Safaricom Kenya yaomba ulinzi kwa Serikali. Ni baada ya Starlink kushusha bei hadi Tsh. 26,000/= kwa GB 50

simu zangu nyingi kutwa natumia WhatsApp asilimia kubwa...huwezi amin watanzania wanabip hadi WhatsApp.
Kuna homie yupo Burundi bando la mwezi hata elfu ya 10 ya Tanzania haifiki na anamaliza mwezi na hiyo Bando.

NAPE alikuwa anakunja mkwanja mrefu toka kwa makampuni ya Simu ili asiruhusu ujio wa Starlink Tanzania.
 
Vodacom nao wajiandae, hatuwezi kuendelea kuibiwa kwa uzembe na manufaa ya watu wachache!!
 
Hata ukiwa hapa Tanzania unaweza kuunganisha hiyo Starlink na ukatumia fresh tu, na tayari kuna watu wanatumia starlink hapa Tz. Ni kinyume cha kisheria za Tz lakini nani anajali ikiwa sheria zenyewe ni kandamizi.
Kweli Mkuu?

Mchawi wa Watanzania ni Mtanzania mwenzetu hasa huyo aliyekataa starlink isifanye kazi Tanzania
 
Hata Malawi GB 1 ni chini ya Tsh 1000. Tanzania gharama ni kubwa sana, maeneo mengi spidi si ya kuridhisha, kiufupi wanatufanyia uhuni sana.

Hatari sana ,waziri wa mawasiliano na TCRA kimya wanakula commissions tu za MABEPARI kwa kuwaumiza walaji wa mwisho(Users) , Gharama za Internet ni kubwa sana halafu mtu ana subscribe kwa wiki inaisha kwa siku ,TRCA na Mwaziri wa Mawasiliano ebu angalieni bei za vifurushi vya internet ,ni ghali sana! Mbona Voice tumeweza? Kwanini kwenye internet tushindwe?
 
Sisi huku nape alituambia jamaa amegoma kuweka ofisi za makuu hapa bongo. Huyu waziri wa Sasa hawezi kufanya kitu?
Unamjua mmiliki wa tigo tanzania?.
Hyo ni biashara za watu.hawawezi kukubali.tunapigwa na wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…