Safari ya Shaaban Robert kutoka Tanga kwenda Mpwapwa

Safari ya Shaaban Robert kutoka Tanga kwenda Mpwapwa

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
ABIRIA CHEO CHA PILI

DARAJA yangu katika kazi sasa ilikuwa imeniwezesha kusafiri kama abiria wa cheo cha pili katika gari moshi. Mapendeleo haya
yanayotamaniwa yalinijia baada ya miaka kumi na nane ya kazi serikalini. Julai 13, 1944, nilichukua tikiti, na baada ya kuagana na marafiki, nikasafiri kwenda Mpwapwa. Nilishuka Korogwe kungoja safari ya lori. Karibu ningalilala nje Korogwe kwa ukosefu wa malazi ya abiria Waafrika, lakini mtu mmoja aliyenijua zamani alinichukua kwake akanipa malazi mema. Asubuhi nilionyesha tikiti zangu za safari kwa msimamizi wa safari. Mtu huyu alinitupia jicho kwa haraka kisha akaamuru nijipakie katika lori.

Palikuwa na malori manne tayari kwa safari siku ile. Nilikwenda nikajipakia katika lori la abiria wa cheo cha pili. Mimi nilikuwa
msafiri wa kwanza kujipakia. Dakika chache baadaye Iori letu lilijaa abiria. Abiria Waafrika tulikuwa mimi na watoto wangu tu. Wengine wote walikuwa ni Wahindi. Karibu na dakika ya mwisho kusafiri pakaja Wahindi wanne wengine. Kuwapa watu hawa wanne nafasi katika lori nililojipakia mimi ilipasa watu wanne Waliokuwa wamekwisha kuingia washuke. Msimamizi wa safari, Mhindi vile vile, hakuona mtu mwingine wa kushuka ila mimi.

Baridi ina mzizimo siku zote kwa kondoo mwenye manyoya haba. Kwa maneno ya karaha alinilazimisha kushuka chini nikajipakie
katika lori la abiria wa cheo cha tatu au la mizigo. Nilimkumbusha nikisafiri kwa kazi ya serikali; nilitangulia kujipakia alikuwa hana haki ya kuniteremsha: atakavyo ililazimu vilevile yeye kunipa stashahada ya kuonyesha namna nilivyosafiri kutoka Korogwe.

Kwa maneno hayo ulimi wa msimamizi wa safari ulianza kupotoka akadai kuwa aliweza kuzuia kusafiri lori nililoingia.

Kundi kubwa la watazamaji lilikuwapo. Karibu watu wengi katika kundi lile walicheka kwa maneno ya msimamizi wa safari. Kivumo cha kicheko kilichemsha hasira yake akaamuru niteremshwe chini kwa nguvu. Matarishi waliokuwa chini ya amri yake walitii wakawa tayari kunijia wanikamate na kunitupa chini kama mtumba. lakini kitu gani sijui kiliwafanya kusita kutimiza amri ya bwana wao. Halafu nilisikia kuwa desturi ya matarishi wale ilikuwa kutii na kutimiza kila amri njema waliyopewa, na kuacha mbali kila amri mbaya hata katika hatari ya kutolewa kazini mwao. Nilifurahi sana kusikia habari hii. Idadi ya watu wema ni kubwa siku zote kuliko jumla ya watu wabaya.

Siku zangu zilikuwa zikihesabiwa. Sikutaka kuchelewa bure pale Korogwe. Niliita watu kuja kushuhudia mwamale niliotendewa
na tabia ya msimamizi wa safari. Watu wengi walikuwa tayari kunipa sahihi za mikono yao kuwa walishuhudia yote yaliyotokea.
Kisha mimi na watoto wangu tulishuka tukajipakia katika gari jingine. Nafasi iliyokuwa imebaki mle garini ilikuwa si kubwa.

Basi tulikaa juu ya mizigo yetu. Kutoka Korogwe tulikwenda Morogoro. Mchana wote ulituishia njiani. Hii ilikuwa siku ya pili
ya safari yangu, nikafurahi kushuka katika gari. Saa mbili na nusu usiku nilijipakia katika gari moshi lililotoka Dar es Salaam hata saa tisa usiku nikashuka Gulwe. Kutoka Gulwe nilichukuliwa na Iori la Idara ya Utunzaji wa Wanyama kwenda

Mpwapwa. Saa kumi alfaiiri nikawa Mpwapwa. Mwisho wa safari yangu ilikuwa ni Kikombo, lakini niliambiwa nikae juu ya gari hata saa moja asubuhi wakati mwendeshaji wetu alipoingia kwake kulala.

Kulikuwa kukizizima sana kwa baridi na umande na lori letu lilikuwa wazi. Taya za watoto wangu zilitingishika na meno yakagongana kwa kipupwe. Julai ni mwezi wa kipupwe kikali pande zile za dunia. Mbwa hafi maji akiona ufuko, na Sisi kwa kuwa sasa tulikuwa karibu kufika mwisho wa safari yetu jaribu la baridi halikutufadhaisha sana. Tulikuwa na mablanketi yaliyoweza kuzuia mzizimo wake kutudhuru.

Tulijifunika mablanketi yetu tukasaburi kuche polepole. Saa moja na nusu asubuhi nilikuwa mbele ya Msimamizi wa Afisi ya Idara ya Utunzaji wa Wanyama. Huyu alikuwa ni Mzungu. Hakuwa tayari kushikana mikono na mimi kama nilivyozoea kuona Wazungu wengine. Labda mimi nilikuwa si kitu mbele yake lakini tuliongea vema. Alisema kuwa nitapata nyumba lakini kwa namna maneno yake yalivyotamkwa niliweza kufahamu kuwa idara ilikuwa na dhiki ya makao mema. Dhiki hii ilikuwa imeenea duniani wakati ule. Bati na simenti vilikuwa adimu kupatikana kwa sababu ya Vita Kuu Na. 2. Hii ilikuwa ni Jumapili, siku ya tatu ya safari yangu. Nilipewa ruhusa nikapumzike nihudhurie kazini Jumatatu asubuhi.
 
RED GIANT,
Uandishi huu wa mababu zetu ulikuwa na ufasaha sana , siyo magazeti 'pendwa' ya kwetu zama hizi zetu za kijiditali hakuna mgeni anaweza kutumia gazeti lolote la lugha ya kiSwahili hapa Tanzania kujifuzia lugha yetu adhimmu ya kiswahili.

Nikisoma gazeti la Taifa Leo la Kenya litokalo ktk lugha ya kiSwahili naona wamedumisha uandishi wa kama huyu Shaaban Robert .

TAIFA LEO gazeti Siku 365 za kufa kupona – Taifa Leo

Siku 365 Za Kufa Kupona​

Na CHARLES WASONGA

NI mwaka wa lala-salama taifa linapokaribisha siku 365 zenye pilkapilka tele za kisiasa huku macho yote yakiwa kwa wagombeaji wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Katika kipindi cha miezi 12 ijayo, wanasiasa wanaokimezea mate kiti cha urais wanatarajiwa kuendeleza kasi ya kampeni zao katika mazingira yaliyobanwa na masharti yaliyowekwa na serikali kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.

Hata hivyo, wagombeaji wakuu, kama vile, Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ODM Raila Odinga, Kalonzo Musyoka (Wiper), Musalia Mudavadi (ANC) na Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi wamebuni mbinu ya kuendesha kampeni zao kupitia majukwaa ya makanisa na kukutana faraghani na makundi mbalimbali.

Japo, Bw Odinga hajatangaza waziwazi kwamba atawania urais, mwanasiasa huyo mkongwe amekuwa akitangaza sera mbalimbali ambazo ananuia kutekeleza endapo atafanikiwa kuunda serikali ijayo.

Kufikia sasa ametoa ruwaza yake inayojikita katika ukuzaji wa uchumi kuanzia ngazi ya vijiji, uboreshaji wa utumishi wa umma na kufanikisha mabadiliko katika sekta ya afya kupitia utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote (UHC).

Bw Odinga amedokeza atatangaza rasmi azma yake ya urais mwishoni mwa mwezi huu baada ya mahakama ya rufaa kutoa uamuzi kuhusu mswada wa mageuzi ya katiba kupitia mpango wa maridhiano (BBI).

“Mwishoni mwa Agosti, tutatoa tangazo kubwa ambalo litasababisha Tsunami kubwa katika uwanja wa siasa nchini. Hata hivyo, wakati huu tunasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu hatima ya BBI na tuko tayari kukubali uamuzi wowote utakaotolewa kwa sababu mimi na Rais Kenyatta ni wanademokrasia,” akasema Julai kwenye mahojiano na Radio Citizen nyumbani kwake Karen, Nairobi.
Jopo la majaji saba wakiongozwa na Rais wa Mahakama hiyo, Daniel Musinga, hapo Agosti 20 litatoa uamuzi kuhusu kesi iliyowasilishwa mbele yalo na wakereketwa wa BBI kupinga hatua ya mahakama kuu kuharamisha mageuzi hayo ya katiba.

Katika kipindi cha miezi 12 ijayo, Dkt Ruto, ambaye ametangaza azma yake ya kuwania urais kwa tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) baada ya kugura Jubilee, anatarajiwa kuendeleza kampeni zake licha ya kudinda kugura chama hicho tawala.

“Sisi si wageni popote pale. Tunajiunga na vyama vya kisiasa kwa hiari na kuondoka kwa hiari. Hamna anayepaswa kuuliza kwani tungali hapa. Hatukualikwa nchini,” akasema Alhamisi baada ya kuongoza mkutano wa wabunge wanaoegemea mrengo wa Tangatanga.
Dkt Ruto alikuwa akijibu miito ya wandani wa Rais Kenyatta na Bw Odinga wanaomtaka kujiondoa rasmi kutoka Jubilee na serikalini badala ya kuendelea kuikosoa akiwa ndani.

Mkutano huo uliofanyika katika makazi rasmi ya Naibu Rais, mtaani Karen pia ulijadili mikakati ya kuvumisha sera yake mpya ya kuchochea ukuaji wa uchumi kutoka mashinani, kuendelezwa kwa shughuli za usajili wa wanachama wa UDA na kufanyika chaguzi za mashinani za chama hicho kuanzia Oktoba 2021.

Kuanzia sasa hadi mwezi Mei 2022 wakati vyama na miungano, itakapoanza kuteua wagombeaji wa urais, Dkt Ruto na Bw Odinga watakabiliwa na kibarua kigumu cha kuteua wagombeaji wenzao.

Duru zinasema wawili hao wanatarajiwa kuteua wagombeaji wenza kutoka eneo la Mlima Kenya endapo eneo hilo halitatoa mgombeaji urais mwenye ushawishi mkubwa kumzidi Bw Muturi anayetoka eneo la Mlima Kenya mashariki.

Muungano wa One Kenya Alliance (OKA) unaoshirikisha Mbw Musyoka, Mudavadi, na kiongozi wa Ford Kenya, Moses Wetang’ula watakabiliwa na kibarua cha kuamua ni nani kati yao atakayepeperusha bendera yake katika kinyang’anyiro cha urais.
Mbw Musyoka na Mudavadi wamekuwa waking’ang’ania nafasi hiyo huku kila mmoja akidai ndiye anayefaa kupambana na Dkt Ruto na Bw Odinga katika uchaguzi hui

Mbali na wagombeaji urais, macho ya Wakenya yataelekezwa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ambayo inakabiliwa na kibarua kizito cha kufanikisha maandalizi ya uchaguzi mkuu huku ikilalamikia bajeti finyu. Kulingana na mpango wake kuhusu uchaguzi (Election Operations Plan-EOP) wa hadi Agosti 9, 2022, IEBC imeorodhesha shughuli kadhaa ambazo zitahitaji fedha nyingi.
Kuanzia Septemba, IEBC itaanza kutekeleza mpango huo kwa kuzindua usajili wa wapigakura kwa halaiki.

Tayari tume hiyo imetangaza zabuni ya ununuzi wa vifaa vya kutumika katika uchaguzi mkuu ujao.

Septemba IEBC, inatayariwa kupata makamishna wanne wapya walioteuliwa na Rais Kenyatta wiki hii.

Wao ni; Francis Wanderi, Justus Abonyo, Juliana Cherera, na Irene Cherop ambao majina yao yamewasilishwa bungeni kupigwa msasa.
 
RED GIANT,
Shajara alizotunza na kutusimulia ktk lugha ya Kiswahili cha 'kina' Shaaban Robert kinavutia, unajiona kama upo nao kipindi hicho cha matukio katika safari yao.

GAZETI LA TAIFA LEO HUKO KENYA WANAKIENZI KISWAHILI KWA UANDISHI BORA

  • Aug 06, 2021

Uganda Yamruka Ruto Kuhusu Ziara Yake Iliyotibuka

Na LEONARD ONYANGO

SERIKALI ya Uganda imemruka Naibu wa Rais William Ruto kuhusu ziara yake iliyotibuka mapema wiki hii, ikisema haikumtarajia.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Okello Oryem jana alisema hawakufahamishwa na ubalozi wa Kenya kwamba Dkt Ruto alistahili kuzuru taifa hilo mnamo Jumatatu.

Oryem pia alikanusha madai kwamba Rais Yoweri Museveni anaingilia siasa za Kenya kwa kuunga mkono Dkt Ruto.Mnamo Jumatatu, Dkt Ruto alizuiliwa kuelekea nchini Uganda kama alivyopanga.

Alilazimika kukaa katika uwanja wa ndege wa Wilson kwa muda wa saa tano, lakini mwishowe maafisa wa uhamiaji wakakataa kumruhusu kusafiri.

Lakini wabunge Oscar Sudi (Kapseret), Benjamin Tayari (Kinango) na Ndindi Nyoro (Kiharu) pamoja na wafanyabiashara wandani wake waliruhusiwa kusafiri hadi Uganda.

Dkt Ruto alisisitiza kuwa ziara yake ilikuwa ya kibinafsi, hivyo hakuhitajika kupata idhini kutoka kwa mtu yeyote.

“Hatukupokea ombi lolote kutoka kwa ubalozi wa Kenya la kututaka kutoa huduma za mapokezi kwa Dkt Ruto,” Bw Oryem aliambia gazeti la New Vision la Uganda.Bw Oryem alisema sera ya Uganda hairuhusu taifa hilo kuingilia siasa au masuala ya ndani ya nchi nyingine.

“Kenya inaongozwa na kiongozi aliyechaguliwa, Rais Uhuru Kenyatta na anafanya kazi nzuri na hakuna sababu yoyote ya Uganda kuingilia siasa za majirani wetu. Hatuna mamlaka ya kuingilia masuala ya Kenya na wao ndio wanajua kwa nini walimzuia Ruto kuja Uganda,” akasema.

Jana alipokuwa akihutubia wanahabari baada ya kukutana na wabunge wanaomuunga mkono, Dkt Ruto alikataa kuzungumzia ziara yake nchini Uganda.Mnamo Jumatano alisema kwamba Rais Museveni ni rafiki yake.

“Ni kweli kwamba Museveni ni rafiki yangu. Nimewahi kumfanyia kampeni. Na viongozi wote wa Nasa pia wamewahi kumfanyia kampeni. Sasa ikiwa yeye ni rafiki wa wote, mbona kuna shida kubwa ikiwa nitamtembelea kiongozi huyo?” akauliza.

Wandani wa Dkt Ruto wamefichua kuwa analenga kujumuisha washauri wa siasa wa Rais Museveni katika kikosi chake cha kampeni anapojiandaa kuwania urais 2022.

Bw Sudi aliambia Taifa Leo kuwa walienda Uganda kujifunza kutoka kwa chama tawala cha Uganda, Nation Resistance Movement (NRM) ambacho kimekuwa mamlakani kwa miaka 35 chini ya Rais Museveni.

Ufichuzi huo umezua mjadala mkali nchini, huku wanasiasa wa ODM wakidai kuwa Dkt Ruto anapanga kutumia NRM kusababisha machafuko nchini endapo atapoteza katika uchaguzi wa urais 2022.

Source: Taifa Leo – Page 3 – Ng'amua ukweli wa mambo
 
RED GIANT,
Shajara alizotunza na kutusimulia ktk lugha ya Kiswahili cha 'kina' Shaaban Robert kinavutia, unajio kama upo nao kipindi hicho cha matukio katika safari yao.

Source : Taifa Leo – Page 3 – Ng'amua ukweli wa mambo
Wako vizuri sana, inafurahisha kuwasoma. Bahati mbaya waandishi wengi leo hawana ufasaha wa Shaaban Robert. Robert si tu alikuwa na misamiati mingi, lakini hata namna anapanga sentensi zake, ukisoma leo unaweza sema kakosea kumbe ndivyo inapaswa kuwa. Nimesoma vitabu vyake, hiki cha tano, nimemvulia kofia.
 
Ubaguzi miaka hiyo ulikuwa mwingi sana, sasa tuna wakoloni weusi wanaoitwa CCM ni wezi na wavunja haki kuliko wakoloni weupe
 
Wako vizuri sana, inafurahisha kuwasoma. Bahati mbaya waandishi wengi leo hawana ufasaha wa Shaaban Robert. Robert si tu alikuwa na misamiati mingi, lakini hata namna anapanga sentensi zake, ukisoma leo unaweza sema kakosea kumbe ndivyo inapaswa kuwa. Nimesoma vitabu vyake, hiki cha tano, nimemvulia kofia.

Tazama muandishi wa habari wa Tanzania zama zetu hizi vijana wa kidijitali anavyoandika kusimulia au kuhadithia :

VIDEO Vixen Bongo, Ana Kimario ‘Tunda’ amesema anashangaa kuona watu wakimnanga kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameachana na mpenzi wake wa sasa Whozu wakati si kweli. Akizungumza na Amani, Tunda alisema Wabongo siku zote wamekuwa na mawazo hasi tu badala ya kuwawazia mazuri.

“Nashangaa watu wanasema kuwa mimi nimeachana na Whozu, yaani wanapenda kuniombea mabaya tu, siku nyingine wawe wananiombea heri basi. Sasa niwapashe tu, sijaachana na Whozu na sitarajii kuachana naye, watasubiri sana kwa hili,” alisema Tunda
 
Na uandishi huu unavikuta kwenye riwaya nyingi leo. ukisoma kidogo unakuta hamu imeisha. Ni kweli lugha inabadilika na inatakiwa kuwa rahisi, lakini kwa waandishi wetu imekuwa too much. Hata waandishi wa scripts za filamu zetu hawana ufasaha/lugha ya kuvuta watu. Mwisho wake kisa kizuri kinasimuliwa vibaya.
 
Kiswahili cha wakati ule na sasa ni tofauti kubwa sana kitu ambacho naona sio kibaya au kizuri, lugha zote zinabadilika na wakati na maneno mapya huzaliwa kila siku ndio maana hata dictionary/kamusi ya kizungu kuna maneno mapya huongezwa kila mwaka, kuna maneno tulikuwa tunatumia miaka ya 90 ukiongea leo mtoto mdogo hawezi kukuelewa na ki8swahili sanifu kabisa
 
Nakubaliana lugha ya kuzungumza mitaani au vijiweni inaweza kubadilika lakini inapokuja ktk uandishi ktk magazeti, somo la kiswahili shuleni, kuandika barua kuomba kazi, utangazaji ktk media inatakiwa kiswahili sanifu kitumike na siyo tunachotumia mitaani.

Na ndiyo maana tunaona tofauti ya uandishi wa habari Kenya pamoja na kuwa mitaani wana kiswahili cha 'sheng" lakini inapokuja kiswahili cha kuandika mashuleni, magazetini na utangazaji wanazingatia utumiaji wa maneno rasmi ya kiswahili.
 
Back
Top Bottom