Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,158
Ilikuwa 2012, nilichukua package holiday ya siku tano ilijumlisha hoteli ya nyota tatu, nauli ya ndege na usafiri wa ndani kwa £1,200. Hii ilikuwa inajumlisha chai asubuhi na chakula cha usiku.
Tulikuwa watu 10 kwenye group kwetu. Tulipofika airport Dereks wa tour alishika bango eneo la mapokezi alihakikisha wote 10 tumeonana nae alichukua passports zetu na kwenda nazo immigration. Sifahamu ilikuwaje aliweka kupita na kutupokea baada tu ya kushuka kwenye ndege.
Alirudi baada ya nusu saa akiwa na passport zenye visa ya miezi mitatu. Tulipanda kipanya mpaka hotelini.
Alituaga kuwa atakuja kutuchukua saa moja usiku kwa dinner. Dinner kwenye boat ndani ya mto Nile.
Kulikuwa na supermarket inatazamanana na hoteli, unaweza kununua matunda na maji na vitu vingine vidodogo.
Dance ilikuwa live band na tuliachwa kukaa pale mpaka saa sita usiku. Kulikuwa na chupa ya mvinyo kwa kila mtu insensate na chakula, baada ya hapo pombe ya ziada unajigharamia. Saa sita usiku tour driver aliturudisha hotelini lakini waliotaka kuondoka mapema walisaidiwa pia.
Asubuhi alikuwa saa nne alituchukuakwenda kupanda ngamia. Saa tisa mchana aliturudisha hotelini kupumzika. Wengine walikwenda beach mchana ule, wengine walilala ili mradi wote tulichukuliwa tena saa moja kwa chakula.
Siku ya pili tulitembelea pyramids, ni ajabu lile joto la Cairo ukiwa chini ya pyramid hakuna joto kabisa. Tulitemelea na kupewa historia yake. Tulirudi hotelini saa 10 jioni kupumzika.
Siku ya tatu tulitembelea shamba la maua na shamba la viungo. Wanalima mauwa ridi ya rangi zote. Pia wanakamua mafuta ya uaridi unauziwa kwenye ki chupa cha ukazo wa 100 mls. Yote haya yanamwagiliwa na mto Nile.
Siku ya mwisho kuondoka Cairo wote tulimpa bakshish tour driver kwa mapikezi na huduma aliyotupa.