Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Siku mbili tatu zilizopita, nilijaribu kutembelea vijiji kadhaa katika mikoa mitatu; nilichokutana nacho huko ni kama ifuatavyo:-
Vijana wamepungua vijijini
Kuna vijana wachache sana, waliobaki vijijini; nilikuwa natembea umbali mrefu sana bila kukutana na mtu/kijana.
Katika mita sq 2000 naweza kubahatisha kukutana na kijana mmoja au hakuna.
Wazee ni wachache
Hii inatokana na wengi kufikia umri mkubwa na kufariki, na hatimaye idadi kupungua.
Vijana waliopo vijijini wanazeeka haraka
Baadhi niliokutana nao walikuwa na sura au miili ya kuwa wazee, kutokana na mazingira ya kijiji au unywaji wa pombe unaopelekea kuchoka mapema.
Majengo/nyumba hazina watu
Watu wanajenga kijijini lakini wanaishi mjini; na huku kijijini wanakuja kipindi cha mwisho wa mwaka, na kupelekea nyumba nyingi kutokuwa na wakaaji au kuonekana maghofu.
Fursa nyingi kijijini ila wajanja hawataki kuwekeza vijijini
~ Kuna ardhi yenye rutuba.
~ Kuna vyanzo vya maji.
~ Kuna nguvu kazi nafuu 'cheap labour' n.k.
Ushauri
Tuliopo mjini, tujitahidi tuwekeze kijijini kwa uzalishaji, na masoko yawe mjini; hii itaongeza idadi ya watu vijijini pamoja na kuboresha maisha ya wakazi wote wa vijijini, kuliko kwenda kuwarushia matope na vumbi kipindi cha mapumziko.