Ishu ya kupigana sio nzuri kwani inadhalilisha sana utu wa mtu, ingawa ni vigumu sana kuvumilia kejeli na vibweka vya nyumba ndogo, lakini mfano alioutoa AshaDii na wengine, ni wa kuigwa. ni vyema kukaa kimya, lazima mume atashtakiwa na dhamira, sijui awe na moyo wa ajabu kiasi gani.
Nilichoeleza hapo ni mojawapo ya vyanzo vinavyoasisisiwa na wanawake katika kuwasindikiza waume zao kwenye nyumba ndogo, lakini pia labda niseme tu kuwa pale ambapo akili ya mwanamke imeng'ang'ania kwamba "lazima mume wangu ana nyumba ndogo". Na akaamini hivyo ni dhahiri hilo litatokea kwa sababu umemjengea akili hiyo........ Naamini wengi wanafahamu kuwa kauli huumba, na sio kauli tu bali pia hata ile kuwaza tu, jambo linaweza kutokea. kwani kila tunalowaza linaingia katika akili zetu za kina na kufanyiwa kazi.
Mwanamke,.......... Jenga kujiamini, muamini mumeo kwani alikupenda na ndio maana akakuoa, acha Ghubu kwani ghubu ni adui mkubwa sana katika uhusianao na sio katika ndoa tu bali pia uhusiano wako na jamii iliyokuzunguka unakuwa wa mashaka.