndugai ameutoa wapi,kwamba kuna ndege ilikodiwa toka Nairobi?Hiyo ndege ni ipi?kwamba aliomba itumie "airspace" ya Tanzania kinyume na sheria za nchi?Kwani sheria za nchi zinavunjwaje kwa ndege iliyoomba kibali kutua Tanzania na ikaruhusiwa?

Huu uwongo ni wa nini?hiyo ndege mliyokodi toka Kenya ni ipi?Maana kila mtu hata siyekuwa Dodoma aliona ndege iliyoondoka na Lissu ni 5H-ETG mali ya kampuni ya FlightLink.

Hii ni kampuni ya Tanzania,ndio maana usajili wa ndege umeanza na "5H",ndege zote zilizosajiliwa Tanzania huanza na "5H",zile za Kenya huanza na "5Y" na majirani Uganda ni "5X"...Wewe Ndugai hiyo ndege ya Kenya mliyoiombea kibali cha kutumia "airspace" yetu tena kinyume cha sheria ni ipi?Na sheria zipi mlizovunja?

Sasa unaona mtu anakuja humu anasema eti Lissu alitoka na ndege Dodoma hadi Dsm then ndio akaenda Nairobi.Huu uwongo mnauzalisha toka wapi??Wacheni upumbavu katika uhai na maisha ya watu sbb ya siasa!!Eboooo!!!!

Nimemsikiliza Ndugai hapa Jf kwenye video,ameongea kwa uchungu na huzuni,sababu maneno ya Lema yamemuingia sana,amefikia hatua ya kusema kama CHADEMA wanataka kumpeleka Lissu India,bunge lipo tayari endapo Waziri atakubali.Maneno ya Lema yamegusa mfupa,Job anajua aliondoka na hali gani hapa nyumbani kwenda India,amekaa miezi kibao akiugua.

Kila aliyekuwa anasimama bungeni,kabla ya kuchangia,alimuombea Spika afya njema na arudi mzima nyumbani.Watu walisali...Kuna siku Bulaya aliongoza sala ya kuomba afya ya spika katika Canteen ya Bunge.

Malumbano yanayoanzishwa na Spika ndani ya bunge juu ya afya ya Lissu si afya kwa ubinadamu na utu.Kuanzia lile la kutofautiana idadi ya risasi na Kubenea mpaka kamati ya maadili,na lile la kusema Turky ndio kachangia.Turky ni muislam safi,sadaka isiyo na mawaa na yenye dhawabu haitangazwi.

Palipo na tendo jema,Mungu hufungua riziki...Kuitangaza sadaka ya Turky bungeni ni kumuondolea neema na thawabu kubwakubwa na ndogondogo mja wake aliyetoa sadaka.Mh.Spika,tumia busara kufunga malumbano ya afya ya Lissu Bungeni,wakati upo India,watu walijibiidisha kukuombea na si kujadili na kulumbana juu ya afya yako na matibabu yako.FUNGA MJADALA WA KUSIMANGANA BUNGENI KUHUSU AFYA NA HALI YA TUNDU LISSU...HUU SI UBINADAMU.

Kuna kijana sijui ni msemaji wa chama naye katoka kabisa na "Press Release" kupongeza hali ya Mbunge Turky,kutoa "mali kauli" ya safari ya ndege.Jamani mnaharibu sadaka za wenzenu.Turky mwenyewe amenukuliwa akisema;
" Mbowe akaniomba kwa kuwa nafahamiana nao (wenye ndege) niwadhamini wamuwahishe Lissu halafu wao watalipa. Na ndicho nilichofanya (kuwadhamini kwa mali kauli) na pesa hiyo imelipwa jana. Tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake” .Watu mnaharibu sadaka za watu bila kujua,nia njema ya Turky ipo katika hayo maneno yake ya mwisho yenye "bold".

Msaidieni Lissu kama nyie mlivyosaidiwa kwa kofia za ubunge na uspika wenu,wacheni masimango,tendeni kama vile mlivyotendewa,wengine mlikwenda India miguu haingii hata katika viatu,mlivaa suti na sandozi.Mungu amewaponya...Lipeni wema juu ya wema!!Mnaleta "urasimu" wa taratibu za matibabu nje ya nchi kwa mwili wa binadamu ulipigwa na kulowa rasasi zaidi ya 10?Ebooo!!HIZO PESA ZA MAMA ZENU?

We Live Once,but Legacy Lives forever!!
View attachment 588456
Juu ni ndege ya kampuni ya FlightLink(Tanzania) iliyompeleka Lissu Nairobi

View attachment 588458
Hii ni ndege ya Safari Air Link iliyokusudiwa kumleta Dsm ikashindikana
Ahsante sana mkuu kwa kuliweka hili vizuri.
 
Salary Slip nilikuona siku hile,poleni sana kwa kadhia hii,na namuombea rais wangu wa tls na mtani wangu maisha marefu!
Na wale waliohusika na uovu huu iwe kwa kutenda,kuwaza au kunena ile albadiri ya kesho iwatendee sawa sawa na yale waliyomtendea Lissu!
 
Kuua sio tu kutoa roho ya mwanadamu kwa sumu,SMG au hata kwa moto au njia yoyote ile inayoonekana.Kuua huanza na fikra za kutoona umuhimu wa nafsi ya mwenzio kuishi. Vitendo vya mauaji huwa ni kilele tu cha kile kilichoko nafsi mwa mtu. Aina yoyote ile ya kutoguswa na uzima Wa mwanadamu mwenzio ni mauaji na hakuna lugha nyingine mbele ya Mungu.

Maneno ya Ndugai Mara zote ni kiashiria kuwa anatumia macho mawili na sio matatu katika kuyaangalia mambo. Nadhani ameshasahau jinsi moyo unavyouma ikiwa mauti yanakunyemelea. Madhali bado yuko hai, iko siku atafahamu tena kuwa kumbe kunyodolea wengine panapohusika uhai sio jambo la kujaribu kabisa.
U remind me back!!30 yrs ago!!In a good class of Moral Theology!!I little cry for yr theological Concepts!!
 
Pia hakuna kitu kimeniuma sana kama nilivyosikia Ndugai alikuwa kwenye ile kamati ya bunge iliyokwenda nyamongo kisha kupindisha ukweli eti maji ya mto hayakuwa na sumu lakini wananchi walipowataka wabunge wa kamati ile waguse maji wabunge wote waligoma. Halafu leo hii Ndugai anasimama na kujifanya mzalendo eti anapigania raslimali za taifa huku akisahau Lissu ndio aliyekuwa akiwatetea wananchi wa nyamongo dhidi ya sumu ile kwenye mto. Halafu ukimsikia anavyozunguza kwa kejeli na ulevi wa madaraka huku akiwananga wapinzani kwamba ndio kipimo cha kutokuwa dhaifu. Yaani hajui hata udhaifu uko kwenye nini.
Duh! Haya mambo yanatokea Tanzania tu. Kwa kweli mchawi wetu alishakufa na mganga pia na mitishamba yao na uchawi, yaani tuna speed ya kujitoa ufahamu. Ccm adui mkubwa mno taifa hili.
 
Malumbano wanaoanzisha ni chadema wenyewe..wakijibiwa wanaona wanaonewa..ndugai alielezea taifa wingi wa risasi alizopigwa lisu kwenye gari..kubenea akasema ndugai muongo..wakati kitendo tu cha kutaja wingi kule wa risasi ilibidi mumpongeze..maana angeweza pia kukaa kimya..kamsema zito bungeni..zito akagusia lisu..wakati lisu hausiki..Lema nae anamshutumu kuhusu lissu..
Sasa vitu mnaanzisha wenyewe..mkijibiwa mnasema malumbano..basi kaeni kimya uguzeni mgonjwa wenu..ila msidhani shughuli zitasimama kwa sababu ya ugonjwa au kifo cha lisu..hata vikao vya Acacia na timu ya magufuli havijasimama
Wewe Jisambaa la wapi unatia aibu hivyo?
 
Asante Barafu! Naweza kusema bila hofu kwamba kwa sasa Taifa linaendeshwa kishetani zaidi! Ni aibu kubwa kuwa na Viongozi aina ya Ndugai!
Ndugai alipewa amri hadharani ya kuwashughulikia wapinzani, haikuchukua muda wabunge waliochaguliwa na Wananchi kwa kura halali wakafukuzwa! Kibaya zaidi akapigiwa simu za pongezi kutoka kwa waliomtuma! Kichwa kikapanuka! Leo anatamba na kutetea kasoro ya serikali na Bunge kutomsaidia Lissu!
Esther Bulaya aliyeongoza maombi kwa Afya ya Spika hayupo Bungeni leo, kashughulikiwa na Spika aliyemuombea kwa Mungu! Naamini shetani anamkejeli Mungu wetu kwa kumponya kiumbe huyu!
Wenzetu huomba uongozi kulitumikia Taifa, lkn kuna wengine wapo kwenye uongozi kutumikia kikundi cha watu!
Ipo siku Taifa hili la Nyerere litapata Uhuru wake kamili! Siku zinahesabika!
Mwenyezi Mungu hajawahi kushindwa na viumbe dhaifu!
 
Malumbano wanaoanzisha ni chadema wenyewe..wakijibiwa wanaona wanaonewa..ndugai alielezea taifa wingi wa risasi alizopigwa lisu kwenye gari..kubenea akasema ndugai muongo..wakati kitendo tu cha kutaja wingi kule wa risasi ilibidi mumpongeze..maana angeweza pia kukaa kimya..kamsema zito bungeni..zito akagusia lisu..wakati lisu hausiki..Lema nae anamshutumu kuhusu lissu..
Sasa vitu mnaanzisha wenyewe..mkijibiwa mnasema malumbano..basi kaeni kimya uguzeni mgonjwa wenu..ila msidhani shughuli zitasimama kwa sababu ya ugonjwa au kifo cha lisu..hata vikao vya Acacia na timu ya magufuli havijasimama
Why all these hate comments?!!
 
Asante sana barafu, kwa post hii umelitendea haki hili jamvi letu pendwa la JF. Ni muda mrefu nimejiuliza ni wapi ilipoenda JF yetu ile ya miaka ilee hadi nikajikuta na mimi naingia kwenye mipasho ya ajabu ajabu na kuanza kukimbizana na vichaa nikisahau wanaotusoma watashindwa kuona tofauti. Hii post yako imenizindua, imeniamsha lakini zaidi ya yote imenipa faraja...hongera sana.

Ninachoomba ni kitu kimoja, turuhusu tuisambaze huu mchango wako uwafikie wengi wakati huu tunapomuombea Mh. Tundu Lissu apone haraka. Tunaomba Mungu amnusuru kutoka mikononi mwa watesi wake wanaotamba mitaani kama vile Tanzania imetekwa na kuwa ngome yake shetani. Turuhusu tuitafsiri na kuisambaza hii ripoti yako ili raia wema wajue kinachoendelea.

Mungu akubariki sana barafu
 
Back
Top Bottom