Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Barafu, Mungu awabariki nyote ambao mlitoa michango ya namna mbalimbali kumfanya mpendwa wetu Lisu aweze kupata matibabu. Hatuna maneno mazuri ya kusema. Hamkutenda kwaajili ya Lisu bali kwaajili yetu sote tuliopatwa na simanzi kubwa katika tukio hili.

Mungu wetu tunaomba usikie maombi yetu, ni maombi yetu sisi wenye huzuni, siyo maombi ya Tundu Lisu. Kama ulimfufua Lazaro, kama uliwaponya viwete, vipofu na wengine wengi, kwa nini isiwezekane kwa Lisu? Tunajua katika wewe Mungu wetu hakuna usiloliweza, ukitaka, mpendwa wetu anaweza kusimama wakati wowote.

Wewe ulisema, 'Ombeni mtapewa', tunajua wewe ni mwaminifu katika ahadi zako. Tunaomba kwaajili ya uhai na afya ya Mpendwa wetu Tundu Lisu.

Tena ulisema, 'Tafuteni mtapata', tunakutafuta wewe uliye asili ya yote, umjalie uzima na afya ndugu yetu Tundu Lisu, aliyepo kitandani, si kwa mapenzi yako bali kwa mapenzi ya ibilisi.

Bwana wetu ulituambia, 'gongeni mtafunguliwa', tunagonga kwenye nyumba ya mamlaka yako ili mkono wako wenye nguvu ukamguse na kumnyanyua ndugu yetu Tundu Lisu.

Ni mapenzi yetu, ndugu yetu arejee katika hali yake lakini kwa mapenzi yako katika haya mateso anayoyapitia, unaweza kumvusha, hata akatoka akawa bora zaidi kama ilivyokuwa kwa Ayubu. Mapenzi yako yatimizwe, sasa na hata milele.

Sent using Jamii Forums mobile app

Very powerful prayers....

May God, The Almighty in Jesus Christ of Nazareth, bless you now and forever....

Amen!!
 
Ahsante barafu kwa taarifa iliyonyooka Mungu amsaidie sana apone arudi kuja kutetea wanyonge ,Ndugai dhambi anayoibeba ni kubwa mno hivi kwa jinsi anavyofanya tutakosea tukisema alikuwa ni mshirika wa mpango wa mauaji
 
Sina cha kusema zaidi ya bravo Barafu, you are fantastic. Andiko ni fact tupu ila umelifikisha kwa emotions kama tulikuwepo. Daima huwa unaandika vizuri ila hili moja kati ya maandiko yako bora kabisa.

Ni maskitiko sana kwa nchi saa hii ni kama kila mtu amefungia kichwa chake store watu tunatembea na kuwaza kwa viwili wili tu
 
Malumbano wanaoanzisha ni chadema wenyewe..wakijibiwa wanaona wanaonewa..ndugai alielezea taifa wingi wa risasi alizopigwa lisu kwenye gari..kubenea akasema ndugai muongo..wakati kitendo tu cha kutaja wingi kule wa risasi ilibidi mumpongeze..maana angeweza pia kukaa kimya..kamsema zito bungeni..zito akagusia lisu..wakati lisu hausiki..Lema nae anamshutumu kuhusu lissu..
Sasa vitu mnaanzisha wenyewe..mkijibiwa mnasema malumbano..basi kaeni kimya uguzeni mgonjwa wenu..ila msidhani shughuli zitasimama kwa sababu ya ugonjwa au kifo cha lisu..hata vikao vya Acacia na timu ya magufuli havijasimama
Ww na family yako muunganishwe kwenye albadir ya kesho!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malumbano wanaoanzisha ni chadema wenyewe..wakijibiwa wanaona wanaonewa..ndugai alielezea taifa wingi wa risasi alizopigwa lisu kwenye gari..kubenea akasema ndugai muongo..wakati kitendo tu cha kutaja wingi kule wa risasi ilibidi mumpongeze..maana angeweza pia kukaa kimya..kamsema zito bungeni..zito akagusia lisu..wakati lisu hausiki..Lema nae anamshutumu kuhusu lissu..
Sasa vitu mnaanzisha wenyewe..mkijibiwa mnasema malumbano..basi kaeni kimya uguzeni mgonjwa wenu..ila msidhani shughuli zitasimama kwa sababu ya ugonjwa au kifo cha lisu..hata vikao vya Acacia na timu ya magufuli havijasimama
Kifo cha lissu!?? Kwamba mnadhani mtampata tena!?

Pilato 007
 
Kumbe ile "patasi" ilienda India ikiwa imevaa suti na malapa, alafu leo inakuja na kibesi eti ipo smart, watu wasimchezee. shwaini wahed kabisa.

Kuua sio tu kutoa roho ya mwanadamu kwa sumu,SMG au hata kwa moto au njia yoyote ile inayoonekana.Kuua huanza na fikra za kutoona umuhimu wa nafsi ya mwenzio kuishi. Vitendo vya mauaji huwa ni kilele tu cha kile kilichoko nafsi mwa mtu. Aina yoyote ile ya kutoguswa na uzima Wa mwanadamu mwenzio ni mauaji na hakuna lugha nyingine mbele ya Mungu.

Maneno ya Ndugai Mara zote ni kiashiria kuwa anatumia macho mawili na sio matatu katika kuyaangalia mambo. Nadhani ameshasahau jinsi moyo unavyouma ikiwa mauti yanakunyemelea. Madhali bado yuko hai, iko siku atafahamu tena kuwa kumbe kunyodolea wengine panapohusika uhai sio jambo la kujaribu kabisa.
 
Kaka MUNGU akubariki sana kwa somo zuri la hekima ulotoa. Kweli kabisa viongozi wetu walipaswa kabisa kuangalia namna ya kusaidia mgonjwa na ndugu wanaouguza mgonjwa. Sisi sote tunajua ni jinsi gani familia ya mheshimiwa Lissu inavyopitia kipindi kigumu ila tumejitoa ufahamu tumefanya jambo hili kuwa la kisiasa tukishindana kwa kejeli kama walevi.
Asante kaka mkubwa hakika MUNGU Amekujalia hekima kubwa na busara za ajabu.

Hakika bandiko lako limenifanya nitokwe na machozi
 
Back
Top Bottom