Safari ya miaka 9 tangu kuacha kazi. Hamasa kwa vijana wenye maono makubwa

Yaah Kikubwa ameachana na dhiki kuu hayoo mengine sijui kuwa km bakheresa na mo ni reference tu sidhani km anamaanisha kweli..!
 
Kwanza binafsi naweza sema mpaka hapa umefanikiwa pakubwa sana

Muanzilishi wa Ali baba jackma ambaye huwa napenda sana kusoma quote zake instagram anasema,ukitaka kujifunza mambo kwa watu basi jifunze kupitia magumu waliyopitia,na hii ni kweli kabisa shida ndio zinazo tufanya tukue,,wewe hapo mwandishi umejifunza mengi katika harakati zako hivyo kwa kila anguko ambalo umepitia umejifunza kitu

Iko hivi watu wengi ambao walifanikiwa walifeli sana katika harakati zao lkn mwisho wa siku walikuja kufanikiwa,,,michael jordan alikataliwa na timu yake akiwa shuleni,,na alikosa mitupo ya kikapu karibia 9,000 lkn kila mtu ukimtaja michael jordan unajua alikiwa nguli wa basketball

Kuna bwana mmoja nimemsahau jina lake alikuwa mwandishi wa kitabu cha Harry potter,kitabu chake kilikataliwa kuchapishwa mara kumi na mbili [12] lkn baadae kikaja kuzalisha filamu za harry potter

Tunaweza kutaja list ndefu hapa,,kifupi wewe ushapitia njia ya kufeli sana trust me endelea kupambana ipo siku utakuja kukumbuka maneno yangu

Nimependa spirit yako ya mafanikio,,mcheza sinema maarufu na aloyewahi kuwa gavana wa California Shwaziniga, anyways nimeandika jina lake kiswahili kwakuwa spelling za jina lake zina mbwembwe sana,aliwahi sema,alitaka kuwa mtunasha misuli bingwa duniani pamoja na kuwa katika fani ya burudani,na alisema hakuwa na plan b,aliamini atakuwa vile anavyotaka kuwa,na kweli alikuwa body builder wa dunia na mkali wa sinema kama terminator,command john na movies nyingine nyingi tu,,aliamini katika ndoto zake,hata wewe pia utaweza.

Mwisho kupitia story yako kuna mambo tumejifunza ambayo yatasaidia wengine ima wasirudie makosa uliyofanya au kuwa na adhma ya kuwa na moyo wa kijasiri na kutokata tamaa kama wewe.

Asante
 
Seen.
 
Asante sana mkuu kwa kunielewa na kuelewa lengo la uzi huu.
N
 
Shukrani sana kiongozi kwa kunitia moyo. Hii imenipa faraja sana. Barikiwa mnoo
 
Ndugu zangu mwaka 2016 kama Mungu atapenda niwe hai nitakuwa na miaka 38.
2016 utakua na Miaka 38? Nimesoma Andiko lako lote lakini nilichogundua unafanya yote hayo kwa ajili ya mtu fulani ukiangazia maumivu ya kuachwa na mkeo wa Pili aliekuzalia mtoto wako wa kike lakini utakuja kuvunjika moyo huyo mtu atakapokuja kukwambia yote uliyoyafanya kwa ajili yake ni km ujinga au upumbavu na hapo ndipo utakapo umia zaidi maana atakua km ameupasua na kuuraruararua kabisa moyo wako bila huruma na kujiuliza hata huyu nimefanya yote haya kwa ajili yake but still haoni chochote nilichokifanya kwa ajili yake?

Sikiliza, umesema mtoto wako wa kike yupo kwa Mama yake na Wewe una Mwanamke mwingine na huyo mkeo wa Pili huko alipo ana Mwanaume mwingine anaemridhisha sasa Wewe umeegemea kwa mwanao wa kike kusema kila ninachokifanya ni cha yule mtoto wangu wa kike sababu Wewe umeoa huyo cheupe Ila moyo wako haupo kwa huyo cheupe moyo pamoja na kwamba unamsifia anapambana n so on

Wewe moyo wako upo kwa Mwanamke aliekuzalia mtoto wako wa kike na una andaa safina ya kutaka kurudi kule kwenda kuonyesha kwamba sasa nimefanikiwa rudisha moyo kwangu njoo unipende.

Mimi ni Mwanaume na nakwambia kiume zaidi, huyo cheupe zaa nae watoto alafu focus na hao Watoto wa huyo cheupe ili kuuondoa moyo wako kule umefungwa kwa yule mtoto wa kike uliezaa na Mwanamke wako wa Pili, ukishazaa na huyo cheupe focus na hao Watoto wako wa Ndoa hii ya sasa usifocus kule yule sio mke wako tena hata uwe zaidi ya MO au Bakhresa hatokurudia kamwe yeye ataendelea kukuona km takataka tu km alivyokuona Mwanzo usifanye vitu kuridhisha watu ukifikiri kwamba ukiwa na mapesa mengi basi atarudi my bro unajidanganya

Wewe ulichobahatisha ni kitu kimoja tu na hii nakupa km Siri Mungu amekupa km zawadi na hio zawadi ukiichezea haitorudi tena kwako itaenda mazima sasa ni kwako Wewe kuamua kuipoteza au kuendelea kuishi nayo Mungu amekutoa kwenye tanuru la Moto alipokupitisha kwa Miaka mingi na Mafanikio yako sio ya kwako peke yako ni ya hao watu wanaokuzunguka ukianza na huyo cheupe wako na huyo mpwa wako mtoto wa Dada yako km unavyosimulia kua bila hao Wewe asingekua hapo na hio ndio milango yako ya kutokea milango yako ya Mafanikio ilipo

Sasa nitakachokufungua macho katika hao wawili mmoja au wote kwa pamoja ndio wanaokuangazia Maisha yako wanakufanya ufanikiwe aidha kwa kukushauri vizuri na kukupa ABC zote za kukuonyesha geti lako la Mafanikio lipo wapo na utumie funguo ipi ili uweze kulifungua na kufika mbali Ila Wewe umewekewa mtego mmoja tu na mtego wenyewe ni wa kijinga sana ambao ukienda fyongo ukanasa utaenda kuporomoka vibaya sana

Nitakuuliza swali katika Mafanikio yako hayo yule mkeo wa Pili amechangia nini? Kuna chochote amechangia mpaka umefanikiwa? Mpaka umefika hapo ulipo sasa amekuchangia nini? Km Jibu lako ni hakuna kaa nae mbali sana sasa km ulikua hauelewi ngoja nikutoe tongotongo mtego uliowekewa ni kurudi kule kwa mkeo wa Pili kwa kigezo kwamba unaenda kwa Mtoto wako wa kike kumbe lengo ni kumrudisha Mama yake arudiane nawe na kuanza kupadharau huku palipokunyanyua utapoteza kila kitu

Story yako nikiifanyia summary kwa ufupi tu inaonekana Wewe una maumivu makali sana moyoni ya kuachwa na mke wa Pili ambae umezaa nae mtoto wa kike alafu akakukimbia na sio mke wa kwanza na sio kupoteza mtoto wako wa kwanza na pia huyu mke wa sasa umeoa sio kwamba unampenda sana hapana umeoa sababu huna wa kukusaidia utafanyaje sasa na huyo Mwanamke ameolewa na Wewe sababu ya kukusaidia kukuondoa kwenye hali yako unayoipitia

Sasa umepata anaekusaidia unataka kurudi kwa ambae hakukusaidia chochote na hapo ndipo wengi wanapofeli hapo ndipo wengi mnapoharibu, Wanawake ni Baraka (huyo mkeo cheupe ni Baraka na Zawadi kwako) hio ni zawadi kutoka kwa Mungu na Wanawake ni laana (mkeo wa Pili aliekukimbia sababu huna kitu ni laana khum) usirudi kule kujihusisha nae sijui mtoto wangu wa kike na upumbavu mwingine km huo utapukutika ubakie km 1

Wewe unakuaje mjinga unakumbatia laana iliyoamua ikuache Wewe unaifuata tena? Una Akili Wewe? Utanisamehe kwa my deep critical thinking lakini ingia ndani zaidi Waza na kufikiria zaidi Waza kuhusu watoto utakao zaa na huyo cheupe huyo ndio MTO wa Baraka zaa nae huyo watoto wako na huyo cheupe ndio uwarithishe hizo kazi zako usije ukacheza fyongo Mjomba utajuta na kusagwa Meno, hao walio na Wewe ndio Baraka yako wale waliojiondoa kwako na kwenda ukiwa huna chochote ni laana na mikosi na nuksi ukiifuata utapukutika na usibakie na Jani hata 1 mwisho utakufa ukiwa huna kitu chochote, maneno yangu sio Sheria maneno yangu unaweza ukayaona hayana maana leo Ila kuna siku utarudi hapa kuyasoma upya na kusema nilikwambia

Stick na hao walio na Wewe uondoe moyo wako kule yule hayupo na Wewe tena ameesha enda ameenda haupo tena Moyoni mwake wala hakuwazii na chochote na Wewe umeshaoa tayari unataka kurudi kule na kuonyesha umwamba kwamba sasa umetajirika ulikimbiwa wakati huna kitu ili arudi tena kwako hio haisaidii kitu sana sana unairudia laana Ile Ile na kukaribisha mikosi Ile Ile iliyokukimbia tu na haina time na Wewe utapukutishwa
 
Kujiajiri kusikie tu,kunahitaji moyo kweli..halafu familia nyingi hazipendi kabisa vijana wao wajiajiri ukiwatoa wachaga,wakinga na watu wa arusha huwa wanatoana sana na kusapotiana,ila sisi jamii zingine balaa tupu.
Ajira ni ngumu,unaenda sehemu kuomba kazi ambayo sifa yake uwe umesoma ngazi ya cheti au diploma unakuta na watu wa digrii nao wanaomba hukohuko,tena mtu wa digrii anasema wazi kuwa yupo tayari kuchukua mshahara wa ngazi ya cheti au dip.
 
Wengine wapo tayari kujitolea.....
 
Kiufipi mleta mada katupa somo tusiache kazi kwa kukurupuka. Kama Covid 19 walikubali kusaliti chama ili waingie mjengoni ww ni nani.? Mtu unajijua umetokea familia ya kimaskini unapangwa kazi Songea ndani ndani unaanza nyodo. Hilo ndio tulilojifunza hapa. Tanzania ya sasa imefunguka kila mkoa umeungwa kwa lami. Serikali imeruhusu mabasi yatembee masaa 24 ww unapelekwa sehem unaleta nyodo. Kuacha kazi lazma uwe na backup plan mzee. Ujue kunawatu wakukushika ukianguka. Ukiwa kwenye mfumo inakusaidia usidokoe vihela kwenye biashara.
 
Hongera Kwa kuutambua uhalisia wako. Kwa vile umekutana na maisha halisi na mwanamke halisi.

By the way bongo hakuna Ajira ila kuna utumwa na vibarua. Hao wanao beza ni uoga tu wao walitaka uwe na maendeleo ambayo wamelenga majumuisho ya mshahara wa miaka 9. Wakisahau kuwa kuna elimu ya ujasiriamali na biashara Kwa ujamla ambayo umeipata na enaenda vizazi na vizazi Nina mifano halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…