cmoney
JF-Expert Member
- Oct 14, 2011
- 3,570
- 5,508
Basi safari yangu ikanituma kwenda kisiwa cha Mafia ambapo nashukuru Jamiiforums ndo moja ya sehemu nilipopata maelekezo zaidi jinsi ya kufika huko kwa kupitia bandari ndogo ya nyamisati ambapo kuna majahazi yanayokupeleka hadi kisiwani.
Safari ilianzia mbagala mida ya saa 11 jioni ambapo kwa nauli ya 5500 iliweza nifikisha hadi bandari ya nyamisati ambapo tulifika saa 3 na kwa bahati mbaya tiketi za majahazi zilizokua zinakatwa kwa tsh 16000 zikawa zimeisha ila wenyeji wakaniambia itakapofika alfajiri tutaongea na Mabaharia na safari itakua sawa.hili ni swala la kuangaliwa kwa ukaribu kwani ilipofika saa 9 alfajiri waliona tiketi walifanikiwa panda ila bado tusiokuwa na tiketi tulikua zaidi nusu ya wasafiri na wote tulipanda ingawa kutokana na kutokua na uangalizi wa mamlaka zinazohusika jahazi lilionekana kabisa limepandisha kupita kiasi bila kua na vifaa vyovyote vya uokoaji kama vile maboya au vitu kama hivyo na jahazi likiwa limepandisha wanaume wanawake na watoto wakiwa wengi.
Tunashukuru Mungu safari ilifika salama bandari ya kilindoni na kutokana na tishio la ugaidi hata usalama ulikua juu ambapo kila abiria aliyekua anaingia alitakiwa kuonesha kitambulisho ili kujua wanaoingia kisiwani hapo.
Nilifikia nyumba ya wageni iliopo eneo la kilindoni na baada ya kuulizia wageni wakanielekeza eneo la utende ambapo kuna hotel za kitalii na fukwe za kuvutia.Nilipokua fukwe za bahari za utende zilizojaa hotel mbalimbali za kitalii hupendelea kukaa na wenyeji na kubadilishana nao mawaidha ili niweze ujua zaidi mji au eneo nnalolitembelea.
Ndipo nilipopata bahati ya kukutana na vijana wanaokaa fukwe za bahari kwa jina beach boys ambapo mmoja wapo akaja na katika kuonge naye akanambia anarupia ya kijerumania ambayo kama naweza mtafutia mteja.
Kusema kweli nilivutiwa kujua zaidi kuhusu hiyo sarafu kwani tumesikia historia mbalimbali kuhusu fedha hiyo.Kama alivyoahidi kijana alienda sehem na kurudi nayo na katika kuiangalia ilikua ni robo rupia ya mjerumani iliyotengenezwa kipindi cha utawala wao nchini Tanganyika.Kwa msaada wa google niliweza pata thamani yake kua kama paund 33 za kiingereza.Nilichojifunza hizi pesa kweli zinathamani hata kwenye masoko ya wenzetu wazungu na kama unapata bahati ya kuzipata nyingi let say 100 au 1000 unaweza jipatia kiasi kizuri...basi wadau wenzangu ambao mpo tayari kusaka utajiri*'TREASURE HUNTS. Bado hamjachelewa.
Nawasilisha