Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Hongera kutalii.

Siku nyingine jaribu route hizi

1. Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Songea - Mbinga hadi Mbamba bay Nyasa ziwani, kisha rudu Dar kupitia Njombe - Iringa - Moro.

2. Dar - Moro - Iringa - Makambako - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga hadi Katavi (Mpanda) Kisha rudi Dar kupitia Stalike - Majimoto - Muze - Mtowisa hadi utokee Mlowo ili uende Mbeya kisha Chunya - Makongolosi hadi Tabora ndio uende Dar kupitia Itigi - Manyoni - Dom - Moro.

Amini nakuambia, ukimaliza route hizo, utakuwa umejifunza mengi sana.

Tembea kwa saa kumi au kumi na moja kwa siku. Kisha pumzika kwenye mji, furahia maisha kisha siku ya pili uendelee. Usitembee usiku kwa safari za kitalii.
 
Fuel consumption ni the best. Nilijitahidi sana isipungue nusu tank. Nilijitahidi pia RPM isivuke 3-4 kwahio nilikua nakimbia kwa tahadhari hio.

Nilizingatia service sana na nilijitahidi kuisikiliza Kila wakati

Namshukuru Mungu sikupata tatizo LA kiufundi kwa kweli. Kwa ujumla nilifanya uchaguzi sahihi kutumia IST
 
1. Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Songea - Mbinga hadi Nkata bay Nyasa ziwani, kisha rudu Dar kupitia Njombe - Iringa - Moro.
Hii niliwahi kwenda, natamani sana Ile ya Mbeya-Itigi....

Sumbawanga nimefika Mambwemkoswe, Kaburi Wazi, katavi-Tanganyika-Mlele Hadi Tabora kwenye Abuja sema ilikua kikazi sio binafsi
 
Dah, usisahau kufika msimbati kuna bonge la beach hatari, ukitaka kusafisha macho nenda shuttaz
 
Mpwa Nisamehe, kesho nitakua na safari ya Dar to Dodoma then nitageuza Dodoma-Tanga. Naahidi kukutafuta kesho au keshokutwa asubuhi. Tutaenda kugonga breakfast pale Mwambao Restaurant kwa Wale Wapemba
Fanya hivyo maana nina hasira hapa balaa unaachaje kuja WASWANU kula makange ya samaki?
 
Hongera sana. Nami pia nilikuwa likizo, almost njia hiyo hiyo, ingawa mimi nilipitia mbeya, Rukwa, Katavi, kuingilia uvinza.

Niseme ukweli, Mkoa wa Kigoma umesahauliwa sana, na hasa kwenye Miundombinu! Kile kipande cha Kaliua-Nguruka na Malagarasi-Uvinza kina zaidi ya miaka 5 kiko vile vile,

Kiukweli kabisa inauma mnoo, kwakuwa haikupaswa mpaka muda huu kiwe vile, sababu imekuwa muda sana na kiasi kwamba mtu unajiuliza je, Sirikali ina agenda ya siri juu ya watu wa Kigoma juu ya maendelo yao??

Lakin pia wakati narudi nilipitia njia ulosema kwa maana ya kasulu-Nyakanazi! hali ya barabara inatisha mnoo!

Serikali iwakumbuke wakazi hawa, maana nadhan umebaki mkoa pekee ambao haujaunganishwa kwa lami hapa Tanganyika.
 
Kote huko nimepita Wakandarasi wako kazini, wale wa Kasulu-Kibondo-kakonko na Buhigwe hawatachelewa maana ni mkopo kutoka AfDB
 
Nimependa Tripu,Mimi ni mdau wa Road Trip,Naona IST imefanya KAZI nzuri hadi inaona RAHA.Hongera.


Mi napanga TRIP YA MANYARA MUSOMA MWANZA KAHAMA TABORA
 
Hizo pic zako ungekuwa unazipa na rebo kabisa ili tujue ni wapi, hongera sana kwa safari, wengine tukisafiri sana chalinze na bagamoyo [emoji23]
Labda siku nikiwa kwenye laptop nitafanya editing, nilitamani sana kufanya hivyo. Shukrani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…