Safari yetu wana JamiiForums Udzungwa Mountains National Park, Mwanihana Peak na Sanje Waterfalls

Safari yetu wana JamiiForums Udzungwa Mountains National Park, Mwanihana Peak na Sanje Waterfalls

View attachment 2443943

Noela Shoo ni binti mdogo kwa umbo lakini she is so tough in action. Wadada na wamama Tunaopenda hiking tumekuwa tukiongozwa mara nyingi na wanaume, na kama ujuavyo changamoto zinazokabili mbuga na hifadhi zetu, vyoo ni mpaka ukute camp, kwa hiyo ukiwa njiani huwi comfortable sana.

This weekend from Thursday to Sunday nilikuwa nimeenda na Mr. Husband na baadhi ya wana JamiiForums wenzangu mbugani kidogo, kuvuta hewa ya baridi.

Tulichagua kwenda Udzungwa National Park ambapo tungeweza kuona wanyama, kufanya hiking (kupanda milima mirefu) na kutembelea maporomoko ya maji.

Safari yetu ilikuwa nzuri na tukaanza safari ya mlimani siku ya Alhamis hiyohiyo saa kumi jioni.

Safari yetu ilikuwa ya wabeba mizigo kadhaa, mizigo yangu na husband ilibebwa na WAGUMU Frank Mathias Pulapula na MGUMU Gaudence Williams, wana JF wengine pia walikuwa na wapagazi wao, wakitaka kuonesha shukrani na kuwathamini mchango wao watafanya hivyo kwa wakati na nafasi zao binafsi.

Pia tulikuwa na ranger, kijana wa Kichagga kutoka Rombo, kijana mkakamavu Peter Swai (Ismail) na binti kiongozi wa msafara na muongoza watalii Noela Shoo.

Siku hiyo ya Alhamisi tulianza safari ya kupanda kilele cha MWANIHANA kwa kupitia maporomoko ya Sonjo, kisha tukaelekea eneo la kupumzika, wenyeji wanapaita shell.

Hili ni eneo ambalo mto unapita na pana mawe mawe, makubwa kwa madogo yakiwapa wageni na wenyeji wao nafasi ya kupumzisha miili, kunywa maji, kujilowanisha na kuchota maji ya kunywa njiani.

Tukaendelea kwenda mdogo mdogo huku tukipanda milima na vilima hadi kulifikia eneo la MIZIMU. Hapa pana mto unapita na pana miti mirefu sana. Pia pana kidaraja cha chuma. Hapo tukapumzika na kupiga picha, tukanywa maji tena na kuchota mengine. Hapa tulifika saa 12 kasoro.

Baada ya hapo safari ikaendelea kuitafuta camp ya GMP ambapo tungepiga kambi, kupika, kula na kulala.

View attachment 2443979
Hapa camp GMP tulifika saa mbili kasoro kumi usiku tukiwa na mahema yetu, nguo na vyakula.

Usiku huo tulikuta kambi imefurika watu wengi waliokuwa wanatengeneza njia kwa ajili ya watalii wanaoenda Mto Rumemo na Rumemo Peak.

Hapa tulitengeneza chakula laini, mikate, mayai, siagi, matunda na chai ya masala. Pia tulikula nuts mbalimbali, karanga, korosho na almonds.

Asubuhi WAGUMU hawakuwa tena na kazi ya kutubebea mizigo, safari yao ilikomea GMP CAMP. Wagumu walitusongea ugali ambao tulikula na mayai ya kukaanga yaliyochanganywa na nyanya, pia tulikula samaki, na mtindi. Baada ya mlo safari ya kilometa 7 kupanda milima kwenda Mwanihana Peak ikaanza.

TAREHE 09.12.2022. SAFARI KUTOKA GMP CAMP TO MWANIHANA PEAK.
Tuliondoka GMP CAMP saa moja na dakika 37 asubuhi, huku tukiwaacha WAGUMU hapo camp wakipumzika na wakituandalia chakula cha usiku, ili tukishuka kutoka mlimani tule, tulale na kesho yake asubuhi tushuke Mang'ula Mwaya kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kwenda Sanje Waterfalls kesho yake.

Tulianza safari yetu kwa kuvuka kijito kilichopo kandokando ya camp, tukachota maji ya kunywa hapo maana hiyo ndiyo LAST WATER POINT, huko mbele hamna tena maji.

Baada ya kuchota maji, tukaanza mdogo mdogo kupanda milima huku tukisindikizwa na sauti mbalimbali za ndege. Muongoza watalii wetu Noela Shoo alikuwa ni mahiri wa kututajia majina ya ndege tunaowaona. Aliwataja kwa majina ya Kiswahili, ya Kingereza na ya Kibaiolojia. Pia alitutajia sifa za ndege hao.

Mwingoni mwa ndege niliovutiwa nao sana alikuwa ni Hondo hondo.
View attachment 2444429
Noela alitueleza kwamba hondo hondo joke anapoanza kulalia/kuatamia mayai, basi hujinyonyoa manyoya yake yote mwilini, na huyapanga sehemu anayotarajia watoto watakaa.

Dume lina jukumu la kuijenga hiyo nyumba/ kiota na mifumo yake yote ikiwa ni pamoja na choo.

Baada ya hapo dume husiliba kiota chote kwa matope na kuacha tundu sehemu ya mdomo tu. Ambapo dume atawajibika kumletea mkewe matunda 150 kila siku.

Jike ataendelea kukaa bila manyoya hadi atakapo angua mayai yake na atakaa katika hali hiyo hadi watoto wake wakianza kuota manyoya ndio naye manyoya yake yataanza kuota.

Manyoya ya watoto wake yakikomaa na manyoya ya mama huwa yamekomaa na huo ndio huwa mwisho wa maisha ya kiotani.

Ikitokea baba hondo hondo ameuawa kwenye hekaheka za kutafuta chakula cha mkewe na watoto, basi huo ndio utakuwa mwisho wa familia. Kwani mama huwa hana manyoya wala uwezo wa kuruka na anakuwa amefungiwa kiotani.
Mlinyanduana tena kama siku Ile mmeona papa?
 
Nshapanda sana huko Swimming Kwa sana pale Sonjo Falls na Prince Bernard falls, Vipi hukwenda Sanje mangabey trekking njia Njokomoni, Raha sana Udzungwa.
Hakuchoshi aisee
 
Nilitegemea picha nyingi kunishawishi
hata kumpa pongezi tu umeshindwa umekimbilia kulilia picha utadhani ulimlipa.

hongera sana mwanadada mleta mada kwa kufanya hiking milima ya udzungwa. uzi mzuri sana.
 
Sawa twende Mlima Kilimanjaro na...
Mothercity safaris.com
 

Attachments

  • IMG-20221215-WA0063.jpg
    IMG-20221215-WA0063.jpg
    81.1 KB · Views: 9
  • IMG-20221215-WA0047.jpg
    IMG-20221215-WA0047.jpg
    54.8 KB · Views: 10
  • IMG-20221215-WA0052.jpg
    IMG-20221215-WA0052.jpg
    60.1 KB · Views: 10
  • IMG-20221215-WA0050.jpg
    IMG-20221215-WA0050.jpg
    51.4 KB · Views: 10
  • IMG-20221215-WA0051.jpg
    IMG-20221215-WA0051.jpg
    45.8 KB · Views: 10
  • IMG-20221215-WA0054.jpg
    IMG-20221215-WA0054.jpg
    47.2 KB · Views: 12
  • IMG-20221215-WA0053.jpg
    IMG-20221215-WA0053.jpg
    45.9 KB · Views: 9
  • IMG-20221215-WA0048.jpg
    IMG-20221215-WA0048.jpg
    67.6 KB · Views: 8
sintokaa tena nikapanda Milima udzungwa nilitaka kukata moto yanii milima unapanda non slop khaa ukikuta kislop basi ni kijimto kidogo unainukaa tena. na bara uanzie Getini kuliko sanje
 
Unaonaje ukianza Kuitangaz na ku arrange ili mwisho wa mwaka tunaopenda hiking na adventure hapa jukwaani tuichangamkie?
Mkuu Kampuni inapeleka wageni kila siku huko juu hii ya JF ni nzuri ngoja tutaiandaa moja nzuri hata ya mbugani pia huko Ngorongoro Crater season ya Ndutu Migration ni nzuri zaidi..
 
Mang'ula mang'ula hiyo, enzi hizo nakwenda huko lodge nzuri ilikuwa inaitwa Mountain Peak 🗻 kama sikosei..

Hivi ile barabara wameitia lami?
 
Back
Top Bottom