Safari ya Rais Magufuli kwa barabara yawatumbua mameneja wa TANROADS Lindi na Pwani

Safari ya Rais Magufuli kwa barabara yawatumbua mameneja wa TANROADS Lindi na Pwani

Sababu ya kuwa na ulazima wa waziri kuwa mbunge ni moja tuu; ili waweze kuingia Bungeni kujibu hoja na maswali ya waheshimiwa wabunge..Na kama sio mbunge huruhusiwi kukanyaga floor ya Bunge..ndio maana ata AG ni mbunge pia. Mawaziri wa SASA wanaendelea kuwa wasaidizi wa Rais mpaka pale utakapofanyika uteuzi mwingine manake serikali iko active muda wote na haivunjwi kama Bunge.
AG sio mbunge mkuu ila ni sehemu ya bunge. Issue ya kusema lazima waziri awe mbunge ili apate kuingia bungeni sioni mashiko yake, inaweza kutungwa sheria ya waziri kuingia bungeni hata kama si mbunge kama anavyoingia huyo AG au rais.

Rasimu ya Warioba ilipendekeza waziri awe ni muajiriwa na hii kwa maoni yangu ilikuwa jambo jema sana na ingeondoa hizo sintofahamu zote.
 
Tumbua tu Kamwelwe ila nakuhakikishia siku yako nawe itafika.
 
Sio kweli lazima ukubali kuna uzembe wa watendaji haiwezekani barabara inaharibika kiwango kile na wewe upo tu unaamka asubuhi unamuaga mkeo/mumeo unaenda kazini wakati huendi kufanya chochote halafu mnakuja na kisingizio cha kukosa pesa[emoji53]

Tupunguze kufanya kazi kwa mazoea (Business as usual)
Mkuu kama unatembea tembea maeneo mbalimbali utagundua kuna shida somewhere. Pita barabara ya Iringa to Dom via Mtera uone, Shelui to Nzega na kisha Nyasamba hadi Misungwi utajionea kuelekea Mwanza.

Miundombinu ya barabara ipo hoi maeneo mengi ila serikali inachojua ni kuweka tochi nyingi ili kukusanya mapato kwa kigezo cha kudhibiti ajali wakati miundombinu mibovu inachangia ajali kwa kiasi kikubwa sana.
 
Hizi ni siasa za awamu ya tano, pesa za miradi hazitolewi ila hujikosha kwa kuwaonea wadogo. Wa kutumbuliwa ni baba mwenye nyumba
Nao si waseme mbona hutupi pesa barabara zinakarabatiwa na nn,wapo kimya ss tunajua pesa wanapewa Kama ni waoga kusema inakula kwao.
 
Waziri wa ujenzi mh Kamwele amewaondoa madarakani mameneja wa Tanroads wa mikoa ya Lindi na Pwani kufuatia kushindwa kuifanyia matengenezo barabara ya Dar hadi Mtwara.

Maamuzi hayo ya mh Kamwelwe yanafuatia maagizo yaliyotolewa jana na Rais Magufuli ya kutaka hatua zichukuliwe kutikana na ubovu wa barabara alioushuhudia kwenye takribani zaidi ya km 90 .

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Aisee toa huo upuuzi wako "MAENDELEO HAYANA VYAMA"
Kamuulize Bwege ndio atakuambia yana vyama au hayana

Kwa kifupi it is official, maendeleo yana vyama ndio maana majimbo yote yanayoongozwa na ccm pato lao ni dollar 3,000 na kule kunakoongozwa na upinzani wanaishi chini ya dollar na umasikini wa kutupwa
 
WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Issac Kamwelwe ametengua uteuzi wa meneja wawili wa Wakala wa Barabara (Tanroas) wa Mikoa ya Lindi na Pwani kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ya kusimamia miundo mbinu ya barabara kwenye maeneo yao.

Uamuzi huo wa Waziri Kamwelwe umefanyika ikiwa ni siku moja tangu Rais John Magufuli alipopita kwenye barabra za mikoa hiyo akitoka mkoani Mtwara kuhudhuria maziko ya Rais mtaaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na kukerwa na uharibifu mkubwa wa barabara za mikoa hiyo.

Kamwelwe alichukua uamuzi huo jana alipokuwa akikagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye kilometa 1.6 inayotoka Kibaoni kwenda Makao Makuu ya Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoani Katavi.

Alikuwa njiani kutoka Mji Mdogo wa Inyonga uliopo wilayani Mlele kwenda mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Waziri Kamwelwe, mameneja aliotengua uteuzi wao ni Issac Mwanawima, Meneja wa Lindi na Yudas Msangi aliyekuwa Kaimu Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Pwani.

Waziri Kamwelwe alisema Rais Maguguli alipita juzi kwenye barabara hizo na kushuhudia lami ikiwa imeharibika na barabara imekuwa kama ya vumbi wakati zipo fedha za matengenezo kupitia Mfuko wa Barabara zipo.

Alisema Tanroads walikuwa na sifa nzuri lakini wameanza kuharibiwa na watumishi wachache. “Kwa hiyo watambue kuwa kipindi hiki siyo cha kufanya mchezo kila anayebainika kushindwa kutekeleza majukumu yake atambue kuwa atawajibishwa,” alisema.

Aliwataka mameneja wa Tanroads kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu barabara zote zilizoharibiwa na mvua za msimu huu zinakarabatiwa na zinakamilika.

Akifafanua, Kamwelwe alisema wizara yake imetoa zaidi ya Sh bilioni 35 kwa matengenezo ya barabara hizo na kwamba meneja atakayeshindwa kukamilisha, ajihesabu kuwa umeneja wake utaishia tarehe hiyo.

Alisema kabla ya kutoa agizo, aliwaita mameneja wa Tanroads wa mikoa yote kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma na kuwaelekeza wahakikishe wanafanya matengenezo ya barabara zote zilizoharibika kwa mvua za masika.
 
Huyu mtu ndo maana hataki hata kusikia rasimu ya Katiba Mpya.

Hivi kutokukarabati barabara na kuharibu market system ya zao la korosho kipi kimeigharimu zaidi nchi yetu?
 
Huyu kamwele nae uwaziri atausikia tu kupitia tbc FM baada ya October, boss wake keshammulika vilivyo

Labda umri inaweza kuwa kikwazo, lakini ni Engineer mbobevu, muaminifu, myenyekevu, mtiifu, mpenda watumishi wake, na sio mla rushwa. Ila tangu 2010 Waziri wa Ujenzi yeyote akiwa na chembe chembe ya rushwa kazi kwisha. Kuna vetting ya kutosha kwa waziri wa Ujenzi.
 
Back
Top Bottom