Jemima Mrembo
JF-Expert Member
- Jul 19, 2021
- 2,864
- 8,328
Noela Shoo ni binti mdogo kwa umbo lakini she is so tough in action. Wadada na wamama Tunaopenda hiking tumekuwa tukiongozwa mara nyingi na wanaume, na kama ujuavyo changamoto zinazokabili mbuga na hifadhi zetu, vyoo ni mpaka ukute camp, kwa hiyo ukiwa njiani huwi comfortable sana.
This weekend from Thursday to Sunday nilikuwa nimeenda na Mr. Husband na baadhi ya wana JamiiForums wenzangu mbugani kidogo, kuvuta hewa ya baridi.
Tulichagua kwenda Udzungwa National Park ambapo tungeweza kuona wanyama, kufanya hiking (kupanda milima mirefu) na kutembelea maporomoko ya maji.
Safari yetu ilikuwa nzuri na tukaanza safari ya mlimani siku ya Alhamis hiyohiyo saa kumi jioni.
Safari yetu ilikuwa ya wabeba mizigo kadhaa, mizigo yangu na husband ilibebwa na WAGUMU Frank Mathias Pulapula na MGUMU Gaudence Williams, wana JF wengine pia walikuwa na wapagazi wao, wakitaka kuonesha shukrani na kuwathamini mchango wao watafanya hivyo kwa wakati na nafasi zao binafsi.
Pia tulikuwa na ranger, kijana wa Kichagga kutoka Rombo, kijana mkakamavu Peter Swai (Ismail) na binti kiongozi wa msafara na muongoza watalii Noela Shoo.
Siku hiyo ya Alhamisi tulianza safari ya kupanda kilele cha MWANIHANA kwa kupitia maporomoko ya Sonjo, kisha tukaelekea eneo la kupumzika, wenyeji wanapaita shell.
Hili ni eneo ambalo mto unapita na pana mawe mawe, makubwa kwa madogo yakiwapa wageni na wenyeji wao nafasi ya kupumzisha miili, kunywa maji, kujilowanisha na kuchota maji ya kunywa njiani.
Tukaendelea kwenda mdogo mdogo huku tukipanda milima na vilima hadi kulifikia eneo la MIZIMU. Hapa pana mto unapita na pana miti mirefu sana. Pia pana kidaraja cha chuma. Hapo tukapumzika na kupiga picha, tukanywa maji tena na kuchota mengine. Hapa tulifika saa 12 kasoro.
Baada ya hapo safari ikaendelea kuitafuta camp ya GMP ambapo tungepiga kambi, kupika, kula na kulala.
Hapa camp GMP tulifika saa mbili kasoro kumi usiku tukiwa na mahema yetu, nguo na vyakula.
Usiku huo tulikuta kambi imefurika watu wengi waliokuwa wanatengeneza njia kwa ajili ya watalii wanaoenda Mto Rumemo na Rumemo Peak.
Hapa tulitengeneza chakula laini, mikate, mayai, siagi, matunda na chai ya masala. Pia tulikula nuts mbalimbali, karanga, korosho na almonds.
Asubuhi WAGUMU hawakuwa tena na kazi ya kutubebea mizigo, safari yao ilikomea GMP CAMP. Wagumu walitusongea ugali ambao tulikula na mayai ya kukaanga yaliyochanganywa na nyanya, pia tulikula samaki, na mtindi. Baada ya mlo safari ya kilometa 7 kupanda milima kwenda Mwanihana Peak ikaanza.
TAREHE 09.12.2022. SAFARI KUTOKA GMP CAMP TO MWANIHANA PEAK.
Tuliondoka GMP CAMP saa moja na dakika 37 asubuhi, huku tukiwaacha WAGUMU hapo camp wakipumzika na wakituandalia chakula cha usiku, ili tukishuka kutoka mlimani tule, tulale na kesho yake asubuhi tushuke Mang'ula Mwaya kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kwenda Sanje Waterfalls kesho yake.
Tulianza safari yetu kwa kuvuka kijito kilichopo kandokando ya camp, tukachota maji ya kunywa hapo maana hiyo ndiyo LAST WATER POINT, huko mbele hamna tena maji.
Baada ya kuchota maji, tukaanza mdogo mdogo kupanda milima huku tukisindikizwa na sauti mbalimbali za ndege. Muongoza watalii wetu Noela Shoo alikuwa ni mahiri wa kututajia majina ya ndege tunaowaona. Aliwataja kwa majina ya Kiswahili, ya Kingereza na ya Kibaiolojia. Pia alitutajia sifa za ndege hao.
Mwingoni mwa ndege niliovutiwa nao sana alikuwa ni Hondo hondo.
Noela alitueleza kwamba hondo hondo joke anapoanza kulalia/kuatamia mayai, basi hujinyonyoa manyoya yake yote mwilini, na huyapanga sehemu anayotarajia watoto watakaa.
Dume lina jukumu la kuijenga hiyo nyumba/ kiota na mifumo yake yote ikiwa ni pamoja na choo.
Baada ya hapo dume husiliba kiota chote kwa matope na kuacha tundu sehemu ya mdomo tu. Ambapo dume atawajibika kumletea mkewe matunda 150 kila siku.
Jike ataendelea kukaa bila manyoya hadi atakapo angua mayai yake na atakaa katika hali hiyo hadi watoto wake wakianza kuota manyoya ndio naye manyoya yake yataanza kuota.
Manyoya ya watoto wake yakikomaa na manyoya ya mama huwa yamekomaa na huo ndio huwa mwisho wa maisha ya kiotani.
Ikitokea baba hondo hondo ameuawa kwenye hekaheka za kutafuta chakula cha mkewe na watoto, basi huo ndio utakuwa mwisho wa familia. Kwani mama huwa hana manyoya wala uwezo wa kuruka na anakuwa amefungiwa kiotani.
Safari ya kuoanda milima iliendelea, upto wa asili ukabadilika, tukaingia eneo lenye miti mirefu sana na mikubwa sana, majani ya kijani sana na mawe makubwa makubwa.
Hapa wenyewe wanapaita Mandela
Sehemu hii ni nzuri sana. Tukakaa hapo kidogo kwa ajili ya picha, utani kidogo, vistori vya hapa na pale huku tukikumbushana thread za kusisimua za Mshana Jr, maswahibu ya GENTAMYCINE, vituko vya Bill Lugano na wana JF mbalimbali.
Sikujua kuwa tembo ana uwezo wa kupanda milima mirefu, huko juu kwa mbali tuliliona kundi la tembo, kiongozi wetu Noela Shoo akatushauri tusiwasogelee, tusiwapige picha kwa flash na wala tusipige kelele. Akatuambia kwamba tembo uwezo wao wa kuona ni mdogo ila wana uwezo mkubwa sana wa kunusa na kusikia.
Tukapanda mlima hadi tukalikuta bwawa. Hilo bwawa ndilo hutumiwa na wanyama mbalimbali kunywa maji. Pia hutumiwa na tembo kujipooza miili yao kwa kujipaka tope.
Tuliendelea na safari hadi saa saba kasoro tulipofika summit. Urefu wa kutoka GMP Camp hadi Summit ni kilometa saba. Na umbali wa kutoka GMP Camp hadi tunapo anzia kupanda mlima ni safari ya kilometa 12.
Hivyo basi trail nzima ya kupanda mlima kuanzia mwanzo hadi kileleni Mwanihana Peak ni kilometa 19. Kupanda na kushuka jumla unakuwa umetembea kilometa 38.