Said Bakhressa ana mchango wowote katika kuendeleza elimu?

Said Bakhressa ana mchango wowote katika kuendeleza elimu?

Fugwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
1,676
Reaction score
663
WanaJF,

Hakuna ubishi kwamba Billionia wetu mpendwa SAID BAKHRESSA a.k.a AZAM anamchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu na kwamba anangoza kulipa kodi, kwa hili anastahili pongezi.

Lakini nimejaribu kuchunguza katika Nyanja adimu na muhimu ya elimu, kwa upande wangu sikuona chochote kutoka kwa Bwana huyu, kama kuna mwenye taarifa kuhusu mchango wa Bw. Bakhresa kweye elimu dunia atujuze iwe bara au visiwani

Kwa uwezo wake wa kifedha tulitarajia natuone kwa mfano, AZAM UNIVERSITY OF TECHNOLOGY au AGRICULTURE n.k. Nimejaribu kuuliza wenyeji na majirani zake pale AZAM COMPLEX kama angalao amejenga hata shule ya msingi lakini majibu ya wenyeji ni kwamba ameweza kujenga Misikiti na ofisi ya Serikali ya Mtaa pale Chamazi Mwembe Bamia.

Jamani wenye ushahidi bandikeni hapa tusijekuwa tunamhukumu bure.
 
Analipa kodi . Hiyo tu peke yake inatosha, Swala la Elimu ni juu ya serikali yako sio Mzee SS Bakhresa

Hapana angekwenda zaidi kusaidia ukuaji wa elimu kwa kujenga mashule, vyuo, hata wakati mwingine hospital.

Hapa naona hata wenzake akina DEWJI hawana habari katika kuchangia maendeleo ya elimu
 
Mi nadhani ule ni msaada, tusiufanye kuwa ni haki yetu.

Kama yeye kasaidia kwenye sekta nyingine basi huku kwingine tujikakaue sie wengine au tuendelee kukabana na serikali yetu ituhudumie kutokana na kodi zetu tunazochanga.
 
Pale chamazi wenyewe wanaita AZAM complex kumejengwa msikiti mkubwa wa kisasa, ambapo kuna siku zimetengwa wanaohudhuria ibada huondoka na sh. 20,000/-, unaambiwa misikiti mingine kwa siku hizo hukosa waumini. Anyway ni jambo jema, lakini angekumbuka kuchangia maendeleo ya elimu ingekuwa vizuri pia

Ndomana wenye hekima waliwahi kusema ni vyema usimpe mtu samaki bali mfundishe kuvua samaki.
 
Mi nadhani ule ni msaada,tusiufanye kuwa ni haki yetu.Kama yeye kasaidia kwenye sekta nyingine basi huku kwingine tujikakaue sie wengine au tuendelee kukabana na serikali yetu ituhudumie kutokana na kodi zetu tunazochanga

hapo umenena ndugu yangu...sio huyo mpuuz aliekurupuka huko na kuanza kumpondea baba wa watu...
 
1. kwanza weka ushahidi kuwa anaongoza kwa kulipa kodi.

2. kuchangia elimu au chochote kile ni maamuzi yake. Yeye mwenyewe.

Kaishia la saba lakini kafikia hapo alipo anaajiri watu na analipa kodi. Sidhani ni haki kwa watu waliomzidi elimu kumdai michango yoyote, wakati wao wenyewe wenye kuanzia form four mpaka wenye PhD, hawana chochote cha kuonyesha.
 
hapo umenena ndugu yangu...sio huyo mpuuz aliekurupuka huko na kuanza kumpondea baba wa watu...

Tunachoangalia hapa ni mchango wa watu wenye uwezo kiuchumi kuwawezesha watu wa kawaida kunufaika na uwezxo wa kiuchumi walionao watu kama akina Bakhresa au dewji.

Bill Gate anachangia sana katika sekta za elimu na afya, na huenda hata wewe unayeniita mpuuzi umeshanufaika kwa namna moja au nyingine na michango ya bilionia huyu.

Kwa nini Azam asifanye kama huyo ili walala hoi waweze kufaidika na uwezo wake wa kiuchumi.

Nikwambie wewe ndio umekurupuka, umepewa kichwa ukitumie kufikiri vitu vyenye manufaa kwa jamii pana.
 
SUZA yampongeza Bakhresa na kutunuku Shahada ya Heshima Karume

IMG_0419.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohmed Shein,akimkabidhi zawadi Said Salum Bakhresa,kwa mchango wake mkubwa kukisaidia Chuo,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar leo.

img_0727.jpg

Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha SUZA,Simai Mohamed (kushoto)na Mfanya biashara maarufu Said Bakhresa na Dr Nariman Jidawi,walipompongeza kwa kupata zawadi kutokana na mchango wake mkubwa kwa SUZA,wakati wa mahafali ya 7 chuoni hapo.
 
Hehehe hata sijui niseme nini, Mbona unampangia mtu ? kwani lazima ? wewe hapo ulipo umefanya nini? hata chumba kimoja cha chekechea huwezi?
 
Binafsi siungi mkono lugha za kashfa ambao baadhi wanaandika hapa maana mleta mada huenda ni kweli ana kitu anataka kutueleza na wengine tunaweza tusimwelewe.
Ukweli ni kwamba mtu ambaye ana nafasi katika jamii akitokea hadharani na kuongelea kitu kwa msisitizo watu wengi huwa wanamsikiliza. Mfano ni kweli Azam akitoa msisitizo katika elimu, mazingira, kuondoa umasikini, usalama nk watumiaji wa bdidhaa zake mamilioni kwa mamilioni wanaweza kuwa na mwitiko mzuri tofauti na hya yakisemwa na mtu kama mimi.
Fuatilieni mada vizuri na jitahidi kuandika kwa lugha za staha ili wengine tuelewe pia.
 
Tunachoangalia hapa ni mchango wa watu wenye uwezo kiuchumi kuwawezesha watu wa kawaida kunufaika na uwezxo wa kiuchumi walionao watu kama akina Bakhresa au dewji. Bill Gate anachangia sana katika sekta za elimu na afya, na huenda hata wewe unayeniita mpuuzi umeshanufaika kwa namna moja au nyingine na michango ya bilionia huyu. Kwa nini Azam asifanye kama huyo ili walala hoi waweze kufaidika na uwezo wake wa kiuchumi. Nikwambie wewe ndio umekurupuka, umepewa kichwa ukitumie kufikiri vitu vyenye manufaa kwa jamii pana

mkuu sijuhi kama uliwahi kusikia kwamba makampuni yana wajibu wa kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii inayochangia hiyo faida? (wenyewe wanasema-cooperate social responsibility) .nadhani mtoa mada anayo hoja.
 
1. kwanza weka ushahidi kuwa anaongoza kwa kulipa kodi.
2. kuchangia elimu au chochote kile ni maamuzi yake. Yeye mwenyewe kaishia la saba lakini kafikia hapo alipo. Anaajiri watu na analipa kodi. Sidhani ni haki kwa watu waliomzidi elimu kumdai michango yoyote, wakati wao wenyewe wenye kuanzia form four mpaka wenye PhD, hawana chochote cha kuonyesha.

Gmali, hapa umepiga fyongo, kati ya watu waliopewa tuzo kwa kulipa kodi tena bila usumbufu ni huyu Azam.

Kuchangia elimu ni maamuzi yake lakini kumbuka matajiri bado wana jukumu la kusaida jamii maskini ili ziweze kuinuka kimaisha, comments zako zinaashiria ubinafsi uliokithiri ambao kwa dunia ya sasa ya wapenda maendeleo hauna nafasi.

Acha fikra za ubinafsi.
 
samahani by fungwe. nimekunukuu kimakosa. nilitaka kumnukuu ndugu yangu masai dada.
 
kwa elimu 3 % hata kama watu wanamtetea hapa! Bora mengi kasaidia kujenga shule kama visitation girls na madawati kwenye shule lukuki
 
Binafsi siungi mkono lugha za kashfa ambao baadhi wanaandika hapa maana mleta mada huenda ni kweli ana kitu anataka kutueleza na wengine tunaweza tusimwelewe.
Ukweli ni kwamba mtu ambaye ana nafasi katika jamii akitokea hadharani na kuongelea kitu kwa msisitizo watu wengi huwa wanamsikiliza. Mfano ni kweli Azam akitoa msisitizo katika elimu, mazingira, kuondoa umasikini, usalama nk watumiaji wa bdidhaa zake mamilioni kwa mamilioni wanaweza kuwa na mwitiko mzuri tofauti na hya yakisemwa na mtu kama mimi.
Fuatilieni mada vizuri na jitahidi kuandika kwa lugha za staha ili wengine tuelewe pia.

Wakubeza tuwaache wabeze lakini mtu kama AZAM ni muhimu sana katika ustawi wa nchi hii.

Tuangalie ni wangapi wanaishi kwa kutegemea juhudi alizofanya huko nyuma?? sasa juhudi zilezile azielekeze pia kwenye sekta ya elimu ili watu wengi waendelea kustawi.

Kumbuka MUNGU anapokujaalia hana maana unufaike peke yako bali na wengine. Asante kwa mchango wako
 
Hehehe hata sijui niseme nini, Mbona unampangia mtu ? kwani lazima ? wewe hapo ulipo umefanya nini? hata chumba kimoja cha chekechea huwezi?

Unijui kwa hiyo mchango wangu katika elimu pia huwezi kuujua
 
SUZA yampongeza Bakhresa na kutunuku Shahada ya Heshima Karume

IMG_0419.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohmed Shein,akimkabidhi zawadi Said Salum Bakhresa,kwa mchango wake mkubwa kukisaidia Chuo,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar leo.

img_0727.jpg

Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha SUZA,Simai Mohamed (kushoto)na Mfanya biashara maarufu Said Bakhresa na Dr Nariman Jidawi,walipompongeza kwa kupata zawadi kutokana na mchango wake mkubwa kwa SUZA,wakati wa mahafali ya 7 chuoni hapo.

Hiki sasa ndicho nilichokitaka, kumbe mwenzetu hakulala pia katika elimu, mliokuwa mnachonga mmeona?

Kwa upande wangu sikuwa na ushahidi. Tunawaomba waliokaribu nae wamshauri awekeze kwa nguvu katika elimu kwa kujenga shule na vyuo.

Hongera BILIONEA WETU.
 
Back
Top Bottom