Safaricom Kenya yaomba ulinzi kwa Serikali. Ni baada ya Starlink kushusha bei hadi Tsh. 26,000/= kwa GB 50

Safaricom Kenya yaomba ulinzi kwa Serikali. Ni baada ya Starlink kushusha bei hadi Tsh. 26,000/= kwa GB 50

Monopolies ni tatizo, zinatapeli wananchi.

Kampuni moja kumiliki asilimia kubwa ya soko haijawahi kuwa salama.

Israel wananchi walikuwa wanalalamika sana internet ni ghali, akaja huyo waziri mmoja akalegeza masharti ya kuanzisha ISPs, washindani wakawa wengi, bei zikashuka.

Kuna nchi zilizoendelea zina internet nafuu kuliko sisi yaani.
simu zangu nyingi kutwa natumia WhatsApp asilimia kubwa...huwezi amin watanzania wanabip hadi WhatsApp.
Kuna homie yupo Burundi bando la mwezi hata elfu ya 10 ya Tanzania haifiki na anamaliza mwezi na hiyo Bando.

NAPE alikuwa anakunja mkwanja mrefu toka kwa makampuni ya Simu ili asiruhusu ujio wa Starlink Tanzania.
 
Baada ya Starlink kushusha bei ya plans zake na kuintroduce kifurushi cha Ksh. 1,300 ambayo ni sawa na kama Tsh. 26,000 za kitanzania kwa 50GB kwa mwezi na plan ya Tsh. 400 kwa GB 1 (20KES) pale ambapo utamaliza kifurushi hicho kabla ya mwezi kuisha.

Kampuni ya mawasiliano ya Kenya Safaricom imetoka hadharani na kuomba Serikali ya Kenya kujitokeza na kuregulate bei hizo maana zitaharibu soko lao local providers

Ikumbukwe kuwa Safaricom na mitandao mingine vifurushi vyao vya bei ya chini kabisa ni Tsh. 50,000 kwa GB 45 kwa mwezi, hii ikiambatana na speed ndogo ya internet ukilinganisha na ile ya Starlink.

Pia kampuni hii ya Starlink chini ya bwana mkubwa Elon Musk iliitikia kilio cha wengi na kushusha bei ya antenna zake na installation fee kwa zaidi ya 70%
Vodacom nao wajiandae, hatuwezi kuendelea kuibiwa kwa uzembe na manufaa ya watu wachache!!
 
Hata ukiwa hapa Tanzania unaweza kuunganisha hiyo Starlink na ukatumia fresh tu, na tayari kuna watu wanatumia starlink hapa Tz. Ni kinyume cha kisheria za Tz lakini nani anajali ikiwa sheria zenyewe ni kandamizi.
Kweli Mkuu?

Mchawi wa Watanzania ni Mtanzania mwenzetu hasa huyo aliyekataa starlink isifanye kazi Tanzania
 
Hata Malawi GB 1 ni chini ya Tsh 1000. Tanzania gharama ni kubwa sana, maeneo mengi spidi si ya kuridhisha, kiufupi wanatufanyia uhuni sana.

Hatari sana ,waziri wa mawasiliano na TCRA kimya wanakula commissions tu za MABEPARI kwa kuwaumiza walaji wa mwisho(Users) , Gharama za Internet ni kubwa sana halafu mtu ana subscribe kwa wiki inaisha kwa siku ,TRCA na Mwaziri wa Mawasiliano ebu angalieni bei za vifurushi vya internet ,ni ghali sana! Mbona Voice tumeweza? Kwanini kwenye internet tushindwe?
 
Back
Top Bottom