vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Habari.....
Simba baada ya kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi wakapanga safari ya Dubai. Hii safari ipo kisanii sana, kiukweli kutokana na ufinyu wa muda sidhani kama ilikuwa sahihi kwa Simba kwenda Dubai.
Wachezaji hawana miili ya chuma kuna wasaa wanahitaji kupumzika lakini unawasafirisha kwenda mbali safari tu inaongeza uchovu. Mbali na hapo kuna session kabambe zimepangwa na kocha za mazoezi.
Kuna ratiba ya mechi ya ligi kuu tarehe 17 mwezi huu lakini ndio kwanza wameomba mechi za kirafiki za majaribio, ni kama wale wanafunzi wanaokomaa kujisomea siku za mtihani hadi dakika dakika za kuingia ndani ya mtihani kana kwamba siku zote hakujua kama ana mtihani mbele yake.
Tarehe 15 wameomba mechi ya kirafiki na huku tarehe 17 wanatakiwa kucheza mechi ya NBC dhidi ya Mbeya City sasa haya yanafanywa kwavile wanajua nipo wanajulikana wenye mamlaka ya soka ni mtu wa namna gani hivyo ni rahisi kwa mechi kughairishwa ama hawakujua ratiba ya ligi?
Binafsi sijaona manufaa ya hii safari zaidi ya kwenda kuwachosha wachezaji kwasababu ya ufinyu wa muda labda kama kuna kitu chini ya pazia kilicholengwa juu hii safari kwa mgongo wa kambi.