Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizi zote ni ahadi hewa. Leo Agosti Pili hakuna cha Safari wala cha nini. Subirini Hadi January 2024.Safari zitaanza rasmi au ni majaribio tuu?
Siku wakiacha ibada za uongo ndo maendeleo yafaonekana
NAIBU WAZIRI ATUPELE MWAKIBETE ASEMA SAFARI ZA DAR - MORO KUPITIA RELI YA SGR KUANZA JULAI, 2023
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imepokea mabehewa sita ya reli ya kisasa ya (SGR) ambayo yamewasili kutoka nchini Ujerumani tayari kwa kuanza majaribio mwezi ujao. Naibu Waziri Mhe. Atupele Mwakibete awataka watanzania kuyatunza.
Mabehewa haya ni kati ya 30 ambayo yalitumika na kufanyiwa maboresho nchini Ujerumani, imeelezwa kuwasili kwake ni kiashiria cha kuanza kwa safari za reli kati ya Dar hadi Morogoro.
Akipokea mabehewa hayo Naibu Waziri Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete amesema ameridhishwa na hali ya mabehewa hayo ambayo kwa mara ya kwanza kwenye historia ya reli yameonekana nchini.
Naibu Waziri Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete amesema kinachosubiriwa sasa ni kuwasili kwa kichwa kitachovuta mabahewa hayo ambacho kinatarajiwa kuwasili nchini Julai mwaka huu.
Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Ameeleza kuwa mabehewa hayo ambayo ni ya ghorofa, manne kati yake yana uwezo wa kubeba abiria 120 kila moja na mengine mawili yakibeba abiria 140 kila moja.
“Haya mabehewa yalinunuliwa yakiwa yametumika ila yamefanyiwa marekebisho kwa zaidi ya asilimia 80 na yamekuwa bora pengine sawa na mapya" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi
"Tunatarajia kuanza majaribio mara baada ya kichwa kuwasili mwezi ujao na hilo likikamilika tutaanza rasmi safari za kipande cha kwanza cha Dar- Moro" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Amina Lumuli amesema mabehewa mengine 24 yatawasili nchini Agosti huku kichwa cha pili cha umeme kinatarajiwa kuwasili Novemba.
InawezekanaHii kitu unaweza ukashangaa mpaka 2030 ikawa Bado haijaanza