Said Bakhressa ana mchango wowote katika kuendeleza elimu?

Said Bakhressa ana mchango wowote katika kuendeleza elimu?

It is GROUP OF COMPANIES and not THE MINISTRY OF EDUCATION...know the difference young chap..!
 
Wanao kila asubuhi wanaenda na juice ya embe shuleni bado tuu huo sio mchango? acheni hizo wewe umechangia nini kwanza kabla ya kumrukia mzee wa watu?
 
Tunachoangalia hapa ni mchango wa watu wenye uwezo kiuchumi kuwawezesha watu wa kawaida kunufaika na uwezxo wa kiuchumi walionao watu kama akina Bakhresa au dewji. Bill Gate anachangia sana katika sekta za elimu na afya, na huenda hata wewe unayeniita mpuuzi umeshanufaika kwa namna moja au nyingine na michango ya bilionia huyu. Kwa nini Azam asifanye kama huyo ili walala hoi waweze kufaidika na uwezo wake wa kiuchumi. Nikwambie wewe ndio umekurupuka, umepewa kichwa ukitumie kufikiri vitu vyenye manufaa kwa jamii pana

hahahahahaaaaaaaa.....duuuuhhh....wabongo noma....eti kabsaaaaa.....unang'ang'ania mali ya mwanaume mwenzio....tafuta yako nawe utoe...usilalie mlango waz cha mwenzio...ndomana hamwendelei kwa kupenda misaada....na msaada sio lazma kijana...nyie mmemwona azam tu...wengine hamuaoni
 
Said Bakhressa Institute of Industrial Engineering (SABAIIE) coming soon, though yet to be confirmed.

Stay tuned for more update.
 
Kwan Bakresa ndo serikali ye2? Swala la elimu n serikali kama imeshndwa bas. Mwachen m2 wa wa2 afurahie maisha yake.
 
Nchi hii watu wengi huwa wanatoa misaada kwa ajili ya sekta mbali mbali sema si kila mmoja anapenda kupiga tarumbeta akishasaidia!

Tunafahamu mtu kama Baba Wawili hata siku akipikia pilau walemavu basi hiyo ndo itakuwa habari kwenye media zake, wengine tabia hiyo hawana wanatoa kimya kimya!

Mfano mzuri ni hiyo post # 10 inayoonesha Dr. Shein akitoa tuzo kwa SSB kama ishara ya kuthamini mchango wake ndani ya SUZA!

Si ajabu kama si hiyo sherehe, wengi wasingefahamu kwamba SSB anaisaidia SUZA.
 
Nchi hii watu wengi huwa wanatoa misaada kwa ajili ya sekta mbali mbali sema si kila mmoja anapenda kupiga tarumbeta akishasaidia! Tunafahamu mtu kama Baba Wawili hata siku akipikia pilau walemavu basi hiyo ndo itakuwa habari kwenye media zake... wengine tabia hiyo hawana... wanatoa kimya kimya! Mfano mzuri ni hiyo post # 10 inayoonesha Dr. Shein akitoa tuzo kwa SSB kama ishara ya kuthamini mchango wake ndani ya SUZA! Si ajabu kama si hiyo sherehe, wengi wasingefahamu kwamba SSB anaisaidia SUZA.

Ni kweli kabisa. Halafu kumbuka Bakharesa ni moja ya watu ambao hawapendi makuu kabisa.

Mambo ya kutoa misaada halafu unapiga picha kwa Muislam safi na hata Mkristo makini hawez kufanya. Hivyo siyo lazima anapotoa misaada aje atangaze kama unavyota mtoa uzi.

Kutoa ni moyo na ni baina ya mtoaji na Mungu wake. Hayo mambo ya kujionyesha wengine hawayapendi.
 
WanaJF,

Hakuna ubishi kwamba Billionia wetu mpendwa SAID BAKHRESSA a.k.a AZAM anamchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu na kwamba anangoza kulipa kodi, kwa hili anastahili pongezi.

Lakini nimejaribu kuchunguza katika Nyanja adimu na muhimu ya elimu, kwa upande wangu sikuona chochote kutoka kwa Bwana huyu, kama kuna mwenye taarifa kuhusu mchango wa Bw. Bakhresa kweye elimu dunia atujuze iwe bara au visiwani

Kwa uwezo wake wa kifedha tulitarajia natuone kwa mfano, AZAM UNIVERSITY OF TECHNOLOGY au AGRICULTURE n.k. Nimejaribu kuuliza wenyeji na majirani zake pale AZAM COMPLEX kama angalao amejenga hata shule ya msingi lakini majibu ya wenyeji ni kwamba ameweza kujenga Misikiti na ofisi ya Serikali ya Mtaa pale Chamazi Mwembe Bamia.

Jamani wenye ushahidi bandikeni hapa tusijekuwa tunamhukumu bure.

anaajiri wasomi nao ni mchango
 
mkuu sijuhi kama uliwahi kusikia kwamba makampuni yana wajibu wa kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii inayochangia hiyo faida? (wenyewe wanasema-cooperate social responsibility) .nadhani mtoa mada anayo hoja.

Mbona akina Manji hamuwaulizii au kwa kuwa wanawagaiya kwenye mipira?

By the way hiyo ni Corporate na siyo cooperate.
 
Tunachoangalia hapa ni mchango wa watu wenye uwezo kiuchumi kuwawezesha watu wa kawaida kunufaika na uwezxo wa kiuchumi walionao watu kama akina Bakhresa au dewji. Bill Gate anachangia sana katika sekta za elimu na afya, na huenda hata wewe unayeniita mpuuzi umeshanufaika kwa namna moja au nyingine na michango ya bilionia huyu. Kwa nini Azam asifanye kama huyo ili walala hoi waweze kufaidika na uwezo wake wa kiuchumi. Nikwambie wewe ndio umekurupuka, umepewa kichwa ukitumie kufikiri vitu vyenye manufaa kwa jamii pana

Mtoa mada naona anakurupuka tu,,,afu sio lazima Serikali yako ndio inatakiwa ifanye hivyo kwenye sekta ya Elimu na social service zote
 
Alitoa milioni 100 kujenga jengo la madarasa Benjamin Mkapa....nasikia zilitafunwa, jengo halijakamilika...
 
Mbona akina Manji hamuwaulizii au kwa kuwa wanawagaiya kwenye mipira?

By the way hiyo ni Corporate na siyo cooperate.

Nashukuru kwa kunisahihisha hiyo typing error.

Akina manji hatuwazungumzii kwa sababu post tunayochangia imemtaja bakhresa na sio manji au dewji.

Kuzungumzia wasiotajwa ni kwenda nje ya mada, ukianzisha uzi unaohusu wengine tutachangia lakini uzi huu unamuhusu bakhresa and not otherwise.
 
1. kwanza weka ushahidi kuwa anaongoza kwa kulipa kodi.
2. kuchangia elimu au chochote kile ni maamuzi yake. Yeye mwenyewe kaishia la saba lakini kafikia hapo alipo. Anaajiri watu na analipa kodi. Sidhani ni haki kwa watu waliomzidi elimu kumdai michango yoyote, wakati wao wenyewe wenye kuanzia form four mpaka wenye PhD, hawana chochote cha kuonyesha.
Hapo umenena Mkuu nadhani ambaye hajakuelewa atakuwa na utindio wa ubongo tu.......
 
Watanzania hivi ni nani katuloga? Ilitakiwa tukomae na serikali, tuishikie kidedea kwa njia zote tunazozijua ili ifanye majukumu yake ya elimu, afya etc lakini tunaenda kuwatwika majukumu hayo watu wasiyonayo wakati mhusika yupo tu analipa mabilioni kwa waganga njaa huko BMK.
 
Kwa taarifa za ndani ni kwamba ni vigumu sana kujua SSB kasaidia nini kwa sababu hana tabia ya kupiga tarumbeta anapotoa msaada.

Inasemekana hii huenda inatokana na mafunzo ya dini yake yanayomtaka muumini anapotoa asijitangaze wala kutaka sifa.

Hizi ni speculations tu na taarifa za watu mbalimbali walio karibu na duru za huyu bwana.
 
unajua mm binafsi naamini kuwa jf ni forum inayounganisha wasomi wenye uwezo wa kufikiria mambo mbalmbal kwa upambanuz na uyakinifu kwa kutumia busara stahiki.

Leo hii mtu anatoa mada ambayo kama ikijadiliwa vizuri mimi,ww na hata yy anaweza kunufaika kwa namna moja ama nyngne.

Badala yake watu wametawaliwa na ubinafsi, kebehi,ufedhuli na dharau.
Mtoa mada kauliza swali ambalo kama kuna ushahidi unaweza kuutoa.

Sijaona ktk post yake kama kuna sehemu katumia lugha ya kulalama.
Wallahi huu ni msiba (inna lillahi wa inna illahi raaj'un).

Tunatakiwa tutumie busara jamani ktk mambo ya msingi na yenye mashiko.
Una comments "changia", hauna basi we "pita" waache wachangiaji.
Kama mtoa mada kakosea basi we fanya kama una"PM" kumsahihisha sio kukebehi publicily.

Binafsi naipenda thread hii maana najua huyu SS B. kwa uwezo wake anaweza fanya mengi sana, kujenga shule,vyuo,kugharamia miundombinu mashuleni, n.k. ili jamii izidi kumtambua, kumkumbuka na kumuenzi.

Lakin km alishawah kufanya bac tunaomba evidence.
 
Back
Top Bottom