benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Tanzania na China zimekuwa na mahusiano ya muda mrefu, toka enzi zile za kufuata misingi mikuu ya Ujamaa chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Baba wa Taifa la China Mao Ze Dong.
Kwa miaka 61 sasa nchi hizi zimeendelea kushirikiana katika mambo kadhaa lakini zaidi ni namna asilimia kubwa ya wafanyabishara wanavyotegemea kuagiza bidhaa kutoka China kwa ajili ya soko la ndani ya Tanzania na nchi za jirani.
Tangu janga la Korona lilivokuja kuitikisa dunia hadi sasa sehemu kubwa ya "Supply" ya mizigo kutoka China kuja hapa Tanzania imekuwa ni ya kusuasua na chanzo kikubwa ni gharama kubwa za usafirishaji kwani mashirika mengi bado yamesitisha safari za kwenda nchini China
Leo tarehe 17 Julai 2022, Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limeanza rasmi safari za moja kwa moja (Direct flight) kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou, China katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Baiyun, safari zitakazofanyika kila Jumapili, hii ni fursa hii ni neema kwa wafanyabiashara ikitumika vizuri
Pamoja na kwamba Uhusiano wa Tanzania na China utaimarika zaidi hii ni fursa kubwa ya kuimarisha biashara kati ya nchi hizi ambayo thamani yake hadi kufikia mwaka 2020 ilikuwa ni zaidi ya Shilingi Trilioni 10.
ATCL iangalie namna ya kuweka gharama rafiki ili kuweza kulisha na kuhudumu uhitaji mkubwa uliopo wa kufikisha (Delivery) mizigo na huduma kutoka China. Wakati wengine wakiwa wamesitisha safari zao, huu ni wakati wa ATCL kusimika mizizi na kujiimarisha ili hali itakaporejea kawaida wao wawe tayari wametengeneza wateja wanaowaamini (Loyal Customers) kutokana na huduma watakazowapatia.
All in all ni mwanzo mzuri, tushikilie hapo.