Revocatus Mweyunge
New Member
- Aug 1, 2022
- 2
- 2
Utangulizi
Elimu ni ufunguo wa Maisha ni neno ambalo limekua likizungumzwa sana katika jamii yetu. Neno hili limekuwa likitumika kuhamasisha wanafunzi kupenda shule na kuongeza juhudi zaidi katika masomo yao.
Wazazi wengi wamekua wakiamini na kuwaaminisha watoto wao kuwa bila ya kuwa na elimu unakua na wigo mdogo wa kupata mafanikio katika Maisha. Jambo hili kwa namna moja au nyingine linahakisi uhalisia katika jamii yetu na duniani kwa ujumla. Changamoto iliyopo ni jinsi gani kila moja anavyofahamu elimu na ni kwa jinsi gani anaweza kutoa maana halisi ya elimu.
Elimu ni ujuzi alionao mtu juu ya jambo fulani, na kwa kutumia ujuzi huu mtu anaweza kutatua changamoto mbalimbali katika jamii inayomzunguka.
Elimu inaweza kugawanywa katika mifumo tofauti kama vile elimu inayofuata mfumo rasmi yaani ile inayofuaata mtaala maalumu na ile isiyofuata mtaala maalumu ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo inakusanya kundi kubwa la watu kwani hata wanafunzi wenye kufuata mfumo rasmi nao kwa namna fulani wanapata elimu hii kwa njia mbalimbali, kwa kujua ama kwa kutokujua. Elimu hii umsadia mtu kujifunza ujuzi fulani ama kwa kuambiwa, au kuona na kufanya kwa vitendo.
Makuzi ya Mtoto
Mtoto anapokuwa katika elimu ya msingi ndipo sehemu anatakiwa kutazamwa sana kwani ndio wakati ambapo anajifunza vitu vingi, hivyo ndio wakati mzazi anatakiwa kugundua talanta / kipaji cha mtoto wake kutokana na vile vitu anavyovipenda kufanya. Hii itamjengea mtoto wepesi wa kuelewa mambo na kufanya vyema katika masomo yake kwani atakuwa anafanya mambo kwa kufurahia.
Pamoja na majukumu tulionayo, wazazi tunatakiwa kuwa karibu sana na watoto wetu ili kuwasadia katika safari yao ya kuitafuta elimu, kwani mtoto anaanza kujifunza nyumbani na tukifanya hivyo tutarahisisha kazi ya mwalimu shuleni.
Ndoto
Kila mmoja ana kitu anachokiamini, ndoto anayotamani kutimiza, matamanio ya unavyotaka kuwa ama unavyotaka kuishi kipindi cha uhai wako.
Ndoto ni maono, taswira ama matamanio ya mtu juu ya jambo fulani, ni hali anayokuwa nayo mtu inayomfanya kila mara awe na tamaa ya kuifkia. Ndoto zinaweza kuwa zakufanana au kutofautiana, ila hata zikiwa zinafanana kila mmoja atatumia njia yake kutimiza ndoto yake “kila mtu ni wa pekee”. Ndoto bila ya malengo itabaki kuwa ndoto kila siku, kwani bila ya kuwa na mwendelezo katika kuikamilisha kamwe haitotimia.
Changamoto inayosababisha wengi kutokufikia ndoto zao ni pamoja na mwanafunzi kutokuwa na mpango dhabiti wa kufikia ndoto zake, kukata tamaa kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri katika masomo yake, na wengine kukatishwa tamaa kutoka jamii inayowazunguka kwa kuwaambia kuwa hiyo taaluma anayofanya haina maslai ya kifedha ama kwa kuwaambia kuwa hiyo ndoto awezi kufikia kwa kuwa wao waliishindwa , hivyo kumsababisha mwanafunzi kufanya kile wazazi wanacho kiitaji ama kusikiliza jamii inasema nini.
Wazazi wanawajibu mkubwa wa kuwasaidia watoto wao kutimiza za zao na sio mtoto kutimiza ndoto za mzazi, unapomchagulia mtoto fani ya kusoma ni kama unataka atimize ndoto yako, sijasema kuwa mzazi usimshauri mtoto ila ni vyema umshauri mtoto kutokana na kile anachokifikiria kukifanya na sio kumpangia cha kufanya.
Matarajio ya Mwanafunzi
Mwanafanzi anapohitimu masomo yake ya chuo kikuu anakuwa na mategemeo makubwa ya kupata ajira inayohusiana na ujuzi alioupata kipindi alipokuwa chuoni, hali hii husababisha wanafunzi wengi wanaohitimu elimu ya chuo kikuu kuwa na ugha mdogo katika uwezo wao wa kufikiri, kwani wanafunzi wengi huwa wanaanza kutafuta ajira sehemu mbalimbali na wanatumia muda mwingi kuhudhuria kwenye usaili na hivyo kupelekea kuwa na matumizi makubwa ya rasilimali muda na fedha bila kujua hali hiyo ni sawa na kucheza michezo ya kubahatisha. Ili kukabiliana na hali hii inatupasa kuangalia tena mitaala ya elimu yetu ili itusaidie kuaandaa vijana wenye uwezo wa kujiajiri kabla hatujawaza watapataje mitaji. Tupunguze muda wa kusoma kwa nadharia na tuongeze muda wa vitendo zaidi. Vyuo vingi mwanafunzi anasoma mambo mengi sana ambayo wala hata hayatumii katika maisha yake hii inapelekea kuwa na wahitimu wengi wenye ujuzi wa kudonoa donoa katika nyanja zaidi ya moja na kufanya elimu yetu isiwe na tija katika jamii yetu.
Kujikita kwenye fani moja kwa muda mrefu
Tumekuwa na kasumba katika soko la ajila mwajili kutaka mtu mwenye fani zaidi ya moja ili kupunguza idadi ya watu watakao waajili, hali imesababisha hata walimu na wahadhiri vyuoni kuhimiza watu kujifunza fani zaidi ya moja wawapo masomoni. Japo ni kweli Mungu ametupa uwezo mkubwa binadamu lakini wahenga walisema kuwa mshika mawili moja umponyoka, mimi naamini endapo mwanafunzi atakapojikita katika fani moja kwa muda mrefu itamsaidia kuwa mahiri katika fani hiyo na pia atakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuona changamoto zinazohusu fani hiyo katika jamii na kuzitatua hivyo elimu yake ikawa na tija.
Mfano wanafunzi wanaosoma masomo ya TEHAMA, wanasoma mambo mengi wanapofika chuo kikuu, unaweza ukakuta mwanafunzi anasoma sayansi ya komputa lakini katika kipindi chake cha masomo anaandaliwa kuwa msimamizi wa kanzi data (Data Administrator), msimamizi wa mifumo, mlinzi wa mifumo na fani nyingine nyingi. Mwanafunzi asipokuwa makini anaweza akajikuta fani hizi zote anauwelewa wa juu juu tu, lakini kama angechagua eneo moja mfano usimamizi wa kanzi data pekee angekua mahili na angeweza kuitumia fani hiyo vizuri na kusaidia jamii na taifa kwa ujumla.
Utaratibu wa kupima utendaji wa mwalimu / mhadhili
Utaratibu uliopo wa kupima utendaji kazi wa walimu ni kwa kuangalia kama ametimiza idadi ya vipindi alivyotakiwa kufundisha ama amemaliza mtaala mwa mwaka husika au muhula husika. Hii changamoto inasababisha wakufunzi (walimu/ wahadhiri) wetu kujikita zaidi kumaliza mtaala ili kuendana na muda aliopewa, hii inasababisha mkufunzi kutokujali mazao anayoyatengeneza na kupelekea kuwa na kikazi chenye uwezo mkubwa wa kukalili na kukosa uwezo wa kuchanganua mambo kwasababu wakufunzi wanatumia muda mchache ili kukimbizana na mtaala.
Hitimisho

- Tunatakiwa kuangalia upya mitaala yetu ya elimu ili kutengeneza kizazi ambacho kinaweza kutumia elimu walionayo kutatua changamoto zilizopo katika jamii yetu.
- Wazazi wawe kitalu cha kwanza cha kutengeneza kizazi kilicho bora kwa kutambua vipaji vya watoto na kuwawezesha watoto kutimiza ndoto zao.
- Wahadhiri wa vyuo vikuu wakubali kuwa walezi wa wanafunzi kwa kuwaelekeza njia sahihi ili kuwasaidia wanafunzi kwenda kwenye mwelekeo uliosahihi na kushiriki nao kwa karibu kwa yale mawazo wanayowashirikisha.
# wanaokudharau siku moja wataendelea kukudharau usipo badilika.
Upvote
3