MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Lauryn Hill
Huyu ni moja kati ya binadamu wenye vipaji vikubwa sana vya utunzi wa mashairi na sauti ya kipekee kabisa. Anaweza kuimba muziki wa aina mbalimbali, kuanzia Soul, Blues, Jazz, Reggae, RnB na Hip-Hip.
Lakini kuna video inaonyesha akiwa mtoto wa miaka 13 akiimba wimbo wa Who's Lovin You wa The Jackson 5 akiwa anatetemeka na watu kumzomea (It's Heart Breaking), inashangaza kuona watu wakimbeza mtoto ambaye miaka michache baadaye alikuja kuwa mwanamuziki mkubwa sana duniani.
Somo: Usipuuze mtu, Usimchukulie mtu powa na Usikate Tamaa, Like Al Pacino said "Every dog has it's day"