Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Habari za wakati huu, nimeona niwashirikishe kidogo Wazee wenzangu wa Road trip haka kamsafara kangu kadogo.

Nilipanga kuwa mwaka huu nizunguke kwa gari baadhi ya mikoa, LENGO ikiwa ni kupunzisha ubongo tu na kujionea huko kwingine...LENGO ilikua nianzie Dar-Lindi-Songea-Njombe- Mbeya-Rukwa-Katavi-Kigoma-Bukoba-Mwanza-Mara-Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma-Moro-Dar ila baada ya kuwaza sana nikaona kwa mwaka huu nijaribu route fupi kidogo.

Safari yangu ilianza tarehe 5/12/2021 kutoka Dar mchana kwenda Njombe, niliondoka Dar saa kumi jioni, nikapumzike Moro kidogo then nikapumzika Mafinga Kisha nikamalizia safari Hadi Njombe, nikifika muda wa saa tisa usiku, nikaenda giraffe pale nikamalizia usiku hapo.

Siku iliyofuata nikatembea hapa na pale kidogo ila kesho yake Ikawa nataka kwenda Kitulo kupitia Makete nikalale Kitulo Kisha nidondokee Mbeya, kwa bahati mbaya sana baada ya kufika Makete almost two or three kilometers kutoka Makete nikapotea njia... nilikuta junction sasa baada ya kwenda kulia nikapita kushoto. Nikatembea mwendo mrefu tu huku Barabara ikiwa mbaya, ikafika mahali mlimani na msituni nikakwama, nikaamua kurudi, ndio nikauliza wenyeji wakasema nimepotea sana. Nikaghadhibika nikarudi Njombe Mjini. Siku Ikawa imeisha.

Siku iliyofuata mchana nikaamua kuondoka Njombe, kuanza safari ya Kigoma. Saa nane mchana baada ya kupata lunch pale Glory Hotel nikaondoka taratibu sana.

Nikafika Dodoma usiku wa saa Tano, nikaamua nisogee Hadi Manyoni. Nikapumzika Manyoni pale Pretoria Hadi saa Moja asubuhi nikaondoka zangu.

Saa nne nikafika Tabora, nikapumzika one hour nikapata supu. Muda wa saa Tano nikaondoka sasa kuitafuta Kigoma, Barabara ilikua mbaya baadhi ya maeneo, kuna maeneo kuna lami na kwingine hakuna lami Hadi uvinza. Nikafika Uvinza saa 11 jioni.

Nikatembea sasa kwenye lami Hadi Kigoma, Nikalala Mwitongo Hotel, asubuhi nikazunguka mjini nikaenda kuonana na wadau wangu siku Ikawa imeisha.

Asubuhi nikaondoka kwenda Kasulu, nikafika Kasulu nikatafuta kifungua kinywa nikaendelea na safari, kuanzia Kasulu Hadi Kibondo mjini ni rough road Moja matata sana, lami Iko Pale mjini tu, nikaonana na Wadau wangu hio ni saa tisa mchana sasa nimeshapunzika. Jamaa wakanishauri nisiondoke, tukabadilishana mawazo pale na networking.....

Asubuhi nikaondoka kutoka Kibondo na penyewe ni rough road ya maana tu sema Kuna Ujenzi inaendelea kwa MKOPO kutoka AfDB. Lami nikaikuta Kakonko sasa, nikasimama nikapiga picha kuagana na rough road.

Nikatembea Hadi Nyakanazi, Runzewe, Masumbwe to Kahama. Kahama nikapumzika kidogo maeneo ya kule kwenye maegesho ya serikali, Kahama Pana starehe aiseeee.

Nikatembea zangu saa tisa mchana Shelui, nikapata Company nikajivuta Hadi Singida. Nikalala sikutaka kuendelea na ligi na yule kijana, alinikuta kule mizani namwaga Maji kidogo, akasimama tukaagana nikamwambia sitaweza kuendelea na safari.

Asubuhi nikaanza safari Hadi Dodoma nikapumzika, mchana nikaanza safari Tena Hadi nafika Dar ilikua saa sita usiku.

Hivi ndivyo nilivyoitumia Likizo yangu ya December 2021 kwa kutembelea maeneo hayo kujenga network na kubadilisha mazingira kidogo.



























 
Tanzania ni kubwa jamani..unaweza kuta kuna mtu kazaliwa sehemu kasoma shule za kata hapo hapo na kama alipo kuna chuo pia kasoma hapo hapo mtu kama huyo hana exposure yoyoye..
Niko Mtwara mikindani nabarizi kidogo..wa pande hizi mje basi.
 
Hongera sana msafiri kwa kusafiri.

Binafsi napenda sana kusafiri na huko mbeleni nataka ninunue gari nzuri zaidi ya kuniwezesha kusafiri bila mawazo ikiwezekana na familia kabisa.

Pesa ni ngumu naamini nitazipata tu.
 
Nitakuja January mwishoni Mungu akitupa uhai
 
Duhhhh hiyo IST ndo umepiga nayo masafa marefu hivyo.. anyway nzur sana mkuu nakumbuka mwaka jana nilipiga road trip dar-arusha-karatu-babati-hydom-singida-dodoma-dar n nzur kwa kwel especially upo na kampan ya watu wawil ...
 
Hongera sana msafiri kwa kusafiri.

Binafsi napenda sana kusafiri na huko mbeleni nataka ninunue gari nzuri zaidi ya kuniwezesha kusafiri bila mawazo ikiwezekana na familia kabisa.

Pesa ni ngumu naamini nitazipata tu.
Mungu ajibu haja ya moyo wako. Amen
 
Duhhhh hiyo IST ndo umepiga nayo masafa marefu hivyo.. anyway nzur sana mkuu nakumbuka mwaka jana nilipiga road trip dar-arusha-karatu-babati-hydom-singida-dodoma-dar n nzur kwa kwel especially upo na kampan ya watu wawil ...
Niliwaza kutumia Nissan Xtrail nikahofia kama nikipata breakdown, zile gari ni umeme 100% na mafundi wetu wa mkoani hawa
 
Kwa hiyo mkuu ulitembelea hiyo IST kwa safari yote, yaani kwenye barabara nzuri (lami) na mbovu (vumbi)?

Tupe uzoefu wako katika hilo la kutumia IST, kuanzia kwenye mafanikio, matatizo, changamoto, tahadhari, mbinu nk.

Maisha ni safari...
Maisha ni mafunzo...
Safari ni mafunzo....
Mafunzo ni safari.....
Maisha ni safari ya mafunzo....
Safari ya mafunzo ni maisha...
Mafunzo ni safari ya maisha...
SAFARI NI MAFUNZO YA MAISHA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…