Safari za wanaume kuelekea nyumba ndogo zinavyoanza…….!

Safari za wanaume kuelekea nyumba ndogo zinavyoanza…….!

Kila la heri katika safari yenu, maana wengine hata mfanyiwe vipi akili zenu zishajijenga kuwa bila nyumba ndogo maisha hayaendi..
 
Ishu ya kupigana sio nzuri kwani inadhalilisha sana utu wa mtu, ingawa ni vigumu sana kuvumilia kejeli na vibweka vya nyumba ndogo, lakini mfano alioutoa AshaDii na wengine, ni wa kuigwa. ni vyema kukaa kimya, lazima mume atashtakiwa na dhamira, sijui awe na moyo wa ajabu kiasi gani.
Nilichoeleza hapo ni mojawapo ya vyanzo vinavyoasisisiwa na wanawake katika kuwasindikiza waume zao kwenye nyumba ndogo, lakini pia labda niseme tu kuwa pale ambapo akili ya mwanamke imeng'ang'ania kwamba "lazima mume wangu ana nyumba ndogo". Na akaamini hivyo ni dhahiri hilo litatokea kwa sababu umemjengea akili hiyo........ Naamini wengi wanafahamu kuwa kauli huumba, na sio kauli tu bali pia hata ile kuwaza tu, jambo linaweza kutokea. kwani kila tunalowaza linaingia katika akili zetu za kina na kufanyiwa kazi.

Mwanamke,.......... Jenga kujiamini, muamini mumeo kwani alikupenda na ndio maana akakuoa, acha Ghubu kwani ghubu ni adui mkubwa sana katika uhusianao na sio katika ndoa tu bali pia uhusiano wako na jamii iliyokuzunguka unakuwa wa mashaka.
 
Mkuu Mtambuzi, I like your analysis

Hivi na siye wanaume tunakuwaga na GHUBU?
 
lakini yataka moyo si kidogo!kuogopa kupigania kilicho chako is it easy na sisi ni binadamu? Nakubali hata wake wanachangia kumshawishi mume kutafuta pumziko. Shida ni kitchen party zisivyo na tija katika kumuandaa binti.

kitchen party kwa sasa ni fashion hazina maudhui
 
Sweetie... kuna member hapo juu anauliza hapo....

lol babe...mi nilikuwa nauliza upande wa wanaume....hivi nataka nijue kama linakuwepo,,,member anauliza kwa ujumla kuhusu Gubu unaweza kumsaidia love?
 
Yataka moyo, ila kama alivosema asha na kingasti kwa kweli ukimya unalipa sana , maana atakuja mwenyewe kugundua anakosea wapi, mie huwa naangalia vitu vidogo kwa kweli kwa mahusiano yetu haya ya kibongobongo, anafanya majukumu yake kama mume, ananipenda kwa dhati? .....mengine naacha kama yanavojiri....kuna wakati unapitaga kwenye mahusiano ni mgumu sana sana ila Mungu anasaidia tu, na ajabu ule wakati ukipita tunasahau kabisa machungu yake
 
Mkuu Mtambuzi, I like your analysis

Hivi na siye wanaume tunakuwaga na GHUBU?
tena usiombe kushuhudia gubu la mwanaume, huwa linakera coz huwezi kuwalk away kama yeye , mwanamke ukiwa na gubu, mume anaweza kukuepuka kwa kuchelewa kuja, akirudi kalewa unaongea yeye anajilalia zake, asubuhi kaondoka, sasa yeye akiwa nalo, unadeal nalo mwanzo mwisho, ataongea weeeeee na madharau juu, nimeshuhudia ndugu wenye waume wenye gubu mmoja ameshindwa kajiondokea
 
Tendo la uzinifu haliko justifiable hata kidogo.......................swali na wanaume je kama ni makelele na ghubu na sisi twende tafuta pumziko

Pia sio wote wenye nyumba ndogo wake zao wana kelele na ghubu basi ni kutokuwa na utu ,huruma na zaidi hofu ya Mungu.

Personally naomba yasinikute na yakitokea naomba Mwenyezi Mungu anipe Busara na haki
 
Mkuu Mtambuzi, I like your analysis

Hivi na siye wanaume tunakuwaga na GHUBU?

Mbona hata makazini na kwenye vikao vya Kahawa na Pombe tunawaona..... wapo wengi tu tena wa kutosha kaka.......... Tena usiombe kuwa na Bosi au mfanyakazi mwenzio mwenye Ghubu, utaacha kazi mwenyewe...........
 
Personally naomba yasinikute na yakitokea naomba Mwenyezi Mungu anipe Busara na haki

Hata mie nakuombea sana uwe na Busara.............Wanaume wengine huharibikia ukubwani kama ulikuwa hujui.........
 
jibu ni kukaa kimya tu, mwisho wa siku atajisikia vibaya
 
Napita tu naona hii mada imewalenga kinamama zaidi.
 
laiti wanawake wangejua....
Hakuna kitu kinachotisha kama mwanamke anapokaa kimya kabisa
huku unajua umemtendea visivyo.....

Her silence speaks so loud.....
yes, so loud
 
Back
Top Bottom