Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunachoangalia hapa ni mchango wa watu wenye uwezo kiuchumi kuwawezesha watu wa kawaida kunufaika na uwezxo wa kiuchumi walionao watu kama akina Bakhresa au dewji. Bill Gate anachangia sana katika sekta za elimu na afya, na huenda hata wewe unayeniita mpuuzi umeshanufaika kwa namna moja au nyingine na michango ya bilionia huyu. Kwa nini Azam asifanye kama huyo ili walala hoi waweze kufaidika na uwezo wake wa kiuchumi. Nikwambie wewe ndio umekurupuka, umepewa kichwa ukitumie kufikiri vitu vyenye manufaa kwa jamii pana
It is GROUP OF COMPANIES and not THE MINISTRY OF EDUCATION...know the difference young chap..!
Wanao kila asubuhi wanaenda na juice ya embe shuleni bado tuu huo sio mchango???achene hizo wewe umechangia nini kwanza kabla ya kumrukia mzee wa watu???
Unijui kwa hiyo mchango wangu katika elimu pia huwezi kuujua
Nchi hii watu wengi huwa wanatoa misaada kwa ajili ya sekta mbali mbali sema si kila mmoja anapenda kupiga tarumbeta akishasaidia! Tunafahamu mtu kama Baba Wawili hata siku akipikia pilau walemavu basi hiyo ndo itakuwa habari kwenye media zake... wengine tabia hiyo hawana... wanatoa kimya kimya! Mfano mzuri ni hiyo post # 10 inayoonesha Dr. Shein akitoa tuzo kwa SSB kama ishara ya kuthamini mchango wake ndani ya SUZA! Si ajabu kama si hiyo sherehe, wengi wasingefahamu kwamba SSB anaisaidia SUZA.
WanaJF,
Hakuna ubishi kwamba Billionia wetu mpendwa SAID BAKHRESSA a.k.a AZAM anamchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu na kwamba anangoza kulipa kodi, kwa hili anastahili pongezi.
Lakini nimejaribu kuchunguza katika Nyanja adimu na muhimu ya elimu, kwa upande wangu sikuona chochote kutoka kwa Bwana huyu, kama kuna mwenye taarifa kuhusu mchango wa Bw. Bakhresa kweye elimu dunia atujuze iwe bara au visiwani
Kwa uwezo wake wa kifedha tulitarajia natuone kwa mfano, AZAM UNIVERSITY OF TECHNOLOGY au AGRICULTURE n.k. Nimejaribu kuuliza wenyeji na majirani zake pale AZAM COMPLEX kama angalao amejenga hata shule ya msingi lakini majibu ya wenyeji ni kwamba ameweza kujenga Misikiti na ofisi ya Serikali ya Mtaa pale Chamazi Mwembe Bamia.
Jamani wenye ushahidi bandikeni hapa tusijekuwa tunamhukumu bure.
mkuu sijuhi kama uliwahi kusikia kwamba makampuni yana wajibu wa kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii inayochangia hiyo faida? (wenyewe wanasema-cooperate social responsibility) .nadhani mtoa mada anayo hoja.
Tunachoangalia hapa ni mchango wa watu wenye uwezo kiuchumi kuwawezesha watu wa kawaida kunufaika na uwezxo wa kiuchumi walionao watu kama akina Bakhresa au dewji. Bill Gate anachangia sana katika sekta za elimu na afya, na huenda hata wewe unayeniita mpuuzi umeshanufaika kwa namna moja au nyingine na michango ya bilionia huyu. Kwa nini Azam asifanye kama huyo ili walala hoi waweze kufaidika na uwezo wake wa kiuchumi. Nikwambie wewe ndio umekurupuka, umepewa kichwa ukitumie kufikiri vitu vyenye manufaa kwa jamii pana
Mbona akina Manji hamuwaulizii au kwa kuwa wanawagaiya kwenye mipira?
By the way hiyo ni Corporate na siyo cooperate.
Hapo umenena Mkuu nadhani ambaye hajakuelewa atakuwa na utindio wa ubongo tu.......1. kwanza weka ushahidi kuwa anaongoza kwa kulipa kodi.
2. kuchangia elimu au chochote kile ni maamuzi yake. Yeye mwenyewe kaishia la saba lakini kafikia hapo alipo. Anaajiri watu na analipa kodi. Sidhani ni haki kwa watu waliomzidi elimu kumdai michango yoyote, wakati wao wenyewe wenye kuanzia form four mpaka wenye PhD, hawana chochote cha kuonyesha.