Asantehene
Member
- Nov 18, 2025
- 8
- 11
Wakuu,
Nimeona kampuni ya Safaricom wamekuja na mfumo mpya wa kuficha baadhi ya tarakimu kwenye namba za mtu anayetuma pesa, nadhani ni wazo zuri sana. Mfano, ukituma pesa, mpokeaji ataona namba kama 0754****00. Ikitokea ukitaka kujua namba nzima, wewe mpokeaji utalazimika kufoward huo muamala kwenda namba 334, yule aliyekutumia pesa ataona ombi lako la kutaka kufahamu namba zake. Akiridhia, atakutumia namba zake, asiporidhia anapotezea.
Kuna haja ya makampuni ya simu Tanzania kama Vodacom, Airtel na mengine kuiga ubunifu huu. Nadhani itasaidia si tu kuongeza faragha ya mtumaji wa pesa, lakini pia kudhibiti wale matapeli wa "tuma kwenye namba hii" kupata namba za watu kwa urahisi.
Nawasilisha.