Safarini NAIROBI kibiashara kwa Mara ya kwanza 🤔

Safarini NAIROBI kibiashara kwa Mara ya kwanza 🤔

kokudo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
2,571
Reaction score
1,760
Nipo njiani kulielekea jiji LA Nairobi nchini Kenya kibiashara ni kiri tu ndo mara ya kwanza kwenda nchi hii kibiashara

Tofauti na mara mbili nilizokwenda kwa shughuli nyingine na tulikwenda jumuia

Njia ni Sirari au Isibania

MWENYE UZOEFU NA NJIA HII LAKINI PIA JIJI HILO
 
Nenda kafanye uchunguzi na tafiti kwakweli ndio mji ambao Serikali yake imefungua biashara kwa watu wake.

Tunakusubiria kwa mengi kutoka huko tupate tofauti na kwenda China.
 
Nipo njiani kulielekea jiji LA Nairobi nchini Kenya kibiashara ni kiri tu ndo mara ya kwanza kwenda nchi hii kibiashara

Tofauti na mara mbili nilizokwenda kwa shughuli nyingine na tulikwenda jumuia

Njia ni Sirari au Isibania

MWENYE UZOEFU NA NJIA HII LAKINI PIA JIJI HILO
Trafiki wa Kenya sio kama wa TZ
 
Mkuu,Fanya biashara kwa umakini....wakenya usiwaamini ukampa mtu Hela yako kabla ya mzigo....au ukampa mzigo wako kabla ya Hela. Njia hiyo ni nzuri.
Isibania.
Migori.
Kisiii.
Kericho
Nakuru.
Narok.
Maimahiu
Hamna usumbufu kabisa.
 
Bidhaa kama simu ni cheap Nairobi kuliko Tanzania, hivyo inalipa kuzifuata huko
Ni kweli kwa nchi ambayo sarafu yake iko juu, panafaa sana kuwa sehemu ya soko; wao kupelekewa bidhaa, kwa mfano kwa mtu atakayefanikiwa kupeleka bidhaa ulaya na marekani, huyu ana nafasi kubwa ya kufanikiwa zaidi, kuliko yule anayetoa bidhaa kule na kuleta huku.​
 
Ukifika Nairobi. Kama utapata mda nenda Tembelea mji mmoja wa kibiashara apo unaitwa Isilii apo biashara ya Nguo Special kutoka uturuki zinafanyika na bidhaa mbali mbali.
Isilii imetoholewa kutoka Eastleigh. Ni kama vile Kariakoo iliyotokana na Carrier Corps; kambi iliyowekwa pale wakati wa vita vya kwanza ya Ulaya.😂
 
Back
Top Bottom